Mama Diamond Atoa Siri ya Zari

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mama mzazi wa staa wa Afro-Pop, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Sanura Kassim ‘Sandra’ ametoboa siri ya mkaza mwanaye, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ kushindwa kuishi Bongo na badala yake kukimbilia nchini Afrika Kusini ‘Sauz’.

Sandra au Mama D aliyasema hayo katika mahojiano maalum na Ijumaa Wikienda juu ya uhusiano wake na Zari kufuatia tetesi kuwa hawaivi ndipo akaweka mambo sawa.

Mama D alisema kuwa yeye na Zari wapo vizuri lakini kinachomfanya mkwewe huyo kushindwa kuishi naye Bongo ni kutokana na biashara zake kudoda nchini Afrika Kusini.

“Unajua anapokuwa huku (Bongo), biashara zake huwa zinayumba sana, wakati mwingine akipiga simu akiulizia biashara zinakwendaje anaambiwa hali ni mbaya au hazijaingiza chochote hapo ndipo huwa anachanganyikiwa.

“Kwa mfano hivi karibuni alipiga simu akaambiwa hakuna fedha kabisa na biashara haziendi. Kilichofuata ni kujiandaa na kumchukua Tiffah (Latifah Nasibu) kisha akaondoka zake.

“Hicho ndicho kinachomkimbiza Zari kuishi Bongo na si kweli kwamba hapapendi au kuna tatizo lolote,” alisema Mama D.

Chanzo:GPL
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mi lijua hakai kwasababu ya watoto wake kumbe biashara kazi kweli kweli

    ReplyDelete
  2. sasa yeye si levo nyingine imekuaje hana pesa?

    ReplyDelete
  3. SI MLISEMA KAPEWA MGAO WA VODA.KIKO WAPI SASA.

    ReplyDelete
  4. he! tajiri anahaha hana pesa? innallillah wainaillahiraajiun.

    ReplyDelete
    Replies
    1. tehe tehe kwani kafa mpaka umsomee sala ya mfu?

      Delete

Top Post Ad