Utajiri wa Vigogo TRA Unatisha..Wajilimbikizia Magari na Majumba ya Kifahari

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Aliyekuwa Kamishina Mkuu, Rished Bade
IMEVUJA! Hakuna shaka kwamba, utajiri wa wale vigogo watumishi wa umma waliokuwa wakifanya kazi Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) unatisha kufuatia gazeti hili kufukunyua mali za baadhi yao, twende hatua kwa hatua.
Ijumaa iliyopita, Waziri Mkuu wa Tanzania, Majaliwa Kassim Majaliwa, alifanya ziara ya kushtukiza kwenye ofisi za Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) na kubaini ukwepaji kodi mkubwa ulioikosesha serikali kiasi cha shilingi bilioni 80.
Katika kikao na viongozi wa TPA sanjari na viongozi wa TRA, akiwemo aliyekuwa Kamishina Mkuu, Rished Bade, Waziri Majaliwa aliamuru papo hapo, kusimamishwa kazi kwa baadhi ya vigogo wa bandari.

PANGA LILITUA KWA HAWA
Vigogo waliosimamishwa ni pamoja na Bade, Kamishina wa Forodha na Ushuru wa Bidhaa, Tiagi Masamaki na Habibu Mponezya wa Kituo cha Huduma kwa Wateja kisha waziri mkuu akamwagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP Ernest Mangu kuhakikisha wote wanakamatwa.
Wengine waliosimamishwa ni Eliachi Mrema (Msimamizi Mkuu wa Bandari Kavu Dar es Salaam), Haruni Mpande (Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano) na Hamis Omar, Nsajigwa Mwandegele, Robert Nyoni na Anengisye Mtafya.

AGIZO ZITO
Kabla hajamaliza kikao, Waziri Majaliwa aliagiza kuwa, licha ya watu hao kukamatwa, hati zao za kusafiria kushikiliwa, pia mali zao zichunguzwe ili kubaini kama zinaweza kumilikiwa na mtumishi wa umma kwa kutumia mshahara wake!

RISASI MCHANGANYIKO LAFUKUA
Kufuatia agizo hilo la Waziri Mkuu katika kipindi hiki cha ‘hapa kazi tu’, gazeti hili liliingia mtaani kwa kufanya uchuguzi wa kina ili kubaini utajiri wa vigogo hao na wengine ambao hawajakumbwa na sakata hilo.

Juzi Jumatatu, Risasi Mchanganyiko lilifika Masaki, Mbezi na Tegeta Madale kwenye makazi ya baadhi ya watumishi hao ili kuona mazingira yao.
Ndani ya nyumba ya mtumishi mmoja, Risasi liliona magari matatu ya kifahari aina ya Toyota Land Cruiser ‘VX’, Mercedes Benz na Range Rover achilia mbali Toyota Noah ambayo majirani walisema huwa inakwenda sokoni kufanyia ‘shopping’.

Kwenye nyumba nyingine, ukuta ulikuwa mrefu kiasi cha wapigapicha wetu kushindwa kuona ndani mpaka wakapiga kengere. Lakini majirani walisema si rahisi kufunguliwa kwa siku mbili hizi kwani kumekuwa na ‘ingia toka’ ya watu wa usalama wa taifa.

Kama hamna namba za simu za mtu yeyote aliye ndani sijui kama mtafunguliwa. Siku mbili hizi, watu wa usalama wa taifa wanaingia na kutoka,” alisema jirani mmoja.
Jirani huyo alisema jumba hilo mmiliki ni mkaaji mwenyewe ambaye ni mtumishi wa TRA na ana nyumba nyingine maeneo ya Mwenge licha ya kumiliki maduka ya nguo Kariakoo, Dar.
Baada ya hapo, gazeti hili lilifunga safari hadi Pugu ambako kuna makazi mengine ya mmoja wa vigogo hao lakini nyumba ilionekana kuwa kimya na kutokuwepo kwa gari hata moja kwenye eneo la maegesho.

Akizungumza na Risasi Mchanganyiko, Mjumbe wa Nyumba Kumi Mtaa wa Pugu Bombani, Abdallah Shaban alisema huwa kunakuwa na magari mengi kwenye nyumba hiyo, lakini kwa siku mbili zilizopita (Jumamosi na Jumapili) hajayaona.
“Hapa ‘panakuwaga’ na magari mengi sana. Unaweza kusema ni yadi ya kuuza magari, lakini siku mbili hizi sijayaona,” alisema mjumbe huyo.

MAGARI HAYANA KAZI
Mjumbe huyo alikwenda mbele zaidi kwa kusema kuwa, kutokana na magari kuwa mengi pasipo watumiaji, mara nyingi asubuhi mmiliki huyo humwagiza mtu mmoja kuyawasha na kuunguruma kwa muda kisha kuyazima kwa lengo la kuyapasha moto.

NYUMBA KAMA KIJIJI
Mjumbe huyo alilionesha Risasi Mchanganyiko eneo kubwa la mtumishi huyo ambapo amejenga nyumba za familia zisizopungua 20 sehemu moja (kama kijiji) na moja tu ndiyo imepangishwa.

UCHUNGUZI WA JUMLA
Uchunguzi wa jumla uliofanywa na Risasi Mchanganyiko ulibaini kuwa, watumishi wengi wa TRA na TPA wanamiliki nyumba na magari licha ya kulipwa mshahara wa ngazi ya serikali ambao wasingeweza hata kununulia gari moja la kifahari kama ilivyo sasa.
GPL
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

10 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. hata rais aliemaliza mda wake anafaa ashtakiwe

    ReplyDelete
  2. WOTE WATAIFISHWE MAGARI NA MAJUMBA NI MALI YA SERIKALI WIZI HAWA WAKUBWA

    ReplyDelete
  3. USILE NA KIPOFU UKAMSHIKA MKONO

    ReplyDelete
  4. Hizo nyumba zitaifishwe ili waishi askari wetu(polisi),maana askari wa tanzania wanakuwa kama hawana msimamizi maalum,wengi wako ovyoovyo ukizingatia ni watu wanabeba maisha yetu uraiani,wana kazi ngumu sana.

    ReplyDelete
  5. Hawa watu hawana Mungu/Dini na moto ushaanza kuwachoma duniani.Unajisikiaje wewe unakuwa na utajiri na kujilimbikizia mali tena haramu wakati unaona binadamu mwenzio anakosa hata mlo mzuri kwa siku?Unajikiaje unaposikia mtanzania mwenzio anakosa dawa na hata kitanda cha kulalia hospitali?Na bado,zamu yenu ya kusota inakuja muda si mrefu mtapata fimbo kali muipate joto la jiwe maana watanzania tumeamua.Mungu ibariki TZ.

    ReplyDelete
  6. Walimu tu. Lkn police ouzo. Madaktar ouzo.

    ReplyDelete
  7. Mnyika alisema kwa sababu ya udhaifu wa kikwete
    Hata spika Sita alisema kikwete kuwa mkali

    ReplyDelete
    Replies
    1. Je Yeye Kikwete dhaifu tu au naye kawekeza.

      Delete
  8. Hizo nyumba zipigwe mnada na pesa irudi serikalini. Pengine tutawapata mafisadi wengine wakati wa mnada. Haya majitu ni kama kinyonga au paka jinsi yalivyokuwa na siri ndani ya siri.

    ReplyDelete
  9. Watu kama hawa hata Uraia wako uchunguzwe inawezekana si raia halali wa nchi hii haiwezekani Mtanzania mzalendo kujimilikisha mali zote hizi kama mfanyabiashara wakati ni mtumishi wa umma tu jamani hii haivumiliki tumsaidie magufuli kwa hali na mali kuwarepoti waovu wote ktk nchi yetu hata hawa wauza unga nao watajeni mitaani kwenu huko.

    ReplyDelete

Top Post Ad