Polisi Wafanya Upekuzi Nyumbani Kwa Halima Mdee

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam jana lilifanya upekuzi mkubwa katika nyumba ya Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (Chadema) baada ya kumtilia shaka kuwa na nyaraka muhimu za vikao vya uchaguzi wa Meya wa Jiji hilo.

Kikosi cha jeshi hilo kilifika katika nyumba ya mbunge huyo majira ya saa tisa alasiri na kufanya mazungumzo na Mwanasheria wake, John Mallya ambapo baada ya kukamilisha taratibu za kisheria walianza zoezi la upekuzi uliochukua zaidi ya saa moja.

Kiongozi wa kikosi hicho cha Polisi, aliwaambia waandishi wa habari kuwa walilazimika kufanya upekuzi katika nyumba hiyo baada ya kusadikika kuwa wakati wa vurugu zilizotokea katika ukumbi wa Karimjee jijini humo wikendi iliyopita kufuatia kuahirishwa kwa uchaguzi wa Meya wa Jiji, Mdee aliondoka na faili muhimu lenye madokezo yanayohusu uchaguzi huo.

Hata hivyo, baada ya kukamilisha upekuzi huo, Polisi walijiridhisha kuwa hakukuwa na nyaraka hizo ndani ya nyumba hiyo wala kitu chochote ambacho wangekitilia shaka licha ya kukuta nyaraka nyingi za mbunge huyo. Hivyo, walitoa cheti maalum cha kuthibitisha kuwa hakuwa na nyaraka zozote kinyume cha sheria.

“Wamekagua nyaraka zote. Madai yao ni kuwa Halima alimpora au alichukua nyaraka za kiongozi wa Jiji, lakini wamekuta hakuna jambo lolote ambalo linatiliwa shaka. Na wametoa Certificate inayoonesha kwamba hakuna chochote ambacho kimechukuliwa,” alisema Mwanasheria wa Mbunge huyo, John Mallya.

Mdee alishikiliwa na Polisi na kulala rumande juzi kutokana na tuhuma za kushiriki katika vurugu zilizotokea katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam, Jumamosi, Februari 27.

Wengine wanaoshikiliwa na Jeshi la Polisi ni Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea na Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

8 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. hakuna democracy nchi hii yani viongozi wa ukawa wanateswa bila sababu kisa kudai haki, halima anawaumisha vichwa hawalali

    ReplyDelete
  2. Mtoto mdogo lakini akili kubwa, hoja zake nzito. CCM hawana raha. Wakimbize Halima.

    ReplyDelete
  3. Ananyea ndoo mna mpa bichwa mbona hamuendi kumsaidia anawakimbiza na anajikimbiza mwenyewe kwa siasa ipi,,,bongo,,,,

    ReplyDelete
  4. Nani kakosa raha? Anaenyea debe au anaelala kwake na ku enjoy uhuru? Eti awakimbize hahaha. Atasubiri sana na uso wake wa chuping. Msagaji namba one. Na vinguo vyake vya bei rahisiiii.msonyo

    ReplyDelete
  5. Anonymous 10:32 kunywa soda ntalipa

    ReplyDelete
  6. apo halima anawaza kinoma akitoka apo mmbu zimeuma mwili mzima makovu kila mahali
    simpendi huyu dada kwa mitabia yake ya kujifanya dume na akome

    ReplyDelete
    Replies
    1. BRAVO HALIMA NAKUFAGILIA ILE MBAYAAAAAAAA MWANAMKE JASIRI SANA. HONGERA

      Delete
  7. WAKIMBIZEEEEE HALIMA WEEE JEMBE !!!

    ReplyDelete

Top Post Ad