CHADEMA Yashinda Kesi......Mahakama Yatoa Kibali Mwili wa Marehemu Alphonce Mawazo Kuagwa na Kuzikwa

Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo Bonyeza Hapa
Taarifa kutoka Mahakama kuu kanda ya Mwanza zinaarifu kuwa Familia ya Alphonce Mawazo na Chadema wameshinda kesi dhidi ya Jeshi la Polisi ya kuzuia mwenyekiti huyo  wa Chadema Geita asiagwe  jijini Mwanza baada ya kuuawa kinyama kwa kukatwa mapanga 

Amri ya Jeshi la polisi kuwa Mawazo asiagwe Mwanza kwa kuwa kuna hofu ya kipindupindu imetupiliwa mbali na Mahakama hiyo. 

Mahakama hiyo iliyoketi chini ya Jaji Lameck Mlacha imetoa ruhusa mwili wa Alphonce Mawazo kuagwa jijini Mwanza na imeagiza Jeshi la Polisi kutoa Ulinzi siku hiyo lakini Ulinzi huo usivuke mipaka.

Sehemu ya hukumu ya kesi hiyo inasema "Kazi ya Polisi ni kulinda raia na si kuzuia mazishi.."
_________

 Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo na Makampuni Bonyeza HAPA

Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. dah! hii nchi kuna watu wanaoneana kuzikwa hadi mahakamani,au alikuwa mkimbizi?

    ReplyDelete
  2. wakubwa hao pia wanawasiliana na mungiu hawezi kufa na wakifa wataenda kuzikwa kwenye sayari ya marsi au pluto. unajua watu wanasahau mambo ya kifo. hawajui hii ndio sherehe ya mwisho ya ndg mawazo lkn haki hadi ipatikane mahakamani ili asherehekee sikukuu yake. Pole ndg mawazo najua huwezi kunijibu lkn jua kitu kimoja watu uliowaacha wanakukumbuka sana.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad