Butiku: Wazanzibar Msikubali Kurudia Uchaguzi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Taasisi ya mwalimu Nyerere imeitaka tume ya uchaguzi ya Zanzibar ZEC kufanya kazi kwa kuzingatia katiba ya nchi na sheria na sio kutanguliza mbele maslahi binafsi ya kisiasa hatua ambayo inaweza kusababisha machafuko na umwagaji wa damu.
 
Akizungumza na vyombo vya habari mjini Musoma, mkurugenzi mtendaji wa taasisi hiyo mzee Joseph Butiku, amesema amekerwa na tabia ya ZEC kusitisha uchaguzi na kushindwa kuwatangazia wananchi kiongozi wao waliomchagua, huku ikishindwa kuheshimu matakwa ya wananchi waliopiga kura katika visiwa vya Zanzibar.
 
Aidha mzee Butiku amewataka wananchi wa Zanzibar kutokubali tena kurudia upigaji wa kura hadi hapo yatakapotolewa maelezo ya kuridhisha na wahusika waliosababisha uchaguzi huo kufutwa pia waweze kuchukuliwa hatua kali za kisheria
 
Kwa sababu hiyo amewataka viongozi kuheshimu sheria na katiba ya nchi na kwamba chama ambacho kinadhani kimeshindwa katika uchaguzi huo kikubali matokeo badala ya kuifanya zanzibar ni mali ya chama fulani pekeee.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. sawa sawa mheshimiwa butiku kilichopo hapa na kinachotakiwa ni kuheshimu sheria na katiba ya nchi.tatizo lililopo zanzibar sasa hivi ni chanzo chake ni mtu mmoja, JAKAYA MRISHO KIKWETE andika hivyo na kisha baada ya muda na matukio tutakuja kugundua ukweli huu.baada ya dr ally mohamed shein kushindwa katika mbio za urais kwa mujibu wa mtiririko wa matokeo ulivyokuwa unaonyesha,dr shein aliwaarifu na kuwaita mhe.kikwete na pia rais mstaafu mkapa.baada ya majadiliano wakiwa wamemhusisha mwenyekiti wa zec jecha ndipo KIKWETE kama amiri jeshi mkuu wa jamhuri ya mungano wa tanzania akamwamuru jecha aandike barua ya kufuta matokeo ya uchaguzi wa kiti cha urais zanzibar.mimi nina imani rais ajaye anayeapishwa jumatano hii,mheshimiwa magufuli hatoukubali wizi huu uendelee kwa sababu utamharibia kazi na heshima na utamuingiza kwenye misukosuko mikubwa ndani ya tanzania na pia kuyaharibu kwa kiwango kikubwa mahusiano yetu na mataifa "yanayotulisha",yanayotusaidia kifedha bajeti ya nchi na misaada mikubwa ya kimaendeleo.na baada ya kulitatua hili la zanzibar kidogo-kidogo mheshimiwa magufuli ataanza"kuutafuta ukweli zaidi wa utawala wa aliyemtangulia,hususani matumizi mabaya ya ofisi".

    ReplyDelete
  2. upo sahihi umeongea,hongera.tuna imani mhe.kikwete atajirudi ili ajiepushe na aibu hii kubwa sana machoni pa mataifa na watu wengine mashuhuri wa kimataifa waliomheshimu sana.aelewe,baada ya kuapishwa mheshimiwa magufuli keshokutwa yeye[kikwete] atakua raia wa kawaida, hana sauti,kusikika wala mamlaka tena ya uamiri jeshi,labda kwa green guards wa ccm tuu ambao nao wakihalifu watakamatwa na majeshi yetu.staafu kwa heshima kikwete ,ukumbukwe kuliko kustaafu huku ukjiandaa kuchukuliwa hatua za kisheria .iangalie mamlaka ya dola,huwa haichelei kuchukua hatua,utakuja washangaa polisi, wale wale waliokua wakikupigia saluti "WAKIWA KAZINI,NYUMBANI KWAKO."

    ReplyDelete
  3. WEWE MSENGE NINI KUWAKATAZA WAZANZIBAR WASIRUDIE UCHAGUZI WEWE KAMA NANI

    MJINGA

    ReplyDelete

Top Post Ad