Naibu Waziri wa Afya, Dk Khamis Kigwangalla Aupa Siku 60 Uongozi Wa Hospitali ya Rufaa Mbeya Kununua Mashine ya CT Scan

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo, Jinsia, Watoto na Wazee, Dk Khamis Kigwangalla amewapa siku 60 viongozi wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Mbeya (MRH) wawe kununua mashine ya CT-scan.

Dk Kigwangalla alitoa agizo hilo juzi jioni, baada ya kuwasili jijini Mbeya ghafla na kwenda moja kwa moja kwenye hospitali hiyo na kupokea taarifa iliyoeleza pia kwamba ni ya kanda, lakini haijawahi kupata mashine za CT scan.

Kukosekana kwa CT-scan kumesababisha wagonjwa kwenda Dar es Salaam au watumie mashine ya mtu binafsi iliyofungwa jijini hapa miaka miwili iliyopita.

“Haingii akilini mtu binafsi hapahapa Mbeya anamiliki CT-scan, lakini hospitali kubwa kama hii imekosa,”alisema.

Dk Kigwangalla alishangazwa zaidi aliposikia kuwa mapato ya hospitali hiyo ni zaidi ya Sh500 milioni kwa mwezi.

“Sasa nawapa siku 60 nataka kuona mashine hiyo imefungwa, vinginevyo mtakuwa mmeshindwa kazi, nitakula sahani moja na nyie viongozi,” alisema.

Aliwataka watumishi wa hospitali hiyo kuwa na mawazo chanya kwa maendeleo na kutoa mfano wa CT-scan nzuri na ya kisasa kama ile iliyonunuliwa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MHN) inauzwa Sh3 bilioni jambo ambalo wanaweza kulitekeleza badala ya kusubiri Serikali iwapelekee.

Awali, Mkuu wa Kitengo cha Maabara cha hospitali hiyo, Abednago Mwakila alisema mbali ya kukosa mashine hiyo kwa miaka yote, nyingine zilizopelekwa hapo hazifanyi kazi baada ya kuharibika na hawajui mafundi wanapatikana wapi.

Alitoa mfano wa mashine ya kuangalia mgando wa damu aliyodai ni kifaa muhimu, lakini haifanyi kazi kwa zaidi ya miaka minne kutokana na kukosekana kwa fundi.

Baada ya kuelezwa hivyo, Dk Kigwangala aliuagiza uongozi wa hospitali hiyo kuorodhesha mashine ambazo hazifanyi kazi na kumpelekea ofisini aweze kufanya utafiti na kubaini watu walioingia mkataba na Serikali wapeleke mashine hizo.

Kaimu Mkurugenzi wa hospitali hiyo, Dk Idsory Thomas alisema agizo lililotolewa na Dk Kigwangalla litatelekezwa kwa wakati.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kwa nini wanaficha kusema kama kifaa kimeharibika mpaka waziri aende

    ReplyDelete
  2. Hongera Waziri Kigwangala kwa kutambua matatizo ya vifaa ktk Hospitali yetu ya Rufaa Mbeya! kwakweli unastahili Uwaziri kabisa na si Naibu Waziri.

    ReplyDelete
  3. Jamani haya majipu ya kizembe hapa nchini kwetu yataisha mwaka gn hongera Mr kingwalangwala hapa kazi tuu

    ReplyDelete

Top Post Ad