Jeshi la Polisi Lapiga Stop Maandamano ya Chadema Kupinga Matokeo ya Uchaguzi Mkuu, Chadema Yasema Maandamano yapo Pale Pale

Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo Bonyeza Hapa
Taarifa ya jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga kwa vyombo vya habari
Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga limezuia maandamano ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema) yaliyopangwa kufanyika Kesho Novemba 03,2015 katika mji wa Shinyanga kwa lengo la kupinga matokeo yaliyotangazwa na tume ya taifa ya uchaguzi katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25,2015.

Akizungumza na waandishi wa habari leo asubuhi kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga SACP Justus Kamugisha amesema wamezuia maandamano yaliyopangwa na Chadema kufanyika Novemba 03,2015 asubuhi akidai kuwa katika kipindi hiki hawaruhusu kufanyika kwa maandamano na mikutano kwa sababu jeshi la polisi limejikita katika kuangalia hali ya usalama utawale ili kusubiria kuapishwa kwa rais mteule na wabunge.
Amesema pia wamezuia mikusanyiko yoyote isiyo rasmi ambayo inaweza kuleta uchochezi na uvunjifu wa amani kwani kufanya hivyo ni kinyume cha sheria na watakaokiuka watachukuliwa hatua za kisheria.

Kamanda Kamugisha amesema Chadema wametoa taarifa kuwa Kesho wanataka kuandamana kupinga matokeo ya uchaguzi yaliyotangazwa na tume ya taifa ya uchaguzi uliofanyika Oktoba 25,2015 na baada ya kufanya maandamaano hayo wanataka kutoa ujumbe kwa serikali.
Amewashauri wananchi wote wa mkoa wa Shinyanga wasishawishiwe na viongozi wa vyama vya siasa,na kuwaomba wabaki majumbani,waendelee na shughuli zao na kutokubali kurubuniwa au kushawishiwa kuandamana kwani wanaowashawishi hawatakuwa mbele .

Katibu wa Chadema wilaya ya Shinyanga mjini George Kitalama amesema hawajapata taarifa wala maelekezo yoyote kuhusu kuzuiwa kwa maandamano yao na wanaendelea kujiandaa na wanachama wao kwa maandamano kama walivyopewa maagizo na viongozi wao wa kitaifa.
Amesema kesho 03.11.2015,watafanya maandamano ya amani kuanzia ofisi za Chadema wilaya kisha kuzunguka mji mzima wa Shinyanga kuanzia saa tatu asubuhi kupinga matokeo ya uchaguzi yaliyotangazwa na tume,na kwamba ni maandamano ya nchi nzima siyo Shinyanga pekee.
_________

 Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo na Makampuni Bonyeza HAPA

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mutatandikwa shauri zenu

    ReplyDelete
  2. Nitakuwa nachungulia,nikiona mr&mrs Lowasa wako mbele nami nitaandamana,kama hawapo nami nabaki nyumbani.

    ReplyDelete
  3. mfululizo wa maandamano haya ya ukawa utachukua jumla ya miaka mitano yaani siku 1865 kuanzia siku mheshimiwa magufuli atakapoapishwa.msingi mkubwa wa maandamano haya yasio na kikomo ni 1.kuyakataa matokeo ya kura ya urais 2.kuilaani kwa nguvu zote NEC chafu 3.kuyalaani matumizi ya nguvu na unyanyasaji vinavyofanywa na polisi 4.kushinikiza kuundwa kwa tume huru ya uchaguzi itakayokua wazi kwa vyama vyote na wanachi wapiga kura 5.kushinikiza madaftari ya wapiga kura yawe wazi na yasambazwe mikoani na wilayani nchini kote 6.mchakato wa kuipata katiba mpya uanze upya[ule wa warioba umeharibiwa na warioba mwenyewe-ameuuza kwa ccm .haya ni yetu wanachi wa kawaida na mengineyo mengi yatatolewa na viongozi wetu wa UKAWA.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Pia usisahau kuja na mkeo na watoto zako na familia yako yote muwe mstari wa mbele sie tutakua nyuma yenu

      Delete
  4. Ndio maana wengi tulishtuka mapemaaaaaaaaaa,chadema hamfai kupewa nchi,mnapanga
    maandamano wakati watoto wetu wanafanya mitihani?Mbaya zaidi asubuhi watu tuko makazini,kwani kuna haraka gani msingoje ijumaa jioni au jumamosi?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mshamba wewe na mkeo
      Nendeni nguzo nane mkanywe Walwa

      Delete

Top Post Ad

Below Post Ad