Ushirikiano wa Zitto Kabwe na Mbowe Bungeni Waacha Maswali Mengi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Zitto Kabwe na Mbowe
 Kuna siri gani? Ushirikiano wa mahasimu wa kisiasa wa upinzani; Zitto Kabwe wa ACT Wazalendo (Kigoma Mjini) kwa upande mmoja na Freeman Mbowe wa Chadema (Hai) na Ukawa kwa upande mwingine kupinga uamuzi wa Serikali bungeni umevuta hisia za Watanzania na kuacha maswali iwapo ni urafiki wa mashaka au ni wa muda mfupi.

Uhusiano huo wa Zitto na viongozi mbalimbali wa Ukawa ambao umedumu kwa wiki moja sasa, umeibua maswali kama utadumu au ni kwa ajili ya kusimamia hoja zao bungeni.

Zitto na Mbowe walionekana wakitabasamu pamoja Jumanne iliyopita baada ya kukutana kutoa tamko juu ya tangazo la Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye kuzuia kurusha matangazo ya moja kwa moja ya Bunge kupitia TBC1 kwa madai ya kubana matumizi ya Serikali.

Tangu Zitto afukuzwe Chadema na kujiunga na ACT- Wazalendo Machi 21, mwaka 2015 kabla ya kuanza kutengwa na viongozi hao wa Ukawa kwa siku za karibuni ameonekana kuwa karibu na umoja huo wa katiba ya wananchi.

Kwa mara ya mwisho, viongozi hao waliunganisha uhusiano wao katika sakata la Escrow mwaka jana lakini baada ya hapo waliendelea kushambuliana hususani wakati wa kampeni za uchaguzi hatua iliyowachanganya zaidi wafuasi wa mabadiliko wa vyama vya upinzani.

Wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanasema, huenda Zitto amebaini kuwa akiendelea kuwa mpinzani pekee asiyekuwa ndani ya Ukawa na asiyekuwa CCM, atakuwa mpweke kisiasa na huenda akaishia kule walikoishia Augustino Mrema aliyekuwa mbunge wa Vunjo na John Cheyo (Bariadi Mashariki) waliokaa bungeni bila kushirikiana na wapinzani wenzao na sasa wameanguka.

Zitto na baadhi ya viongozi wa Chadema na Ukawa wamekuwa wakivutana mitaani na mitandaoni kwa kauli za maudhi tangu Machi 9, mwaka jana, Chadema ilipotangaza kumvua rasmi uanachama kwa madai ya kuendesha mipango ya usaliti wa chama.

Aprili mwaka jana, akiwa wilayani Kyerwa, Mbowe alinukuliwa na gazeti moja la kila siku akisema hawatamruhusu Zitto kujiunga na Ukawa.

Mbowe alitoa kauli hiyo akijibu ombi la ACT la Aprili 15, 2015 kupitia Zitto kwamba, chama hicho kilikuwa tayari kujiunga na Ukawa kama walivyotaka baadhi ya viongozi wa umoja huo akiwamo aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba.

Katika ufafanuzi wake, Mbowe alisema hawamwamini tena Zitto kwa madai kuwa akiingia Ukawa atakuwa akivujisha siri za umoja huo kwenda CCM lakini Zitto alisema Taifa limekuwa na shauku ya ACT kushirikiana na vyama vingine kama njia ya kufanikisha malengo ya kuitoa CCM madarakani.

Vilevile Aprili mwaka jana, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Bara, John Mnyika akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika Uwanja wa Furahisha jijini Mwanza, alisema Chadema haiko tayari kuikaribisha ACT-Wazalendo ndani ya Ukawa kutokana na kile alichosema ‘ni adui kwao’.

Tofauti na hali hiyo, tangu mkutano wa pili wa Bunge kuanza, wanasiasa hao wameonekana kushirikiana katika kujenga hoja dhidi ya zile za wabunge wenzao wa CCM au Serikali.



----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ni kweli kwenye siasa hakuna adui au rafiki wa kudumu.Wakiwa ndani ya mjengo hawana sababu ya kuwazuia kubadilishana mawazo kwani wote ni WAPINZANI na lengo lao ni lilelile la "kuisulubu Serikali".Siku ukimuona Mh Zitto kwenye ofisi za Chadema au Mh Mbowe kwenye ofisi za ACT hapo utakuwa na mashaka lakini ndani ya mjengo! hiyo mbona ni kawaida kabisa!.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Yes it's hata kwenye ofisi zao Kama kuna dili ya kuutumbua jipu serikali ruhusa ili mradi ni kwa manufaa ya Watanzania

      Delete
  2. Halafu udaku, mbona habari za nyuma siku hizi hatuzioni jamani.. wekeni ili tujikumbushe.

    ReplyDelete
  3. wanasiasa waongo wanagombanisha watu kwa masilaha yao wao wanakaa pamoja na kula bata

    ReplyDelete

Top Post Ad