Watu 21 Mbaroni Kwa Kukatakata Mbuzi 75 Mvomero.

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Jeshi la polisi mkoani Morogoro limewakamata watu 21 wanaosadikiwa kuhusika na uhalifu wa kukatakata mbuzi zaidi ya 70 wilayani Mvomero mkoani Morogoro.

Waliokamatwa ni wenyeviti wa vijiji vya Mkindo, Dihombo na Kambala kwa tuhuma za kukata mifugo ya mfugaji mmoja wa jamii ya kimasai, na mmoja kati yao ambaye ni mfugaji akituhumiwa kulisha mifugo kwenye mashamba ya wakulima.

Akizungumza kuhusu chanzo cha kikundi hicho cha wakulima kuvamia na kukatakata mifugo, kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Leonard Paulo, amesema kundi la Ng’ombe zaidi ya 50 likiwa na wachungaji watatu wa jamii ya kimasai, waliingia kwenye shamba la mpunga la hekari moja la Rajab Issa, mkazi wa Dihombo, ambapo mmiliki wake aliwazuia Ng’ombe hao, lakini walijitokeza vijana wanaosadikiwa kuwa morani wa kimasai na kuwachukua ng’ombe hao kwa nguvu, jambo lililofanya mmiliki wa shamba hilo kuripoti tukio hilo polisi.

Kamanda Paul amesema wakati tukio hilo likishughulikiwa na polisi, kikundi cha kijadi cha wakulima maarufu kama mwano kilivamia nyumbani kwa mfugaji wa kimasai, Bi Nuru Keteboi, akiwa nyumbani huku mifugo yake aina ya mbuzi, kondoo na ndama wakiwa malishoni, na kumpokonya simu ya mkononi asiweze kuomba msaada, badala yake wakaipeleka mifugo hiyo porini na kuwakata kata kwa vitu vyenye ncha kali na kusababisha baadhi yake kufa na wengine kujeruhiwa.

Jeshi la polisi limetoa wito kwa wananchi kuheshimu sheria na kutojichukulia sheria mkononi kwani kwa kufanya hivyo kutaleta uhasama usio na sababu za msingi
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad