Magufuli Utaua Mawaziri Waliopita Kwa Njaa, Hawana Cha Kufanya

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mh. Magufuli kwanza nikupongeze kwa kazi nzuri uliyoifanya mpaka sasa, japo sijutii kura yangu niliyompa mamvi na wala sitakaa nijutie, tulikuwa tunataka mabadiliko na sasa ninayo furaha ya dhati kabisa kuyaona haya mabadiliko kupitia kwako

Pili Mh. Nilichofurahi zaidi ni kupunguza gharama kubwa za kuhudumia wizara na mawaziri wake 60 wa awamu iliyopita hakika wewe ni mzalendo, na samia pia najua aliupata uzalendo zaidi katika kipindi za kampeni kijiji kwa kijiji nilimshuhudia akimwaga chozi kwa shida za wananchi alizokumbana nazo huko vijijini hakuamini na alituahidi na wasanii wakiwepo(mashahidi) mtaipitia mikataba yote ya madini

Mh. Magu chukua hii kama New year special, ulivyowatimua wastaafu mawaziri kwenye nyumba za serikali wengine hawana pa kukaaa, hakya Mungu tena ninaapa, hawakuona umuhimu wa kujenga kwa maana walijua nyumba za serikali ni zao

so sad , kuna mmoja anakaa kwa shemeji yake, (kaka wa mke wake) amechoka vibaya, sasa mbaya zaidi kaja na kuku wake kila siku wanatifua bustani za majirani maana humo ndani hamna banda wanafugia nje inaleta usumbufu mno, na hataki kuondoka mpaka ahakikishe kwamba hata ukuu wa wilaya amekosa ndio atarudi mwanzaaaa

Ninachokuomba Mh. harakisha hizo teuzi usifanye kwa nukta nukta utaua watu na njaa, hawana pa kuishi, hawana kazi, ubunge wamekosa, january hii watoto adaa mheshimiwa ujue hawasomi shule za kata, soon watakosa chakula na mimi ninasema ikifika february kuku wake wakiendea kutifua bustani yangu nakula mmoja baada ya mmoja
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hatuhusu sisi
    Kwani walichoiba hakitoshi
    Waende Msoga awasaidie
    Hapa kazi

    ReplyDelete
  2. mtoa mada vipi! mada haina kichwa wala miguu kwa hiyo tatizo ni nini au kuku ndo unawatamani? we una nini? acha kufurahia shida za watu!.

    ReplyDelete
  3. Kama hata ubunge alikosa alitaka serikali imfanyie nini, mwandishi mpambe tu hana hoja

    ReplyDelete

Top Post Ad