Mwili wa Mwanafunzi Mtahiniwa wa Kidato cha Mne Aliyesombwa na Mafuriko Waopolewa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 Miili ya watu wawili waliokufa maji baada ya kusombwa na mafuriko yaliyosababishwa na mvua zilizonyesha mwanzoni mwa wiki hii jijini Mwanza, ukiwamo wa mwanafunzi, imeopolewa kwenye mwalo wa Ziwa Victoria.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Charles Mkumbo, alisema miili iliyoopolewa ni wa mwanafunzi huyo wa Shule ya Sekondari ya Nyamanoro, Zainabu Shaaban (18) aliyekumbwa na mkasa huo wakati akienda kufanya mitihani taifa ya kidato cha nne na wa mwendesha bodaboda, Ibun Rashid.

Matukio hayo yalitokana na mvua hizo zilizonyesha Novemba 2, mwaka huu kwa saa tano huku zikiharibu miundombinu, mali na nyumba kujaa maji.

Mkumbo alisema miili hiyo iliopolewa kwa ushirikiano wa polisi na wananchi na kwamba ilikabidhiwa kwa ndugu kwa ajili ya maziko.

Awali, akizungumza nyumbani kwake, mama mlezi wa mwanafunzi huyo, Anastazia Alex alisema alitoka nyumbani akiwa na mwanafunzi mwenzake, Asnaty Ally kwenda shule na wakati wakivuka daraja aliteleza na kusombwa na maji.

Wakati wanatoka hapa (nyumbani) mvua haikuwa kubwa, ila waliondoka wamevaa nguo za nyumbani, zile za shule waliziweka kwenye mfuko ili zisilowane kabla hawajafika shuleni. Inasemekana aliteleza kwenye daraja akaanguka, akaanza kupiga yowe kuomba msaada,” alisema Alex.

Alisema kutokana na muda huo mvua kuwa iliendelea kunyesha, hakuweza kupata msaada hadi mwenzake alipokwenda kutoa taarifa shuleni.

Mkuu wa Sekondari ya Nyamanoro, Praxeda Kaijage alisema walipata taarifa hizo kwa mwanafunzi huyo baada ya kufika shuleni hapo.

Alisema baada ya kutoa taarifa kwa walimu, walianza kufuatilia kwa kushirikiana na familia yake. “Tulipewa taarifa na mwanafunzi mwenzake aliyekuwa naye (Asnaty) kuwa ameteleza kwenye daraja, akachukuliwa na maji, tulichukua hatua haraka kwenda eneo la tukio ila hatukuona kitu, tulifanya jitihada za kuwasiliana na familia tukawa tunamtafuta ila hatukufanikiwa,” alisema Mwalimu Kaijage.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Nyamanoro Kaskazini, Shija Salileje alisema waliitisha mkutano na kushirikiana kumtafuta mwanafunzi huyo kwenye mitaro hadi ziwani. Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilemela, John Wanga alisema licha ya kutoa boti mbili, waliagiza watendaji wa kata, mtaa na wenyeviti kumtafuta mwanafunzi huyo na kuhakikisha anapatikana.

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad