Diamond Platnumz Ukishindana na Juma Nature Jukwaa Moja Utaaibika

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Zikiwa zimepita siku kadhaa tangu msanii mkongwe wa Bongofleva Juma Nature kufunguka kwenye kipindi cha Friday Night Live (FNL) na kusema kuwa anahitaji shoo moja tu uwanja wa taifa ambayo itamkutanisha yeye na msanii ambaye kwa sasa anasumbua kwenye Bongofleva Diamond Platnumz ili kuona nani ni mkali kati yao.

Mashabiki kwenye ukurasa wa Facebook wa (EATV) walifunguka mambo mengi na wapo watu ambao wanamuunga mkono Juma Nature wakisema kuwa Diamond Platnumz hatauweza muziki wa Juma Nature stejini huku wengine wakisema kuwa Juma Nature kwa Diamond Platnumz bado sana, mvutano wenyewe ulikuwa kama hivi:-

"Diamond ataaibika sana siku akipanda jukwaani kupambana na Sir Juma Nature, asijekubali suala hilo, maana yeye (Diamond) hata awe na Dancers wake, Nature akiwa peke yake tu anatosha kuwaamsha watu, tena uwanja wa taifa pale ndio hata asithubutu," aliandika Harrison Haroun Makaye.

"Kujaza uwanja na kushangiliwa na mashabiki haikusaidii kitu nyanyuka ushindane kimataifa, kweli unajua kuimba ila tatizo Diamond haimbi muziki kwa kushindana na mtu. Na wala hajawai kutangaza kuwa yeye ndio anajua kuimba," hii ni kwa mujibu wa Phemmy Mkuyawa
"Diamond nyimbo zake ni za kuwaburudisha na kuwafurahisha masisita du, lakini mzee mzima Juma Nature mistari yake inasomeka na inakubalika kwa watu wote na rika zote na haina powder wala nini," Fine Jerry naye alifunguka hivyo.

"Ha ha ha ha bado haijaniingia hiyo. Juma Nature na Diamond wapi na wapi? labda angesema tumpambanishe yeye Juma Nature na wasanii kama kina Chege au Temba hao! ndiyo type yake, ila King Kiba ndiye apambane na Dangote siyo yeye mimi hilo sijaafikiria kabisa," Joyce Jackson aliposti mawazo yake hayo.

"Wajinga wajinga ndiyo watasema Diamond mkali kuliko Nature msiangalie visenti au video au kaimba na wasanii wa Nigeria, swali nani mkali kwa kuimba, Diamond mjanja wa kusaka hela na mishe anaziweza ila kwa kuimba hata Ali Kiba anamzidi. halafu Nature kuimba ni nature yake sio anaekti," Rabi Intocavel naye alitupia hiyo.

Hizo ni baadhi ya Comments za watu kutoka kwenye ukurasa wa Facebook wa (EATV) ambapo mashabiki bado wanaendelea kuvutana wengine wakisema Juma Nature atamkalisha chini Diamond Platnumz kama shoo hiyo itakuja kufanyika huku wengine wakisema kuwa Diamond Platnumz si wa kushindana na Juma Natute wakiwa na maana kuwa lazima atamshinda Juma Nature.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

7 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. JUMA NATURE ANATAFUTA KIKI.

    ReplyDelete
  2. vichekesho kweli!!! jamani juma kumshinda diamond?????

    ReplyDelete
  3. Kweli nimeamini bangi ikizidi sana kichwani mtu anakuwa na vision tofauti na real life sometimes mtu hujiona kuwa anaweza kuruka angani kama ndege wakati kitu kama hicho siyo kweli

    ReplyDelete
  4. Du hizi kiki nyingine jamani!!!

    ReplyDelete
  5. mziki wa nature zamu yake ilipita zamani sawa na kumshindanisha Chritian Bella na Muumin Mwinjuma,Nature alijisahau kwa maulevi yao hadi mashavu yamemvimba kwa athari za kuberi,pumzi na stamina ya Diamond haiwezi tena

    ReplyDelete
    Replies
    1. SURE ENZI ZILEEEE SIO SASA!!!

      Delete

Top Post Ad