Rais Magufuli Awataka Watanzania Waepuke Misaada ya Masharti Toka kwa Wazungu.....Pia ameahidi Kuwapunguzia Kodi Wafanyakazi Hadi Asilimia 10 au 9

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefika nyumbani kwake katika kijiji cha Mlimani, Wilaya ya Chato Mkoani Geita kwa mara ya kwanza tangu achaguliwe kuwa Rais, ambapo akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa shule ya sekondari Chato, ametoa wito kwa kila mtanzania kuchapa kazi kwa juhudi ili nchi iondokane na utegemezi wa misaada ya wafadhili ambayo huambatana na masharti.

Dkt. Magufuli amesema jukumu kubwa lililo mbele ya watanzania kwa sasa, ni kushikamana na kujisimamia katika maendeleo ili kila mmoja ahakikishe anaongeza uzalishaji na utendaji kazi mahali pake pa kazi.

"Kwa hiyo ni lazima tujisimamie sisi wenyewe, na tukijisimama sisi wenyewe kwa kila mmoja kuwajibika mahali alipo, kama ni mfanyakazi afanye kazi kwelikweli, kama ni mkulima afanye ukulima wake kwelikweli, kama ni mfanyabiashara afanye biashara kwelikweli, kama ni mfugaji afuge kwelikweli, kama ni mvuvi avue kwelikweli, Tanzania hii tutavuka" Amesema Rais Magufuli.

Aidha, Rais Magufuli amesema serikali yake imeamua kuchukua hatua kudhibiti nidhamu serikalini, kwa kuhakikisha inawachukulia hatua watumishi wa umma wanaolisababishia taifa upotevu mkubwa wa fedha, na ameahidi kuwa hatua hizo maarufu kwa jina la "Kutumbua Majipu" zitaendelea kuchukuliwa hadi tatizo hilo likomeshwe.

Dkt. Magufuli pia amekumbusha viongozi wote wakiwemo Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala na Wakurugenzi, kutekeleza wajibu wao ipasavyo na ameweka bayana kuwa mahali popote ambapo hapatakuwa na ufanisi, kiongozi husika atakuwa amedhihirisha kuwa hatoshi kuendelea na wadhifa aliopewa.

Rais Magufuli amewapongeza walimu kote nchini kwa kufanya kazi nzuri ya kufundisha, licha ya changamoto ya ongezeko kubwa la wanafunzi waliojiunga darasa la kwanza mwaka huu, lakini ametaka Wazazi na kamati za shule kushirikiana na walimu kuwasimamia wanafunzi ili waweze kufanya vizuri katika masomo yao.

"Niziombe kamati za shule zote Tanzania nzima, kama haziwezi kusimamia nidhamu ya wanafunzi shuleni, zile kamati za shule zijiuzulu. Lakini pia kama wewe ni Mwalimu Mkuu, shule yako kila siku inatoa divisheni ziro nyingi kila mwaka, sioni sababu ya wewe kuendelea kuwa Mwalimu Mkuu" Alisisitiza Dkt. Magufuli.

Kuhusu tatizo la wafanyakazi hewa, Rais Magufuli amesema uhakiki mdogo uliofanywa hivi karibuni, umebaini wafanyakazi hewa 1,680 waliokuwa wakilipwa shilingi bilioni 1 na milioni 800, na kwamba ni matarajio kuwa uhakiki unaofanywa nchi nzima utaisaidia serikali kubaini wafanyakazi hewa wengi zaidi na kunusuru fedha nyingi zaidi za watanzania.

Ametolea mfano wa mfanyakazi mmoja wa Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA) ambaye alikuwa akilipwa mishahara ya watu 17, na kueleza kuwa mfanyakazi huyo atafikishwa mahakamani.

Pia Rais Magufuli amesema serikali yake imejiandaa kuboresha maslahi ya wafanyakazi kwa kupunguza kodi kutoka asilimia 11 ya sasa hadi asilimia 10 au 9 kuanzia bajeti ijayo, lakini amesema kwa wale wanaolipwa mishahara mikubwa ambayo inafikia hadi shilingi milioni 40, itapunguzwa na kuweka kima cha juu cha mshahara usiozidi shilingi milioni 15.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. ni masharti gani wazungu wamekuwa wakiwapa ili wawape misaadaa?? kwa nini unakuwa muongo?? wao hawana masharti yeyote isipokuwa ni hizo dosari zilizo jitokeza kwenye uchaguzi wameona hii nchi haina demokrasi ya kweli na ndio maana wamekata kutoa msaada. acha longolongo zako, yatakushinda!

    ReplyDelete
    Replies
    1. YAANI KATIKA MAROFA WEWE NI MMOJA WAPO, NA KAMA SIKOSEI UMEZOEA KULETEWA BILA KUFANYA KAZI NA NDIYO MAANA UNASHABIKIA UJINGA WA MISAADA, AU INAWEZEKANA KAMA NI MWANAMME BASI UTAKUWA UNALISHWA NA MWANAMKE BILA KIJIELEWA NA AU WEWE NI CHAKULA YA WENZAKO MAANA HAO UNAWASHABIKIA NI WASHENZI AMABAO MOJA NA MASHARTI WALIYOTOA NI KUWA NA NDOA YA JUNSIA MOJA. KWA HIYO NDUGU YANGU KUWA MWANGALIFU NA COMMENTS ZAKO ZA KIJINGA NA USIJARIBU TENA KUMTUKUNA RAIS WETU KAMA UMEICHOKA NCHI HII WAFUATE HAO MABWANA ZAKO HUKO MAREKANI.

      Delete
    2. Unaweweseka?Pole wee!Mfano wa wazi ni ndoa za jinsia moja.

      Delete
  2. Msaada yenyewe misaada mbuzi, na masharti kibao na wizi juu, Africa na Tanzania zinaibiwa sana kushinda hata hiyo misaada, wanaiba matrioni kwa matrion alafu wenyewe wanatoa vimilioni tu sisi wenyewe tunaona misaada kumbe ni ujinga, wajinga ndio waliwao, ukichukulia na viongozi kina sultani mangungo wasioelewa kama danganya toto, wenye ugumu wa kufikiri na mustakabali wa nchi zao ndio kabisa wanazidi izamisha Africa iliyojaa baraka na neema za utajili duniani

    ReplyDelete
  3. basi msiwe wanafiki mbona mnajipendekezaga kwa wazungu?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wewe ni kuwadi kwa hao wazungu tunakojipendekeza.

      Delete

Top Post Ad