Wabunge Wageuza Bungeni Uwanja wa Mipasho..Misemo Yatawala...

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Ukumbi wa Bunge juzi uligeuka uwanja wa malumbano na mipasho huku misemo ikichukua nafasi kubwa kutoka kwa wabunge wa chama tawala CCM na upinzani.

Malumbano hayo yalizuka baada ya Bunge kukaa na kujadili Mwelekeo wa Mpango wa Taifa, lakini ghafla wabunge walianza kurushiana maneno wakituhumiana kuwa majipu yanayotakiwa kutumbuliwa.

Katika kikao hicho kilichoongozwa na Mwenyekiti, Mary Mwanjelwa, malumbano yalianza kwa Mbunge wa Viti Maalumu, Jesca Kishoa na Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Harrison Mwakyembe jambo lililoamsha mjadala mzito.

Kishoa alianza kumtaja Dk Mwakyembe kuwa ni jipu linalohitaji kutumbuliwa na Rais na kuwa nafasi aliyonayo hakustahili.

Kishoa alitaja sababu ya kumwita Dk Mwakyembe si msafi kwamba alitumia zaidi ya Sh238 bilioni kwa ajili ya kununulia mabehewa ambayo yalithibitika kuwa ni mabovu.

Kitendo hicho kiliamsha hasira za Dk Mwakyembe na kusimama kisha kukana Serikali kutumia kiasi hicho huku akisisitiza ikithibitika kuwa ni kweli yuko tayari kujiuzulu wadhifa huo.

Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Bunge, Jenista Mhagama alisimama mara kadhaa kutaka Kishoa afute kauli lakini upinzani ulimtetea mbunge huyo.

Hata hivyo, Mwanjelwa aliwataka kuendelea na mjadala ili akaangalie kwanza kumbukumbu za Bunge kuhusu maneno yaliyotamkwa na baadhi ya wabunge.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Lazima liwe hivyo
    CCM kuwaita wabunge WA upinzani
    Mwanafunzi wangu
    Mdogo wangu it's fuck fuck
    Wote ni wabunge wanavyeo sawa
    Na hawa ma dr Na maprofesa bungeni si chuo cha taaluma
    Nafikiri imefuka wakati watu waitwe majina Yao
    Magufuli anza mweyewe
    Kwani kuna tanaka la wabunge hujiona wao bora kwa taaluma zao bungeni
    Bunge linaendeshwa kwa Hoja Na sheria

    ReplyDelete

Top Post Ad