Mh. Diwani Laivu Akimbambia Mwanamuzki Linah....Ni Kwenye Party ya Shilole Kujipongeza Kuachana na Nuhu Mziwanda

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Diwani Baba Levo Akibambia Mtoto
HII ni aibu ya kufungulia mwaka 2016! Mheshimiwa Diwani wa Kata ya Mwanga Kigoma-Kaskazini, Clayton Revocatus ‘Baba Levo’, amenaswa laivu akimbambia staa wa Bongo Fleva, Esterlina Sanga ‘Linah’ usiku mnene, Ijumaa limeshuhudia tukio hilo mwanzo mwisho.

SIKU YA TUKIO
Tukio hilo la aina yake lilitokea usiku wa kuamkia Desemba 29, Mwaka huu Kijitonyama jijini Dar, ambapo wawili hao walikuwa wamehudhuria kwenye bonge la pati lililokuwa limeandaliwa na msanii mwenzao Zuwena Mohamed ‘Shilole’.


NI PATI YA KUACHANA
Shilole aliandaa sherehe hiyo maalum kwa lengo la kufurahi pamoja wakati akijipongeza baada ya kuachana na aliyekuwa mpenzi wake Naftari Mlawa ‘Nuh Mziwanda’.

BABA LEVO NDIYE MC
Wakiwa kwenye sherehe hiyo, Baba Levo alikabidhiwa jukumu la kuwa mshehereshaji (MC) wa pati hiyo, ambapo alianza kwa kuwakaribisha wageni wote waalikwa kisha kuianza sherehe rasmi.

MTUNGI MDOGOMDOGO
Kama ilivyo ada ya watoto wa mjini wanavyosema sherehe hainogi bila ‘maji ya Ilala’, Baba Levo aliungana na wageni waalikwa kuanza kupiga ‘maji matamu’ taratibu huku wakionekana kuchangamka kadiri muda ulivyozidi kuyoyoma.

LINAH AANZA KUCHANGAMKA
Linah ndiye aliyekuwa wa kwanza kuonesha kwamba ‘mambo’ yamepanda kichwani baada ya kuinuka mahali alipokuwa amekaa na kuanza kucheza muziki huku akirusha miguu kama ile staili ya Mapanga Shaa ya Wanaume Halisi.
IMG_8730
Mastaa kibao walikuwepo kwenye pati hiyo.

UVUMILIVU WAMSHINDA MH. DIWANI
Mheshimiwa diwani huyo mwenye mbwembwe na maneno mengimengi ya kufurahisha, naye uvumilivu ulimshinda ambapo alijikuta akiinuka na kuanza kucheza peke yake huku akionekana kumkodolea macho zaidi Linah ambaye wakati huo alikuwa amezidisha mbwembwe.

KABAAAH! AMBAMBIA
Huku na huku haikupita muda mrefu sana, Baba Levo alijikuta tayari yupo kwenye mgongo wa Linah na kuanza kucheza naye huku mrembo huyo akimpa ushirikiano kama anayesema: “Ulikuwa wapi muda wote nateseka kwa kucheza peke yangu.”

WAALIKWA FULL KUSHANGALIA
Kutokana na waalikwa wengi kuwa tayari ‘wameshapendeza’, kadiri Baba Levo na Linah walivyokuwa wakicheza kwa staili ya kukata mauno huku mheshimiwa huyo akiwa amemkumbatia vilivyo Linah, waalikwa walishangilia kwelikweli.
IMG_8732Mwandishi wetu aliyeshuhudia tukio hilo kinaga ubaga aliendelea kuwafuatilia wawili hao kwa kupiga picha ambazo zilidhihirisha wazi kuwa hawakuwa wao bali yale ‘maji’ waliyokunywa.

MASTAA WALIOHUDHURIA
Kwenye sherehe hiyo ambayo waalikwa walikula na kunywa, mastaa wengi walihudhuria akiwemo Mtangazaji Millard Ayo, Said Chigunda ‘Chegge’ (Bongo Fleva), Baby Madaha (Bongo Fleva), Isabela Mpanda (Bongo Fleva), Skyner Ally ‘Skaina’ (Bongo Movies) na wengineo.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

7 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kwani ukiwa diwani ndo hudindi?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Maneno gani hayo pale wanacheza kudinda issue nyingine

      Delete
  2. kuna habari nazisikia sikia kwenye mitandao ya kijamii eti linah ni punda mbeba madawa ya kulevya
    wadau nijuzeni kwa aliyewahi sikia story izi au ndo udaku

    ReplyDelete
  3. Nashangaa. Kuna social life pia. Kama mkwere tu anapolisakata rhumba.

    ReplyDelete
  4. Jamani mavazi hayaa....tutabarikiwa vipii nchi hiiii tunaomba kila siku mungu ibariki tanzania...haya mavazi tutakosa hata baraka za munguuuu ...jamani tujiheshimuu mwanamke staraa....jamani wanawake sisi mungu atupe hidayaa

    ReplyDelete
  5. Wanacheza wanaanzaga hivyo hivyo mwisho unakua mchezo wa kweli mbeke za wt haswa ukinywa maji ya zahabu

    ReplyDelete
  6. basi baba Levo alikula mzigo wa lina

    ReplyDelete

Top Post Ad