CHADEMA Fanyeni Mikakati kuimarisha Chama Acheni Siasa za Kutumia matatizo ya Watanzania

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Naamini viongozi wa CHADEMA wanafika hapa JF, lkn pia najua wanachama ana wafuasi wapo wengi hapa JF. Kwa muda mrefu CDM imetusaidia watanzania kutufumbua macho wakati ufisadi ukitamalaki. Yaliyopita si ndwele tigange yajayo.

Tangu uchaguzi umalizike CDM imekuwa ni chama cha matukio, kwa kizungu reactive to the incident. Tumeona CDM ilivyotumia msiba wa MAWAZO (MUNGU AMREHEMU) kwa sababu kama amekufa kwa sababu ya tofauti za kisiasa watanzania tunaelekea kubaya. Lakini CHADEMA kilitumia msiba huu kujipatia umaarufu km kwamba CHAMA CHA MAPINDUZI ndicho kiliwatuma waharifu kumuua kamanda MAWAZO, sitaki kuamini km CCM kama chama wana uwezo wa kufanya haya kwaani uchaguzi umeisha na walishinda kwa 95% kanda ya ziwa.
Kabla ya hili la mawazo CHADEMA walikuwa wanatafuta sympathy ya wananchi kwa kutumia kesi mbalimbali mfano ni kesi ya SHEKH PONDA aliyeshinda kesi hapo jana. Kuna wakati Fulani alikuwa akitetewa na wakiri maarufu wa CHADEMA pale Morogoro. Sijui kwa nini CDM waliingiliaje kesi hii kidogo wamuharibie mshitakiwa kwaani serikali ingeona kama vile alikuwa anatumiwa na CHAMA.

Jana baada ya kupata ushindi dhidi ya serikali niliona viongozi wote wa CDM wakiongozwa na aliyekuwa mgombea ubunge ndugu MARCUS ALBAN waliongoza waaumini kutoka eno la mahakama mpaka eneo la msikiti wa MUNGU MMOJA.
Wakati wa kampeni tuliskia aliyekuwa mgombea Urais kupitia CHADEMA Mheshimiwa Edward Lowassa kuwa kama angechukua dora basi angewaachia huru watuhumiwa mbalimbali wakiwamo Shekh Farid na Babu seya. Kwa kifupi kama hawana makosa wanastahili kuachiwa kwa mujibu wa sheria lakini siyo kwa mujibu wa matakwa ya mtu.

USHAURI KWA CDM NA UPINZANI:
Fanyeni vitu endelevu na vinavyoenekana, yaani sustainable and tangible la sivyo mtasahaulika, kumbukeni watanzania ni wepesi sana wa kusahau, jumrisha na kasi ya serikali ya awamu ya tano ambayo imezichukua sera za upinzania kuzifanyia kazi hasa ile ya ufisadi iliyotupwa baada ya kumpkea LOWASSA kitendo kilichoitwa na kubadili gear angani.

ACHENI KUTUMIA MATATIZO KATIKA JAMII KUTAFUTA UMAARUFU WA KISIASA.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

8 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Haki tena!kuna watu wanapinga kila kitu anachofanya Magufuli na timu yake hata kama ni kwa manufaa ya nchi kisa tu katoka CCM.sisi walala hoi tumepokea kwa mikono miwili maamuzi,na naamini wanaompinga ni wale matajiri ambao hata pamoja na utajiri wao hawana msaada kwa wananchi.kifo cha mawazo wamekivalia njuga na michango ya harakaharaka,bado kuna jamaa waliokaa ardhini siku 41 wakaenda kuonwa kisa tu kauliza kama Edo alishinda,lakini kuna watu wanaomba misaada wa matibabu kupitia vyombo vya habari,mbona hatuoni chadema wakachanga?Tuacheni ujinga,Tukubali Magufuli ni rais wetu,kikubwa ni kumpa ushauri kwani ni kiongozi ambae anafanyia kazi ushauri wa wananchi sana.

    ReplyDelete
  2. Kuna mmoja kati ya hawa nilimshuhudia kwa macho yangu kasimama sehemu na gari lake,wakaja ombaomba (WATOTO)kutaka msaada,hakutaka hata kuwasikiliza wala kuwapa chochote,badala yake alifunga mlango na kupandisha kioo.Kwani hakuwa na uwezo wa kusaidia wale watoto?au hata kuwahoji tu kwa lolote?Naamini ingekuwa ni wakati wa kampeni wale watoto wangekuwa kielelezo na mabango juu.Kumbe kwa nini tusiseme ilikuwa ni uroho wa madaraka ya kulinda madhambi yao na sio kwa maslahi ya wananchi?SHAME ON YOU.

    ReplyDelete
  3. Baadhi ya watanzania wameshawajua vizuri na wala haisumbui,na ni dhahiri CCM ikisumbua tena Watakaoshika dola ni ACT.Tusubiri.

    ReplyDelete
  4. I think they need to get over the fact they have lost, no need to pretend they are the good guys and work together with the elected government. by the look of it seems they want to create a shift between citizens pretending he (Lowassa) still has the power. I do remember clearly him saying once he lost he'll go back to his village to look after his cows, what happened to that?

    ReplyDelete
  5. Wapuuzi tu...kuna wangapi wameuwawa kinyama na wengine kupata matatizo makubwa hawakuwa mbele kuzika wala kuwasaidia...kwan walikuwa hawapo !!?sasa hivi wanataka kutangaza majina na kujitakasa FYUUU.

    ReplyDelete
  6. Wapuuzi tu...kuna wangapi wameuwawa kinyama na wengine kupata matatizo makubwa hawakuwa mbele kuzika wala kuwasaidia...kwan walikuwa hawapo !!?sasa hivi wanataka kutangaza majina na kujitakasa FYUUU.

    ReplyDelete
  7. Wapuuzi tu...kuna wangapi wameuwawa kinyama na wengine kupata matatizo makubwa hawakuwa mbele kuzika wala kuwasaidia...kwan walikuwa hawapo !!?sasa hivi wanataka kutangaza majina na kujitakasa FYUUU.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ushabiki wa vyama au Chuki dhidi ya mtu hautatusaidia Watanzania, tunachotakiwa kupambana nacho ni ISSUES AND FACTS. Hivi kwa mfano, Mawazo angekuwa ni ndugu yako wewe ungeona ni haki azikwe bila kuagwa na watu wake wa karibu? Mbona hata mtaaani kuna "Nzengo", Vikundi vya kufa na kuzikana, affiliation za aina mbalimbali n.k? Mwenyekiti wa Chama wa Mkoa ni Nafasi fulani kubwa ktk Jamii endapo utatizama bila kuwa na Negativity ya u vyama. Mahatma Gandhi aliwahi kuwashauri wahindi kuwa "INDIANS should not hate the British, rather the British COLONIALISM" Na ndio maana kwa mtazamo wangu, MFUMO anaoubomoa JPM ndio hasa tatizo wananchi ikiwemo vyama vya upinzani vimekuwa vikipigia kelele LAKINI hakukuwa na "TAASISI" wala "SERIKALI" iliyosikia kilio hicho kwa vile mfumo wote ulikuwa CORRUPT. Kwa sasa anachokifanya JPM ni CREATIVITY na COURAGE yake aliyojaliwa na MUNGU wake na Nina imani kama wembe huu utaendelea wengi WATALIA na KUSAGA meno na wengi watakaosalimika ni wale "WAPUMBAVU NA MALOFA"

      Delete

Top Post Ad