Kiba Amlipua Jokate...Adai Hakuwa na Mpango wa Kudumu Naye Kimapenzi....

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Staa anayesumbua na wimbo wa Lupela, Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’ amedaiwa kumlipua Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ kwa kusema hakuwahi kuwa na mpango wa kudumu naye penzini, Risasi Jumamosi linakupa ubuyu kamili.

Hivi karibuni, Jokate alizungumza na wanahabari wa Global Publishers na kudai amemchoka mpenzi wake huyo hivyo ameamua kumuacha rasmi Kiba ambapo habari hiyo ilichapwa jana kwenye Gazeti la Ijumaa.

Chanzo kilicho karibu na Kiba kimeweka bayana kuwa mkali huyo hakuwa na mpango na penzi la Jokate lakini alilazimika kuwa naye karibu kwa shughuli za kikazi (muziki).

“Tunamshangaa Jokate kusema eti amemchoka Kiba leo wakati anajua kitambo tu Kiba hakuwa na mpango naye. Kiba alilazimika ‘ku-fake’ penzi kwa sababu walikuwa wanafanya kazi za pamoja, hakuwa na jinsi.

“Jokate mwenyewe anajua kwamba Kiba hakuwa na mpango naye. Nafikiri kajitokeza kwenye ‘media’ ili aonekane yeye ndiyo kamuacha Kiba kumbe mwenzake hata hakuwa na mpango wa kuwa naye,” kilisema chanzo hicho.
Gazeti hili lilimtafuta Kiba katika simu yake ambapo alidai hapendi sana kuanika mambo yake binafsi kwenye vyombo vya habari lakini mmoja wa mameneja wake aliyeomba hifadhi ya jina, alifafanua suala hilo.

“Kiba hakuwa na mpango na Jokate na ndiyo maana kila siku tunapokuwa kwenye kazi zetu hapendi umtajie ishu za Jokate hata kidogo na alikuwa akisisitiza kweli lakini sisi tulikuwa tunalazimisha waendelee kwa sababu tulikuwa tunafanya kazi za pamoja,” alisema meneja

Chanzo:Global Publishers
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kwa maana hiyo Bongo hakuna uwezekano wa wanaume na wanawake kufanya kazi pamoja bila kuwa na uhusiano ki ngono?

    ReplyDelete
  2. pumbavu zako wewe Ali kiba na wala hukupata umaarufu kutoka Jokate na wala hutopata umaarufu kwanza Jokate ni mrembo sana kukuzidi wewe na sura yako mbaya kama shetani, ndiyo maana Nassibu Abdul au Dangote amekupita sana mpaka Nassib anamiliki mjengo, wewe Ali kiba una nini hauna. Na mziki wako mbaya haufiki popote, huo ndio ukweli. Diamond is a king for real

    ReplyDelete
  3. na wala Jokati hakukupenda alikuwa na bwana mwingine pembeni yako mimi ni rafiki na Jokate, tena Jokate alisema wewe ali kiba hakupendi na unayo sura mbaya bali alimpenda yule bwana mwingine wa pembeni. He he shame on you Ali kiba

    ReplyDelete

Top Post Ad