Wizara ya Nishati Yalikana Gazeti la Mtanzania

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

WIZARA ya Nishati na Madini imeikanusha habari iliyotolewa kwenye gazeti la Mtanzania la tarehe 14 Januari 2016 kichwa chake cha habari kilichosomeka “HARUFU YA JIPU MRADI WA UMEME” aliyoandika mwandishi wa gazeti hilo Jonas.

Habari hiyo ilieleza kuwa, mradi uliozinduliwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya nne, Mh Jakaya Mrisho Kikwete uligharimu shilingi Trilioni 1.6 na kwamba fedha za ujenzi wa mradi huo zimetokana na ubia kati ya serikali ya Tanzania na Japan ambapo serikali ya Tanzania itakuwa na hisa ya asilimia 40 na kampuni ya SUMITOMO ya Japan asilimia 60,pia taarifa hizo zilidai kuwa serikali inachangia fedha za ndani kwa asilimia 12na zilizobaki ni mkopo kutoka benki ya Japan.

Mwandishi wa gazeti la Mtanzania alidai kuwa gharama za mradi huo ni kubwa ukilinganishwa na miradi mingine akitolea mfano wa kampuni ya TALLAWARA Power Station ya nchini Australia anayodai ilitaka kujenga mradi huo kwa dola za kimarekani milioni 350.

Kwa mujibu wa habari hiyo, Msemaji wa Wizara ya Nishati na Madini Bi. Badra Masoud ametolea ufafanuzi wa habari hiyo na kudai kuwa si ya kweli.

“Tunakanusha vikali taarifa hizi zilizotolewa na kwamba hazina ukweli wowote zimelenga kupotosha ukweli na kuichafua serikali.”Alisema Badra wakati akiongea na Waandishi wa Habari  jijini Dar Es Salaam

Badra alifafanua ukweli wa mradi huo na kudai kuwa serikali ya Tanzania iliingia makubaliano na Serikali ya Japan ya mkopo wa masharti nafuu wa dola za kimarekani milioni 292 kwa aajili ya kutekeleza Mradi wa kuzalisha umeme wa Megawati 240 utakaojengwa na kampuni ya SUMITOMO ya Japan kama mkandarasi EPC contractor na sio kama mbia na serikali ya Tanzania kama ilivyodaiwa.

“Mradi unamilikiwa na serikali kwa asilimia 100 kupitia TANESCO na hakuna mwekezaji mwingine katika mradi huo,hivyo si kweli kwamba serikali ya Tanzania imewekeza kwa ubia wa asilimia 40 na kampuni ya SUMITOMO kwa silimia 60.Kwa maana hiyo hatutauziwa umeme utakaozalishwa na mradi huu kwani ni mali yetu.”Aliongeza Badra

Pia alisema kuwa mradi wa Kinyerezi 2 bado haufunguliwa kama habari hiyo ilivyodai,mradi uliofunguliwa ni wa Kinyerezi 1.

Badra alimaliza kwa kuwataka Waandishi wa Habari kufuata miiko na maadili ya uandishi wa Habari kwa kuandika habari zenye ukweli na sahihi badala ya kuandika habari za mitaani kwakuwa zinapotoshajamii

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Tatizo Serikali hamuweki wazi mikataba. Serikali inamikiwa na Watu,Inabidi mikataba yote iwekwe wazi kwa kugha ambayo kila mwenye dukuduku aelewe. Na ni haki ya Watanzania kujua mikataba yote. Kwa hivyo Watu kama Waandishi wa habari Wanapopata fununu ni muhimu waandike kusudi muweke wazi mikataba yote. Hii si dhambi, na Magazeti yaruhusiwe kuibua haya ili Wananchi wajue na waridhike. Ni hivi tu ndipo Serikali itajenga uhusiano mzuri na Wananchi. na kwa njia hii tu Watu wataiamini serikali. Na Wananchi wanapoelewa pia Wanajifunza. Huenda Wanahoja pia kupitia Wabunge wao wanaweza kuzichangia. Uhuru wa Magazeti, wa kuandika na kudadisi uruhusiwe na si kukomomesha. Ukiwa mwazi hutajalali wala kuogopa. Utawajibu Watanzania vipasavyo. Isiwe vita.

    ReplyDelete

Top Post Ad