Mbunge wa Kilombero Peter Lijualikali Akamatwa..

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Jeshi la Polisi  Mkoani Morogoro, wilayani Kilombero  jana  lilimkamata mbunge wa jimbo la Kilombero (Chadema), Peter Lijualikali kwa madai ya kutaka kuingia katika kikao cha Baraza la Madiwani cha kuapisha na kuchagua mwenyekiti na makamu wake wakati si mpigakura.

Lijualikali alikamatwa nje ya ukumbi wa halmashauri na polisi na kuswekwa rumande katika Kituo Kikuu cha Polisi Wilaya ya Kilombero saa 3.48 asubuhi wakati akiingia kwenye ukumbi huo kama mmoja wa mashuhuda.

Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Kilombero, Shabaan Mikongolo alisema mbunge huyo hakutendewa haki na polisi kwa kuwa alifika eneo hilo kushuhudia matukio ya kuapishwa kwa madiwani.

“Ni kama kuna maelekezo yalitolewa kwa polisi kuwazuia wabunge, Lijualikali na Devotha Minja (Viti Maalumu – Chadema) na mwakilishi wa Katibu Mkuu Chadema kutoingia ukumbini lakini viongozi wengine wa Serikali ngazi ya mkoa na wilaya waliruhusiwa." Alisema Mikongolo

Pia, polisi walizuia waandishi wa habari na kutaka kuwanyang’anya kamera zao kwa sababu ambazo hazikuwekwa bayana.

Katika uchaguzi huo, Diwani wa Sanje (CCM), David Ligazo alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kilombero kwa kura 19 dhidi ya Godfrey Lwena ( CHADEMA)  aliyepata kura 18
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Je kwa nini Raisi Magufuli upo kimya. Unaachia watu wa chama chako wakishirikiana na polisi wamo kuwanyanyasa wapinzani. Bado kikkwete na genge lake linahujumu wapinzani.ulisema wewe utamuwa raisi wa watu wote. Lakini unawaachia polisi kuburuga amani. Tuanashuhudia Morogoro na Dar.ebu fumuza hawa polisi wanaoshirokiana na watu wa chama chako..

    ReplyDelete

Top Post Ad