Nyumba ya Mchungaji Lakatware Yasababisha January Makamba Kuchukua Hatua Kali Kwa Maafisa Hawa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

SAKATA la maofisa watatu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), waliosimamishwa kazi kwa tuhuma ya kukiuka miiko yao ya kazi, limechukua sura mpya, baada ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba, kuagiza wafikishwe mbele ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).

Pamoja na hayo, Waziri huyo amemsimamisha kazi aliyekuwa mwanasheria wa baraza hilo, John Mnyele kwa matumizi mabaya ya ofisi.

Akizungumza  jana, alisema tayari amemwagiza Katibu Mkuu wa wizara hiyo, kuwasilisha mashtaka yanayowakabili maofisa hao watatu Takukuru kwa ajili ya uchunguzi na hatua zaidi, ikiwemo kufikishwa mahakamani.

Maofisa waliosimamishwa kazi kutokana na udhaifu huo ni pamoja na Ofisa Mazingira Mwandamizi Dk Eladius Makene, Mwanasheria Daraja la II Wakili Heche Suguta Manchare ; na Ofisa Mazingira Boniface Benedict Kyaruzi. Wanatuhumiwa kukiuka miiko ya kazi yao katika kusimamia kiwanda cha kusindika minofu ya punda kilichopo mkoani Dodoma.

Pamoja na maofisa hao, pia Mwanasheria Mnyele, anayetuhumiwa kuingia mkataba na Mchungaji Getrude Rwakatare wa kuondoa kesi mahakamani kwa niaba ya NEMC bila kuijulisha ofisi, naye anachunguzwa na taasisi hiyo ya rushwa.

Mama Rwakatare kwa sasa ana kesi mahakamani dhidi ya baraza hilo ya kupinga kubomolewa kwa nyumba yake, inayodaiwa kujengwa mahali pasiporuhusiwa.

Kiwanda hicho cha minofu ya Punda cha China, kilianza kazi hiyo rasmi mwaka 2012 huko Dodoma ambapo pamoja na kuchinja, pia huuza nyama hiyo nje ya nchi, hususan China.

Kiwanda hicho kilipatiwa vibali vyote, ikiwemo cha Mamlaka ya Ukanda Maalumu wa Uwekezaji nchini (EPZA) na cha Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi cha kuchinjia.

Pia, kilikuwa na vibali vingine vya Manispaa. Hata hivyo, hakikuwa na kibali cha masuala ya mazingira kutoka NEMC.

Katika ukaguzi uliofanywa siku za nyuma na Baraza hilo, ilibainika kuwa kiwanda hicho hakina kibali hicho cha mazingira, lakini pia kilikuwa kikilalamikiwa na wananchi wanaokizunguka kutokana na kutofuata taratibu za utunzaji wa mazingira.

NEMC ilibaini kuwa kiwanda hicho, hakikuwa na mfumo wa majitaka, lakini pia kilikuwa kikichoma mabaki yanayotumika kuchinjia ndani ya kiwanda hicho na moshi wake kusambaa maeneo yanayokizunguka.

Kutokana na makosa hayo, baraza hilo lilikifungia kiwanda hicho kama adhabu na kukilipisha faini ya Sh milioni 240.

Juzi Waziri January pamoja na kuwasimamisha maofisa hao watatu kwa kukiuka miiko yao ya kazi, pia aliagiza Mkurugenzi Mkuu wa baraza hilo, Mhandisi Bonaventura Baya, apewe barua ya onyo kali na la mwisho kwa tuhuma za udhaifu katika usimamizi wa watumishi wa baraza hilo, hivyo kusababisha malalamiko mengi kuhusu utendaji wa baraza hilo.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Makubwa haya
    Lakini ni mfumo uliokuwepo madarakani wakati huo
    Uvamizi mbona CCM umevamia maeneo mengi Tanzania
    Umeiba viwanja vya watanzania na kuviita vya CCM
    CCM si ya watanzania wote
    Rudisheni

    ReplyDelete
  2. TAYARI IKO KIMAKOSA KWA HIYO VUNJA HARAKA WAKATI KESI INAENDELEA.MBONA WENGINE HAWAKUSUBIRI PAMOJA NA KUWA WALIPINGA NYUMBA ZAO KUVUNJWA?
    SI MTAMLIPA KAMA AKIWASHINDA?ACHENI KUTUZUNGUSHA

    ReplyDelete

Top Post Ad