January Makamba Afunguka Akiri Rais Magufuli Ameipa Pumzi Mpya CCM

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, January Makamba amesema kasi ya utendaji inayooneshwa na Rais John Magufuli na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, imekipa uhai mpya chama chao na kwamba wanaCCM sasa wanatakiwa kutembea kifua mbele.

Akizungumza jana na mwandishi wetu Dar es Salaam, January alisema wakati wa kampeni CCM iliahidi itawaletea Watanzania mabadiliko na jambo hilo ndilo hasa linalofanywa na Magufuli na Majaliwa.

WanaCCM sasa wanatakiwa kutembea kifua mbele na kuwapongeza Magufuli na Majaliwa kwa kutoa matamko ya kuwaunga mkono kwa hatua wanazochukua. Wakati wa kampeni tuliahidi mabadiliko ya kweli. Na sasa tunaanza kuyaona,” alisema January na kuongeza:

“Tusikae kimya. Hii ni vita kali na naamini Watanzania wote wanamuunga mkono, lakini kwa kuwa anatekeleza ahadi ya CCM sisi tunapaswa kuwa mstari wa mbele kwa kumuunga mkono kwa maneno na matendo.

Tulipigana kufa na kupona ili tushinde na baadhi yetu tunaendelea kupokea vitisho na matusi kwa sababu ya kampeni kwa vile kwa wapinzani ushindani haujamalizika baada ya kumalizika kwa kampeni. "
 
Mbunge huyo wa Bumbuli mkoani Tanga na Naibu Waziri katika Serikali ya Awamu ya Nne, alisema kama mwana CCM na MNEC anajisikia fahari kwa vitendo vinavyofanywa na Magufuli kwa vile vimekipa chama pumzi na uhai mpya, akikumbusha maneno yaliyokuwa yakitumika na wapinzani kwamba chama hicho sasa kimeishiwa pumzi.

Lazima CCM ihakikishe Magufuli na Majaliwa wanafanikiwa katika uongozi wao. Hapo ndiyo nguvu iliyotumika katika kampeni itakuwa na maana. Kazi anayofanya Rais inakiletea chama pumzi na uhai mpya.

“Kwa mwendo huu, hakutakuwa na kazi ngumu katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 kama ilivyokuwa mwaka huu. Inawezekana wapo wanaCCM watakaoguswa na utendaji huu wa Rais, lakini hiyo ni gharama ndogo sana ya kulipa kwenye kuitafuta Tanzania ambayo kila mwananchi anaililia,” alisema.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. NILIICHUKIA CCM SANA,ILIBIDI NIJIUNGE NA UKAWA ILI HALI NIKIJUA UKAWA WAMESIMAMISHA RAIS AMBAE AMEINGIA CHADEMA KIMAGUMASHI,LAKINI MAGUFULI KANIFANYA NIJIONE NILIKUWA MWANA MPOTEVU.HAPA KAZI TU.

    ReplyDelete
  2. Huyu naye anatapatapa tu yaani akae kimya hana mvuto

    ReplyDelete
  3. Waandishi wengi mna fikra fupi.

    ReplyDelete
  4. Anaongelea akiwa Dar bila Shaka badala ya kwenda bumbuli kutatua matatizo ya watu wakati huu ni hapa kazi tu mdomo tupa kule

    ReplyDelete
  5. Pumzi ilikuwa imeisha, upinzani wamewaamsha

    ReplyDelete
  6. TULIMCHAGUA MAGUFULI KAMA MGOMBEA BINAFSI AMBAE HAKUWA NA KUNDI LOLOTE NDANI YA CCM. NI MGOMBEA PEKEE NDANI YA CCM ALIYEONYESHA KUKERWA NA KERO ZA WATANZANIA. NI MGOMBEA PEKEE ALIYEONA KAZI KUBWA ILIYOKO IKULU NA SI FAHARI KAMA AMBAVYO WENGI MLIFIKIRI MTAENDA KUCHEZA DISCO HUKO KAMA MLIVYOZOEA. BADO WEWE UTAKAPOULIZWA HELA ZA KUHONGA WASANII ULIZIPATAJE MAKE KWAKE HAIKUWA STYLE YAKE YA KAMPENI ZAIDI YA KUWAELEZA NIA YAKE YA DHATI YA KUITUMIKIA TANZANIA. UTAWALA WAKE SI WA KI CCM NDO MAANA NINYI HAO HAO NDO MNAISOMA NAMBA HASA WEWE MAKAMBA KWA KUSIMAMIA WIZARA YA MAWASILIANO NA NDO INAYOONGOZA KWA KUKWEPA KODI. TUNAKUSHANGAA UNAPOSEMA UTATEMBEA KIFUA MBELE HUKU ULISHINDWA KUIAMURU VODACOM NA MITANDAO MINGINE KULIPA KODI KWA FAIDA YA NCHI YETU.

    ReplyDelete

Top Post Ad