January Makamba 'Wapinzani Mnaolaumu Kazi ya Rais Magufuli Mngepewa Nafasi ni Kipi Mngefanya zaidi ya Hiki?'

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, (Mazingira na Muungano) Mh. January Makamba amefunguka na kusema kuwa wao kama Chama cha Mapinduzi ndiyo wenye dola na wao ndiyo wanaongoza serikali hivyo amewataka baadhi ya wabunge wa upinzani kuwa na lugha nzuri dhidi ya serikali ili waweze kupata ushiriakiano mzuri na viongozi hao pamoja na serikali hiyo pindi watakapo hitaji msaada wowote kutoka serikalini.

January Makamba amesema hayo bungeni na kudai amefadhaishwa na michango ya wabunge wa upinzani ambao walikuwa wakitumia lugha za kuudhi dhidi ya Rais pamoja na viongozi wa serikali.
"Najua kazi ya upinzani ni kulaumu hivi nyinyi wapinzani kwa kazi anayofanya Rais Magufuli leo mngepewa nafasi wapinzani ni kipi ambacho mngefanya zaidi ya hiki? Alihoji January Makamba

Lakini katika hatua nyingine amesema aina ya uchangiaji nyingine ya wabunge bungeni ni kama walikuwa wakiwatisha watanzania juu ya sakata la Zanzibar na alimaliza kwa kusema kuwa utatuzi wa suala la Zanzibar haupatikani barabarani, haupatikani bungeni bali unapatikana katika Katiba na sheria za Zanzibar pekee na si kitu kingine.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Tatizo tulilonalo watanzania Leo hii Kila aliepita shule kidogo anajifanya Ni mchambuzi WA siasa, wengine mnachochea chuki Tu, serikali ipo na rais Ana maamuzi kama mkuu WA nchi atafanya kazi utake usitake tuache kubeza Kila jambo.

    ReplyDelete
  2. wa bunge wa upinzani wamezidi kubibeza serikali
    tujengeni nchi jamani na tuache ujuaji

    ReplyDelete
  3. ndo mwisho wenu wa kufikiri ndo maana mnadhani kuendesha nchi ni hapo alipofika magufuli tu.......bado kuna gap kubwa na wapinzani wanaweza pewa nchi wa boresha zaidi maisha ya wananchi.......

    ReplyDelete
    Replies
    1. muda wenu ukifika wapinzani mtapewa nchi muongoze 2080 uko labda ila kwa sasa mwacheni magufuli na ccm tumeielewa sana serikali ya sasa
      nyie mjipange kwanza endeleeni kukumbatia mafisadi
      Mungu mbariki Magufuli

      Delete
    2. wapinzani labda 3040 ila kwa sasa mwacheni JPJM na ccm imebadilika sana kwa sasa nyie ukawa endeleeni kukumbatia mafisadi na wengine wanashamba limekuwa pori kuligawa kwa maskini hawataki

      Delete
    3. Wapinzani ni wachochezi. Wapinzani ni wahujumu uchumi. Wapinzani ni mafisadi. Wapinzani hamfai lolote wala chochote. Mna tabia ya kuwa vigeugeu kwa kauli ilimradi tu msababishe fujo na kutaka huruma ya wananchi.

      Natamani wapinzani wote wa sasa wakae pembeni tupate wapinzani wengine walio waungwana na wazalendo. Mbowe, Lissu, Lema, Mnyika, Mdee (kutaja kwa uchache), wamechoooka. Hawana jipya, wanatafuta ulaji posho tu. Tuondokeeni. Period!!!!!

      Delete

Top Post Ad