Diamond Azungumzia Collabo Mpya na Yemi Alade na Jinsi Zari Alivyobadilisha Maisha yake

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Diamond Platnumz na Yemi Alade wanatarajia kuja na collabo mpya.
Taarifa hiyo imetolewa na muimbaji huyo wa ‘Make Me Sing’ alipokuwa akiongea na na D’Mike wa kipindi cha Mseto cha Radio Citizen. Amesema yeye na Yemi tangu wakutane kwenye kipindi cha Coke Studio Africa, wameendelea kuwa washkaji wa karibu.

“Wiki mbili zilizopita amenitumia nyimbo yake mpya ambayo tutafanya, na ukiisikiliza hiyo nyimbo ina mahadhi ya kinyumbani East Africa kabisa, siwezi kusema jina inaitwaje japokuwa jina pia ni la Kiswahili,” alisema Diamond.

Katika hatua nyingine, Diamond alieleza jinsi ambavyo Zari amebadilisha maisha yake.

“Kwenye siku hii nzuri maalum ya Valentine’s kitu kikubwa nitakachoweza kumwambia [Zari] ni kwamba nampenda sana na kiukweli amecheza part kubwa sana katika maisha yangu mpaka hapa nilipo,” amesema.
“Amenizalia mtoto ambaye nilikuwa na ndoto hiyo siku zote na kila siku amekuwa akinifanya napevuka kwasababu nakuwa na akili za kimaisha natoka katika utoto nakuwa katika utu uzima ambao unanifanya niweze kutengeneza hata misingi mizuri ya kazi yangu pia. Ukisikiliza nyimbo zangu, strategy zangu za kimuziki zinazidi kupevuka. Ananitunzia moyo wangu vizuri sababu nina mapenzi naye mazito.”

Msikilize zaidi hapo chini.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

8 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kama ww diamond muislam Mtoto anaezaliwa nje ya ndoa mwanamme anakuwa c manawe hata jina la baba yake huyo tiffa aitwe tiffa abdallah na hana haki ya kukurith wale ww kumuozesha

    ReplyDelete
  2. Kama ww diamond muislam Mtoto anaezaliwa nje ya ndoa mwanamme anakuwa c manawe hata jina la baba yake huyo tiffa aitwe tiffa abdallah na hana haki ya kukurith wale ww kumuozesha

    ReplyDelete
  3. Huwa siwaelewi watu maarufu wengi, wakishapata umaarufu huwa hawajali kabisa mafundisho ya dini zao na sijui huwa wanadhani wao wapo juu ya Mungu na kwamba hawatakufa

    ReplyDelete
  4. fix hizo. anamtunzia siri ya Katunzi.

    ReplyDelete
  5. KABEMENDWA MPAKA AKILI. AJIELEWI DOMO

    ReplyDelete
    Replies
    1. wewe umejiona kama hujabemendwa??????? jiangalie kwanza wewe kabla ya kusema ya wengine mshenzi wewe

      Delete
  6. WEWE ULIYECOMENT HAPO JUU UA CHUKI SANA NA HAITAKUSAIDIA. KILA MTU ANAJUA DIAMOND WA SASA SI YULE WA ZAMANI. AMEKOMAA KIAKILI NA ANAONEKANA STRESS FREE. AMEPATA MWANAMKE MWENYE AKILI SIO WALE WAUZA SURA WA MJINI.NA HICHO NDIO KINAWAUMIZA KICHWA. MNAJUA KWAMBA MAFANIKIO YAKE MENGI ZARI ANAHUSIKA NA MNAJARIBU KUMKATISHA TAMAA.

    ReplyDelete
  7. bado anaweweseka na mimba ya Wema. anajaribu kujipoza kwa kila maneno.

    ReplyDelete

Top Post Ad