Gavana BOT Afunguka Kuhusu Watoto wa Vigogo Walioajiriwa Bank Kuu...Adai Hakuna Jipya Kama Wanasifa Kwanini Wasiajiriwe?

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Hatimaye Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Prof. Benno Ndulu amefunguka kuhusu hatma ya watoto 14 wa vigogo wanaodaiwa kuajiriwa kwa kubebwa katika taasisi hiyo nyeti kwa mustakabali wa taifa kiuchumi.

Akizungumza na Nipashe kwa njia ya simu jana, Prof. Ndulu alisema orodha hiyo, ambayo mwandishi alimsomea kuanzia mwanzo hadi mwisho, haina jipya.

Prof. Ndulu alisema hakuna ubaya wowote kwa mtu mwenye sifa kuajiriwa na BoT, bila kujali jina lake.
Kuanzia juzi na jana, orodha ya majina ya watu 14 wanaotajwa kuwa ni watoto wa vigogo waliopo BoT ilikuwa ikisambazwa kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii.

Mjadala katika mitandao hiyo ilikuwa huenda wapo watakaoguswa katika kutekeleza agizo la Rais John Magufuli aliyeitaka BOT kupunguza wafanyakazi wake wasiokuwa na shughuli muhimu za kufanya kutoka jumla ya wafanyakazi 1,391.

Rais Magufuli alitoa agizo hilo juzi baada ya kufanya ziara ya ghafla kwenye benki hiyo na kutoa maelekezo kadhaa kwa uongozi wa juu, akiwamo Gavana Prof. Ndulu.

Majina ya watoto hao wa vigogo ambayo yamesambaa kwenye baadhi ya mitandao, yameendelea kuibua maswali mengi kuhusu hatma yao BoT.

Wengi wa wachangiaji wanadai kilichowapatia ajira ni ushawishi wa majina makubwa ya wazazi wao katika medani za uongozi nchini na siyo sifa za kuajiriwa kwenye taasisi hiyo.

Alipoulizwa suala hilo jana, Prof. Ndulu hakutaka kuzungumzia kwa kina, lakini alisema majina hayo siyo mapya na kwamba yalishaandikwa na kujadiliwa mara nyingi hapo kabla.

“Hayo majina kwani kwako wewe ni mapya? Mbona yameshaandikwa na kujadiliwa sana hayo… mimi nasema hakuna jipya hapo,” alisema Prof. Ndulu na kuongeza:

“Hivi ukiwa na jina kubwa halafu ukiwa na akili ama sifa za kufanya kazi fulani, unataka kuniambia usipewe hiyo kazi kwa sababu una jina kubwa?”

Kwa kauli, ni dhahiri tafsiri Prof. Ndulu ana maana kwamba watu hao wenye majina makubwa walipata kazi kwa sifa zao na siyo majina ya wazazi wao kama inavyovumishwa kwenye kurasa za mitandao mbalimbali ya kijamii.

ORODHA YENYEWE
Orodha ya watu wanaodaiwa kuwa ni ya watoto wa vigogo, na ambayo Prof. Ndulu alisema siyo mpya kwani ilishaandikwa na kujadiliwa sana hapo kabla ni pamoja na Pamela Lowasa, anayedaiwa kuwa ni mtoto wa aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowasa.

Wegine ni Filbert Sumaye anayedaiwa kuwa ni mtoto wa Waziri Mkuu mstaafu katika serikali ya awamu ya tatu, Fredrick Sumaye na Zaria Kawawa, anayedaiwa ni mtoto wa aliyewahi kuwa Waziri Mkuu katika serikali ya awamu ya kwanza, Marehemu Rashid Mfaume Kawawa.

Mwingine ni Harriet Lumbanga anayedaiwa ni mtoto wa aliyewahi kuwa Katibu Mkuu Kiongozi wakati wa utawala wa serikali ya awamu ya tatu, Marten Lumbanga.

Aidha, orodha hiyo pia ina jina la Salama Ali Hassan Mwinyi anayedaiwa ni mtoto wa aliyekuwa Rais wa awamu ya pili, Alhaji Hassan Mwinyi; Rachel Muganda anayedaiwa ni mtoto wa aliyekuwa Balozi katika serikali ya awamu ya nne, Alexender Muganda.

Salma Omar Mahita, katika orodha hiyo anadaiwa kuwa ni mtoto wa aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi wakati wa utawala wa awamu ya tatu, IGP mstaafu Omar Mahita.

Wengine ni Justina Joseph Mungai anayedaiwa kuwa ni mtoto wa aliyewahi kuwa Waziri wa Elimu na Utamaduni katika serikali ya awamu ya tatu, Joseph Mungai.

Pia yumo Keneth Nchimbi anayehusishwa na kada wa CCM aliyewahi kuwa kigogo wa Jeshi la Polisi John Nchimbi.

Blasia William Mkapa, anadaiwa kuwa ni mtoto wa Rais wa awamu ya tatu, Benjamin Mkpa katika orodha hiyo yenyep ia jina la Violet Phillemon Luhanjo, ambaye anadaiwa kuwa mtoto wa aliyewahi kuwa Katibu Mkuu kiongozi wakati wa serikali ya awamu ya tatu na nne, Phillemon Luhanjo.

Liku Kamba anadaiwa kuwa mtoto wa aliyekuwa kada wa CCM wa muda mrefu, Kate Kamba.

Wengine wanaotajwa katika orodha hiyo ni Thomas Mongela anayedaiwa kuwa mtoto wa kada mashuhuri ndani ya CCM; aliyewahi kushika nyadhifa mbalimbali zikiwamo za ubunge, Getrude Mongela.

Jina la Jabir Abdalah Kigoda linadaiwa kuwa ni mtoto wa aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara katika serikali ya awamu ya nne, marehemu Abdalah Kigoda.

KUPUNGUZA WAFANYAKAZI 
Juzi, miongoni mwa maagizo aliyoyatoa Rais Magufuli wakati wa ziara yake ya kushtukiza, ni pamoja na kumtaka Gavana Ndulu kupitia upya orodha ya wafanyakazi wa benki hiyo na kuwaondoa ambao hawana ulazima wa kuwapo.

Rais alielezea kushangazwa kwake na kitendo cha BoT kuwa na wafanyakazi wanaofikia 1,391.

Alipoulizwa kuhusu kupunguza wafanyakazi BoT kama ilivyoagizwa na Rais Magufuli, Prof. Ndulu alisema hayo yatafanyika baada ya vikao vya ndani na kwamba baada ya hapo, Benki Kuu itatolewa taarifa rasmi ya matokeo ya maagizo ya Rais.

Prof. Ndulu alisema si vyema, na wala haamini kuwa ni busara kuzungumzia masuala yanayowahusu wafanyakazi wa BoT kwa vyombo vya habari na badala yake, masuala hayo yatazungumzwa kwenye vikao vya ndani vya menejimenti ya benki hiyo.

“Haya ya kuwaondoa baadhi ya wafanyakazi tutayazungumza kwenye vikao vya ndani kisha tutaandaa na kutoa tamko," alisema Prof. Ndulu.

"Mambo haya si ya kuyazungumza kwenye vyombo vya habari, hata wewe masuala ya wafanyakazi wenu hamyaweki magazetini holela holela tu.

"Nomba niachieni nafasi jamani.”
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

9 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Duuuuh...benki nzima imejaa wana ccm..mbona sioni watoto wa mbowe au tundu lissu hahahahaha aiseee uozooo

    ReplyDelete
    Replies
    1. Yupo mtoto wa raisi wenu fisadi Lowasa

      Delete
  2. Kwa nini kil;a mtoto wa mkubwa yuko hukoooo????? Kwani hakuna taasisi nyingine ambazo wangeweza kuzitumikia kwa taaluma hizo hizo zaidi ya Benki Kuuuu????? Kuna jambo hapo sio siri na hii hali ya kulindana lindana sasa itawatokea puani.

    ReplyDelete
  3. Inawezekana vipi Benki Kuu ya Taifa lililo maskini Duniani ikawa na wafanyakazi zaidi ya 1300??? Haingiii hata akili, utafikiria ni Kiwanda cha kutengenaza Sukari ama Magodoro, Hata baadhi ya viwanda tena vyenye ufanisi mkubwa havina idadi hiyo ya wafanyakazi. Halafu cha ajabu watoto woootee wa wakubwa ndio wameenda huko kajificheni shamba la bibi. Ni lazima huo muundo wa Benki Kuu uangaliwe upya hata ikiwezekana wabakie wafanyakazi wasiozidi 100 kulingana na muundo wake. Hilo ni Taifa la kimaskini sana lka kuwa na wafanyakazi 1300 katika taasisi kama hiyo.

    ReplyDelete
  4. Hmmm hapa unaonekana ni mwendo wa majina tu au mtoto wa furani. Hata kama una sifa lakini si mtoto wa furani. Kuna walakini kupata. Na iweje watoto wa furani tu? Hmmm hapa kuna walakini wa kuwekana. Hamna cha qurificaton wala nini? Wasitudanganye hawa nyani weusi. Wabaya kweli hawana hata ubinadam

    ReplyDelete
    Replies
    1. furani = Fulani
      qurificaton = qualification

      kwa uandishi huo hata silaumu hao watoto wa vigogo kupewa nyadhifa benki kuu.

      Delete
  5. Hmmm hapa unaonekana ni mwendo wa majina tu au mtoto wa furani. Hata kama una sifa lakini si mtoto wa furani. Kuna walakini kupata. Na iweje watoto wa furani tu? Hmmm hapa kuna walakini wa kuwekana. Hamna cha qurificaton wala nini? Wasitudanganye hawa nyani weusi. Wabaya kweli hawana hata ubinadam

    ReplyDelete
  6. SISI ASITUAMBIE KITU NA WALA HATUTAKI MAELEZO YAKE KWA SABABU HATUJAMTUMA SISI KAPEWA AGIZO NA RAIS AFU ANALETA BLAABLAA ATATUMBULIWA YEYE,,KWA MAANA HIYO ANABISHANA NA RAIS MWENYE DHAMANA YA KUTUMBUA MAJIPU.

    ReplyDelete
  7. hahahahahaha magufuli hilo nijipuu tutumbulieeee haiezekan majina yote makubwa wawe bank kuuu kwan hakuna idara zingne au vitengo mahala kwingne serikalini wakaekwaa................hapoo hamna kitu..full kujuanaa hatutaki watanzania mmetulaa sanaa sasa nikutumbuliwaa tuu

    ReplyDelete

Top Post Ad