Waziri wa Afya Ummy Mwalimu Atembelea Hospital ya Muhimbili Kukagua Utekelezaji wa Agizo la Rais Magufuli

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu ametembelea hospitali ya Taifa Muhimbili kukagua utekelezaji wa agizo la Rais John Magufuli la kuwataka watumishi wa wizara hiyo waliokuwa wakilitumia jengo la Kitengo cha Afya ya Uzazi na Mtoto kuhamisha ofisi zao na kuliacha kwa ajili ya matumizi ya wodi ya wazazi.
Akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo katika hospitali hiyo, Waziri Ummy amesema kuwa mpaka kufikia kesho tayari jengo hilo litakuwa limeanza kutumika kwa kuwa watafanya kazi ya kuhamisha makabrasha ya watumishi hao usiku kucha kuhakikisha agizo la Rais John Magufuli linatekelezwa mara moja.

Picha mbalimbali zinaonesha Waziri Ummy Mwalimu akikagua utekelezaji wa agizo la Rais John Magufuli pamoja na watumishi na vibarua wakihamisha nyaraka na makabrasha mbalimbali kutoka kwenye jengo lililokuwa likitumiwa kama ofisi na watumishi wa wizara hiyo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es Salaam.






-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. bravo mh magufuli tunapenda kuona utendaji kama huo na bei ya vyakula tunataka ishuke

    ReplyDelete
  2. Tunamshukuru mungu kwa kututeulia magufuli

    ReplyDelete
  3. Mzigo waziri
    Kwani alipokwenda kumuona mufriti hakuchunguza haya
    Magufuli hawa mawaziri wanaongozwa Na Na wasaidizi wao fukuza

    ReplyDelete
  4. Inaelekea awamu ina ufisadi kwenye vyombo vya habari ili waonekanekani wanafanya kazi
    Nyinyi vyombo habari nafikiri mna kitu hapa
    Fichueni Na maovu Yao
    Magufuli unaendesha nchi kwa media ?

    ReplyDelete

Top Post Ad