Nikipata mwanamke atakayeweza kuziba nafasi ya Shilole ndio nitafuta tattoo zake – Nuh Mziwanda

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Ingawa Shilole tayari amefunika tattoo aliyochora kifuani yenye jina la ex wake Nuh, kwa kuongeza mchoro wa ua juu yake baada ya wawili hao kuachana, Nuh Mziwanda amesema yeye bado hajaamua kufuta tattoo zake.

Nuh ambaye alichora tattoo mbili, moja ikiwa na jina la Shishi Baby na nyingine ikiwa na sura ya Shishi amesema kuwa endapo atapata mwanamke wa kuziba pengo la Shishi ndio atafuta tattoo hizo.

“Mimi sijatoa hii tattoo sababu sijapata bado mwanamke ambaye anayeweza ku-cover nafasi ya yule mwanamke, nikipata mwanamke ambaye ataweza kucover nafasi ya yule mwanamke, akinishawishi kweli kuona anatabia ambazo mimi nazitaka basi…” alisema Nuh kupitia AYO TV.

Nuh aliendelea kueleza sababu za yeye kuchora tattoo za Shishi kwenye mwili wake.

“of-course yule mwanamke mimi nilimpenda kweli na mimi ndio nilianza kuchora tattoo kwake yeye so I was real, nilichora tattoo kwa mapenzi sikuchora kwasababu ya. Unajua ukichora tattoo kwasababu ya inamaanisha moyoni unakuwa unaumia unatamani ile tattoo uitoe ndio maana hata yeye (Shishi) aliweza kuibadilisha ikawa ua. “.


Chanzo cha ugomvi kati ya Shilole na Nuh Mziwanda kilichopelekea penzi lao kuvunjika kimeendelea kubaki kuwa siri yao, kutokana na wote kutotaka kukisema licha ya Shishi kuweka wazi kuwa Nuh ndiye mkosaji.

“Sipaswi kusema kitu gani kimetokea au kipi ambacho kimefanya mimi na bibie tuweze kutengana kwasababu ni maisha. Katika maisha kuna kupata na kukosa kwahiyo unaweza ukampata mtu na ukamkosa mtu, so kuachana ni kitendo cha kawaida tu ambacho kipo katika maisha yetu ya kila siku.” Alieleza NUh.

“Kama yeye anasema mimi ndio nimemkosea its okay all in all najua Mungu yupo na anatuangalia sisi binadamu tunafanya nini, mimi mama yangu kanifundisha kaniambia mtoto wa kiume hutakiwi kuongea, mtoto wa kiume unasifiwa kazi, kwahiyo kama yeye anasema mimi ndo nimemkosea its okay ila moyo wake unajua kitu gani kinaendelea.” Alisema Nuh Mziwanda ambaye amekuwa kwenye uhusiano na Shishi kwa miaka mitatu.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Binadamu tuliongea hapa hapa ya kuwa siku zote mapenzi ya bendera hayadumu,ndio hii imetokea.
    Nakupa pole Nuh ila nakuuliza hivi, umezoea kulelewa je utaweza tena ku-date wa rika lako au mdogo kwako?

    ReplyDelete
  2. nuh umeongea busara sana!!

    ReplyDelete
  3. huyu mtoto kashazoea u mariooo asipoangalia atapakatwa sasa na wajanja wa mjini

    ReplyDelete
  4. Huo ni ukomavu Nuh...

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ridiculous, labda ukomavu wa kulelewa na wanawake.

      Delete

Top Post Ad