Chadema Wadai wako Tayari Kuchangisha Fedha Kuilipa TBC irushe Bunge Lote 'Live'

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesema kuwa kiko tayari kuzunguka nchi nzima kuchangisha fedha kwa ajili ya kulilipa Shirika la Habari Nchini (TBC) gharama za kurusha moja kwa moja matangazo ya vikao vyote vya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Naibu Katibu Mkuu wa Chadema – Zanzibar, ambaye pia ni Kaimu Katibu Mkuu wa chama hicho, Salum Mwalimu ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam alipozungumza na waandishi wa habari akipinga sababu zilizotolewa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye kuhusu uamuzi wa TBC kutorusha ‘Live’ vikao vyote vyote Bunge bali kurusha ‘Live’ baadhi ya sehemu ya vikao hivyo.

Nape alieleza kuwa serikali imechukua uamuzi huo kwa lengo la kubana matumizi kwa kuwa TBC imekuwa ikitumia shilingi bilioni 4.2 kwa ajili ya kurusha moja kwa moja matangazo ya vikao vya Bunge.

“Watafute namna gani ya kuweza ku-mobilize fedha ili ilipwe TBC au Taifa litafute Channel nyingine za kuweza kurusha matangazo hayo. Na Chadema tuko tayari kusaidia hilo. Tuko tayari kuhamasisha Watanzania mwenye shilingi moja, shilingi mbili au tatu atoe tuilipe TBC ili Bunge lirushwe moja kwa moja,” alisema Mwalimu.

Katika hatua nyingine, Mwalimu alionesha kutokubaliana na hesabu za shilingi bilioni 4.2 zilizotajwa na Waziri Nape kuwa gharama za kurusha matangazo ya Bunge ‘Live’ kwa TBC.
“Mimi nimekuwa mwandishi wa habari na nimefanya kazi kwenye TV. Kila nikichambua  shilingi 4.2 bilion kwa ajili ya kurusha Bunge katika muda ambao sio ‘prime’… yaani kila nikipitia rate zote za Televisheni, sioni hiyo 4.2 bilioni zinapatikanaje,” aliongeza.

Wabunge wa upinzani leo pia walitoka nje ya Bunge hilo kushinikiza serikali kubadili tangazo lake kuhusu TBC na vikao vya bunge.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

24 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hachangishwi mtu tulieni Mbowe hatuna shida ya kuona nyuso zenu kwenye luninga jadilini bungeni yaliyo ya maana kwa faida ya mtanzania sio kupotezea wakati nini maana ya bunge ni Law makers yapo ya muhimu muyafanye kuliko kuuza nyago zenu kwenye tv sio blabalaa na wakati wa kampeni umeshipita HAPA KAZI TUU

    ReplyDelete
    Replies
    1. hili nalo limsukure la ccm. boya.

      Delete
    2. Huyu naye takotako hana hoja mkundu wake.

      Delete
  2. Hii mpya wako tayari kuzunguka nchi nzima kuchangisha gharama za kulilipia shirika la habari nchi yaani matatizo kibao ya watanzania hio michango yenu siingeenda palipo na muhimu kuliko hayo matangazo kwa nini mnahadaa watanzania leo kama vile hatujui changamoto za maisha ya mtanzania

    ReplyDelete
    Replies
    1. ficiem huyu, lakini masikini wa fikira

      Delete
    2. tena hayo yote hapo juu ni MAFICIEM MAKUBWA

      Delete
  3. Hawa jamaa cjui ni wa style gani...wananchi wanashida za maisha yao... wao kwakuwa wanakaa viyoyozini...et tuchangishe ujinga...embu changishen mtununulie shuka Mahospitalini tumechoka kulalia shuka zenye madoa doa (damu)

    ReplyDelete
  4. Kwa kweli hata mimi nashindwa kuwaelewa hawa jamaa, unatoka nje kwa sababu ya kutoonekana kwenye luninga? ni matatizo mangapi tunayo kwenye majimbo yetu ambayo yalitakiwa kupewa kupau mbele? chukulia watu tuna shida ya maji, hospital kwenye vijiji vyetu, dawa mahospitalini, shule, madawati n.k eti leo wanaona issue ya kutorusha matangazo ya live iwe kigezo cha kupoteza muda wa kujadili isues ambazo zina mashiko????? tumewachoka na ikitubidi tutawafuata huko huko bungeni ili tuwachalaze viboko maana mnaiba muda wetu wa maendeleo - pumbavu kabisa hamna maana hata kidogo

    ReplyDelete
  5. usitegemee maisha yako usaidiwe na mtu mwingine, au serikali, maisha yako unajisaidia mwenyewe, tunachotaka wananchi ni kujua nini kinaendelea bungeni, Mh Mbowe uko sawa tutachangia mpaka kieleweke, wasitake kutuhadaa na hoja za kitoto, watanzania cyo wadanganyika tena!

    ReplyDelete
    Replies
    1. yani we kweli mjinga wa mwisho apa duniani marekani, uingereza zimepiga hatua kubwa kimaendeleo bila kuonyesha matangazo ya bunge live afu unasema watanzania sio wakubuluzwa sasa kwa taarifa yako unaburuzwa wewe na hiyo ukawa yako
      dawa mahospitalini hakuna, walimu hakuna wakutosha mashuleni, ajira ni shida yani mambo kibao ni shida apa tanzania then unasaport eti kuchangishwa kwa pesa kurusha matangazo ya bunge kwa faida gani we ukitazama bunge unaongezeka uzito?
      mpumbavu mkubwa wewe kazi kushabikia anasa na utachomwa moto kwa laana yako
      huyo mbowe mwizi tuu na dikteta uko ukawa

      Delete
    2. wewe ndo PUMBAF mkubwa, akili zako ziko matakoni, aliyekuambia maendeleo yanakuja kwa kuonyesha bunge live ninani? bwege wewe hata kutafakari habari zilizo andikwa na watu wengine hujui, ndiyo nyie maficiem mnapewa zamana ya uongozi mnaharibu, tunachotaka ni kujua nini wabunge wanafanya bungeni LIVE na cyo kuhadithiwa, wewe unazungumzia MAENDELEO, PUMBA mkubwa wewe!

      Delete
    3. kama unataka ona bunge live nenda dodoma msenge wewe
      hata kutengeneza hoja hujui
      kwahiyo ukiona bunge live ndio utapata maendeleo?
      me nawasi wasi hata mbunge wako humjui wewe chizi kazi kushabikia tv
      kwanza umeshajijibu mwenyewe maendeleo hayaji kwa kuangalia bunge live!
      hapa kazi tuu

      Delete
  6. Nadhani sio wazo baya kuchangisha ili wananchi waweze kuona live yanayotokea bungeni, kwani kuna miswada mingi inayopitishwa na kusimamiwa na serikali bila kujali maslahi ya wananchi. Sasa wananchi watakapoona live uendeshaji na uchangiaji wa hoja bungeni itakua rahisi kwao kumjua ni nani adui wa maendeleo yao, kuliko kusubiri kuhadithiwa baadhi ya mambo baada ya vikao vya bunge kumalizika.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Itakusaidia nini yakusikia wakati huwezi changia lolote watanzania walio wengi wanashida na maendeleo wacha wabunge waitedendee haki ya ubunge wao kuleta masilahi ya nchi sio kuleta longolongo kutizama purukushani za bunge katika tv haisaidii kukuletea maendeleo

      Delete
  7. Kweli kabisa, lazima tuone ni nini kinaendelea. Hii mipumba minne ya mwanzo kutoa comments ni misukule ya fisiem, ovyoooo...go screw yourself!

    ReplyDelete
  8. Kwan ukiona live unapiga simu saa hiyo hiyo? ukiona kipindi baada ya kurekodiwa kuna mapungufu gani? jamani tuache ushabiki tuangalie hoja za msingi....

    ReplyDelete
  9. pawepo Tv licence kila mwenye tele anapashwa alipe sh 50000 kwa mwaka hii itasaidia kuendesha shughuli za live bungeni. lakini sio kuchangisha watu ela kama mboe wanavyosema.Bunge liweke sheria ya kodi ya television.Hii itasaidia radio tanzania kuimili mabadiliko.ENGLAND IKOVILE

    ReplyDelete
  10. tbc irushe bure matangazo kwa kuwa bunge ni la umma na tbc ni mali ya umma gharama za nini?

    ReplyDelete
  11. Na sisi huk tunalipia tv, radio. Watanzania wanahitaj mtu kama Kagame awakogote masikio na midomo ili wasiw wanashabikia upumbav, et wafuate bunge live?? inamaana gani? itakusaidia nini? mko wapunguf wa akili ila sikos lenu muna shabikia tu bila kujielewa.unalala njaa, mtoo anakwend shul bila hata kunyw chai, maji safi hamuna, hospitali mbovu dawa vitand shuka na kathalika hamna kish unashabikia upumbav leta fikra ya kuchangish ili mulet maendeleo kwa wanainch na kushughulikia matatiz yao. Hapo itakua safi.

    ReplyDelete
  12. Eti kuzunguka kuchangisha pesa za TBC. Si mtumie mlizohongwa na Edo au mmeshazibugia zote!CDM mnajitafutia umaarufu wa bei nafuu.

    Kug'anga'ania kwenu hoja ya TBC kunanifanya niamini kuwa kweli mmeishiwa hoja zamu hii.

    Hapa Kazi Tu, itawatoa kijasho!

    ReplyDelete
  13. Ngoma imelala hapo na siasa za akina karume kenge bongo yaani bado sana siasa ya bongo ni sawa na mtoto mdogo anaejifunza kutambaa

    ReplyDelete
  14. mi chadema mindezi kweli ni mihuni mpaka basi inatumia mwavuli wa wananchi kuwahada wananchi
    pumbavu kabisa eti nyie mpewe nchi mavi yenu
    hata sera hamna kazi kuzungusha mikono na ukabila wenu

    ReplyDelete

Top Post Ad