Uchambuzi: Rais Magufuli Hakuwa Sahihi Kuvaa Nguo za Kijeshi, Vinginevyo.....

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Kwanza nianze na cheo cha Amir jeshi mkuu.

Kiuhalisia cheo hiki hakina hakina mahusiano yoyote na vyeo vinavyopatikana katika ngazi za kijeshi! Hiki hata mtu ambaye hajui nini maana ya jeshi akishakuwa rais wa nchi tu hupewa! Hakina mahusiano yoyote na vile vyeo vinavyopatikana ndani ya jeshi ambavyo mwisho wake ni Jenerali!

Mfano ingetokea kama rais Kikwete (enzi akiwa rais) leo angevaa vazi la jeshi basi angevaa katika ngazi ya ukanali ila kwa rais (e. g
angekuwa Kikwete) cheo chake cha Amir jeshi mkuu kingebaki palepale na angetambulika kwa cheo chake cha Amir jeshi mkuu!

Ni amri ya jeshi kuwa mtu anapokuwa katika vazi la jeshi basi awe kirasmi! Kuendana na cheo chake. Ila hii haiondoi maana kuwa mtu akivua lile vazi basi cheo chake hakitambuliki! La hasha! Ila msisitizo ni pale unapokuwa ndani ya lile vazi basi uwe rasmi ndani ya mfumo wa jeshi la wananchi!

Mathalan Mwamunyange akiwa kiraia bado ni mkuu wa majeshi na anapewa sifa zote za ukuu wa majeshi! Ila akiwa ndani ya vazi la jeshi ni lazima awe ndani ya vazi rasmi linalotambua cheo chake ndani ya mfumo wa jeshi (Jenerali)

Kwanini rais Magufuli hakuwa sahihi?
Mbali na kuwa bado ni Amir jeshi mkuu, rais Magufuli hana cheo chochote ndani ya mfumo wa jeshi! Hajawahi kuwa ndani ya jeshi la wananchi kama mwana jeshi! Lile vazi ni la mwanajeshi wa kawaida ndani ya jeshi la wananchi! Kwa maana nyingine rais Magufuli pale alikuwa ndani ya mfumo wa jeshi! Labda tuambiwe kuwa alipoenda Monduli naye alitunukiwa cheti cha kufuzu mafunzo ya kijeshi ndani ya JWTZ!

Vinginevyo rais atakuwa amevaa lile vazi kama wanavyofanya kina Diamond ambapo ni kinyume na taratibu za jeshi na ndo maana wanapigwa marufuku!

Nadhani mmekuwa mkimwona Kikwete enzi akiwa rais alikuwa akitoa saluti kwa viongozi wenzake! Pale alikuwa akitumia mfumo rasmi wa jeshi kwa wakubwa zake kijeshi (Ingawa cheo chake cha Amir jeshi mkuu kilikuwa palepale) hivyo alikuwa hakosei kufanya hivyo!

Narudia tena: cheo cha Amir jeshi mkuu hakipo ndani ya mfumo rasmi wa jeshi. Hata mtoto mdogo akiwa rais wa nchi basi cheo hicho kinafuatia palepale!

Pia inashauriwa kuwa si vyema sana rais wa nchi ambaye amechaguliwa kwa kura kuwa ndani ya mavazi rasmi ya kijeshi kutokana na cheo chake! Hii inazua mkanganyiko wa heshima za kijeshi zinazotolewa! Mathalan Kikwete leo angeamua kuvaa vazi rasmi la kijeshi huku akiwa rais basi angeishia cheo cha kanali! Hapo yupo ndani ya vazi rasmi la jeshi kisha anapokea saluti kutoka kwa jenerali! Hii siyo sawa! Rais wa nchi anabaki kuwa Amir jeshi mkuu hii haijalishi kuwa amepita na/au hajapita jeshini! Kinacholeta mkanganyiko ni lile vazi rasmi la jeshi!

Huwa wanasema "ukiwa nje ya lile vazi utaheshimiwa kwa cheo chako kijeshi, ukiwa ndani ya vazi utaheshimiwa kutokana na vazi" na ndo maana mtu akiwa ndani ya lile vazi basi anawekewa vyeo vyake kijeshi lakini akiwa nje ya vazi hawekewi vyeo vyake ila bado anatambulika maisha yake yote!

Kwa hiyo kuna mawili! Eidha rais Magufuli ameanza rasmi mafunzo ya kijeshi na ana cheo cha chini kabisa kijeshi na/au alivaa lile vazi kama watu wengine! Ikiwa hilo la pili ni kweli basi hakuwa sahihi kutokana na kuvaa vazi rasmi la JWTZ bila kuwa ndani ya mfumo wa jeshi!
Ikiwa hilo la kwanza ni sahihi basi yuko sawa na cheo chake cha Amir jeshi mkuu bado kipo palepale ila kwa hapo yupo ndani ya mfumo rasmi wa jeshi!

By G Sam/Jamii Forums
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

14 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Haya Yale Yale ya samaki WA Magufuli yanatugharimu hadi
    Ikulu imejaaa vibaka , matapeli , mafisadi
    Hivi hawawezi kumshauri rais
    Tulitegemea kukaa kimya angekuja na ya maana
    Aibu aibu

    ReplyDelete
  2. Kitu usichokijua ni sawa na usiku wa giza uliza kwanza kabla hujaandika umbumbumbu wako hapa.

    ReplyDelete
  3. Kitu usichokijua ni sawa na usiku wa giza uliza kwanza kabla hujaandika umbumbumbu wako hapa.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Koma wewe hata amri jeshi mkuu wa dunia USA , hajavaa nguo za kijeshi
      Shame CCM mvalisheni Na madira akienda kwenye taraabu
      Jificha yote hii kumbe hamnazo

      Delete
    2. yani wew aninymous 5:26 ziro kweli kwa taarifa yako obama nguo za kijeshi anavaa sana hata uki google utaona
      acha ushabiki wa kijinga fala wew kichwa maji
      mwalimu wako inaelekea alipata tabu sana kukufundisha

      Delete
    3. utakuwa umekosea njia nenda kasome habari za wema na zari ndo utoe comment wewe anonymous 5:26

      Delete
  4. Jamani shule Ni muhimu au kuuliza sio ujinga , sasa kwa taarifa yako cheo cha juu kabisa kijeshi Ni field marshal na hutunukiwa mwnjeshi kwa sifa maalum, ulichoandika Ni uchanga Wako WA uelewa na kuchaganya mihemko ya kisiasa badala ya kufanya kazi, tembelea makao makuu ya jeshi idara ya habari hapo ujifunze kitu sio ujinga unaouandika

    ReplyDelete
  5. Mada nyingine sio za kuchangia.

    ReplyDelete
  6. mtu anamaliza form 4 na ziro anaenda kusoma chuo cha kariako au ilala course ya uandishi wa habari ndo matokeo yake haya
    hafanyi research ya kutosha ana kaa kwenye vijiwe vya kahawa anasikiliza ujinga anakuja kuuandika kwenye gazeti

    ReplyDelete
  7. UKAWA mmekosa point za kumkosoa JPM kwhy kiongozi uwa akienda kwenye mahafari akavaa joho nae uwa anakuwa graduate ? Acha kukariri

    ReplyDelete
  8. hakuna cha maana awe kavaa au hajavaa! ni same same tu.

    ReplyDelete
  9. mmmmh haya waswahili hao wanalijua jeshi ila sio wanajeshi ilimradi yote kheri tuuu

    ReplyDelete

Top Post Ad