Polisi Yavamia Harusi, Wakamata Bwana Harusi na Watu Wake Kwa Kuhusishwa na Kesi ya Ujambazi Access Bank

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Baada ya kupitapita huku na kule katika maeneo yaliyotokea kadhia ya ujambazi jana nilifanikisha kunasa tukio Moja maeneo ya Chulwi Kongowe Mbagala kama sijakosea.

Mnamo 27.2.2016 majira ya SAA 12 jioni polisi walivamia harusi iliyokuwa ikifungwa msikitini na kuwakamata watu waliokuwemo ndani wakiwatuhumu kuhusika na Ujambazi uliofanywa siku ya tarehe 26.2.2016 katika tawi moja la Bank ya Access lililoko Mbagala.

Raia walisema polisi ilivamia msikiti na kuwakamata walimu wa dini waliokuwa wakifungisha ndoa hiyo na kuwachukua na kwenda nao hadi ilipo harusi na kuwakamata wengine huku wakiwapiga na kuwatuhumu kuwa wamehusika na ujambazi.

Hata hivyo polisi ilimwachia huru bibi harusi na kuondoka na babu harusi na wapambe wake sehemu kusiko julikana.

Miongoni mwa watu waliokamatwa ni Abdullah Saudi, Juma selemani, Saidi Ally na kassimu Othuman wote wakiwa wakazi wa Mbagala waliokuja kusheherekea harusi ya rafiki yao.

Chanzo: Jamii Forums
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mwandishi sio uzuri kuandika habari kama vile unahisia waliokamatwa wameonewa na kuleta taharuki ktk jamii kama vile waliouliwa ktk ujambazi sio binaadamu fikiri kile kitendo kilichofanyika ni cha kinyama na polisi hawataingia msikitini au kanisani na kukamata watu hovyo isipokuwa wana uhakika wanachokifanya jamani tuwe na ubinadamu sheria haichagui mtu awe padri au imamu achilia mbali waumini wasitumie udini kuficha uhalisi wao majizi au majambazi lazima washughulikie

    ReplyDelete
  2. @anonymous 12:42 polisi washafanya uvamizi wa misikiti bila ya uhakika mara nyingi tu,polisi awafanya kazi yao kimaadili hilo lipo wazi tuu isipokuwa kuhusu suala hili yawazekana a walipata taarifa maana hao walichofanya ni kitengo cha kinyama na wanastahili adhabu kali cha muhimu wahakikishe wanakamata wahusika wa tukio na sio raia wema

    ReplyDelete

Top Post Ad