Chadema Bado Hawajakubali Yaishe...Waapa Kumshughulikia Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo Bungeni

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeahidi kumshughulikia Bungeni, Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo kikidai kuwa bado hajasafishwa kwenye kashfa ya akaunti ya  Escrow.

Ahadi hiyo ilitolewa juzi na Kaimu Katibu Mkuu wa Chadema Taifa, John Mnyika katika mkutano wa hadhara wa kampeni za Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Handeni, akimnadi Daudi Lusewa.

Alisema baadhi ya mawaziri, akiwamo Muhongo, bado hawajasafishwa na tuhuma za rushwa zilizosababisha wajiuzulu hivyo wajiandae kwani wabunge wa chama hicho wamejiandaa kumwangusha.

Mnyika alisema amemshangaa kuona Rais John Magufuli akimteua Muhongo kwenye Wizara ile ile alikopatia kashfa, iliyosababisha Rais mstaafu Jakaya Kikwete kumtema kwenye Baraza la Mawaziri.

“Hatukubaliani na uteuzi wa Profesa Muhongo na namhakikishia bungeni patachimbika,” alisema Mnyika ambaye ni Mbunge wa Kibamba, Dar es salaam.

“Hoja yetu ya kwanza tutakapoingia bungeni tu itakuwa kushinikiza Waziri huyu ajiuzulu maana bado hajasafishwa,” alisema Mnyika.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hivi Lowasa mlimsafisha vile??

    ReplyDelete
  2. Mnyika, sio lazima uongee, kama huna la kusema ni bora unyamaze, cdm mlizunguka nchi nzima na hilo FISADI NYANGUMI lenu mkiliombea kura, huku mkijua fika kwamba ni 'chafu'. Jiandaeni'kususa' na 'kutoka' bungeni kama kawaida yenu, lakini sio kumshungulikia Muhongo, jeuri hiyo HAMNA!!! MSHAISOMA NAMBA

    ReplyDelete
  3. magufuli kajiharibia sana kumteua huyu muhongo

    ReplyDelete
  4. nilichosikia katika pitapita wanadai huyo muhongo ndo msomi pekee wa hiyo idara ndo maana hawana jinsi so usishangae wanavyomtetea amewazidi usomi... sijui akifa watafanyaje.. nchi imejaa wasomi vilaza msomi wa ukweli ni mmoja tu pro muhongo ndo maana hatujali ufisadi wake.

    ReplyDelete
  5. Huyu muongo sijui mohongo
    kujiuzuru
    Alilazimishwa kujiuzuru
    Tena kwambinde
    Tena ana mdomo mchafu dharau ya kimsoma
    Kama kweli msomi angekaa huko huko ulaya
    Hana mpango wowote
    Mwizi tu huyu tunaye bungeni

    ReplyDelete
  6. kazi kwanza ngonjera badae.tutafuteni namna ya kuwasaidia wananchi sio kujadiri yalopita

    ReplyDelete

Top Post Ad