Breaking News:Rais Dkt. Magufuli Amfukuza Kazi Mkuu Wa Mkoa Wa Shinyanga, Mama Anne Kilango Malecela

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzanaia Dkt. John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Mkuu wa mkoa wa Shinyanga  mama Anna kilango Malecelakuanzia leo.


Utenguzi huo umetokana na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo Anna kilango Malecela kutangaza kwenye vyombo vya habari kuwa mkoa wake hauna watumishi hewa jambo ambalo lilisababisha Ikulu kufanya uchunguzi wake na kubaini kuwepo kwa wafanyakazi hewa 45 katika awamu ya kwanza na awamu ya pili ya uchunguzi bado inaendelea.


Akiongea Ikulu jijini Dar es Salaam wakati akipokea hundi ya shilingi bilioni sita zilizotolewa na Ofisi ya Bunge baada ya kubana matumizi kwa ajili ya kununulia madawati, Rais Magufuli ameeleza kusikitishwa  sana na hali hiyo.


Amesema idadi ya wafanyakazi hewa mkoani Shinyanga huenda ikaongezeka zaidi kwani wilaya mbili za mkoa huo bado zinaendelea kuhakikiwa.


Rais pia ametengua uteuzi wa  Katibu Tawala wa Mkoa huo Bw. Abdul R. Dachikwa kumshauri vibaya Mkuu wa Mkoa.

 

Mama Anna Kilango Malecela, ambaye katika awamu ya nne alikuwa Naibu waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi na Mbunge wa Same Mashairiki, anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Kwanza kuachishwa kazi akiwa amedumu katika nafasi hiyo kwa mwezi mmoja tu..
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

17 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hatufanyi kazi kwa mazoea, JPM wanyooshe Tu, hdi tutaheshimu kuwa cheo Ni dhamana na sio amana

    ReplyDelete
  2. Hahaha wacha idadi ya majipu iendelee huu ni utawala wa kutumbua majipu. well done jpm

    ReplyDelete
  3. saaafi saaana Mhs Magufuli, ussiwaachie hawa, piga chini tu, wamezoea kufanya kazi kimazoea na kubebwabebwa, hii siyo AWAMU YA NNE bana, kuoneana huruma huku wananchi wakilia, HAPA KAZI TU!

    ReplyDelete
  4. Hapa tutapata kigugumizi. Mwaya Anna pumzika na mzee wako mle pension isiwe taabu.

    ReplyDelete
  5. Hahahhahahahahhahahahahahah ccm ni ile oooh ni ileee....shinyanga mnasemajeeee hahahah tumejipanga mwaka huu wataisoma wataisoma namba

    ReplyDelete
  6. Hilo jipu mama. Wazembe, wavivu, wala rushwa, wakwepa kodi muda wenu umeisha sasa mtabaki kuisoma namba tu. Hapa kazi tu

    ReplyDelete
  7. Hilo jipu mama. Wazembe, wavivu, wala rushwa, wakwepa kodi muda wenu umeisha sasa mtabaki kuisoma namba tu. Hapa kazi tu

    ReplyDelete
  8. pole sana mwanamke shujaa wa tanzania kwa kupoteza kazi... dah kwa ile kweli nimejisikia vibaya sana kwa hatua aliyochukua huyo mh. ni zaidi ya kukurupuka.,. ameshindwa kukuonya hata onyo la kwanza! utadhani na wewe jipu wa makontena! jamani!! Mungu akutie nguvu naamini wewe ni mwanamke shujaa utasimama!JPM??????

    ReplyDelete
    Replies
    1. fala wew
      inaonyesha jinsi gani ulivyo kilaza

      Delete
    2. majizi unayaita shuja

      Delete
  9. Hili kwa Anna sio jipu ni chunusi. Labda jipu kwa afisa aliyetoa taarifa ya uongo. Ripoti ya uchunguzi angepatiwa RC. Halafu yeye ndio angemfukuza kazi huyo Afisa Tawala.JPM hapa kachemsha. Mwanamke wa shoka kama huyo angepewa onyo tu na kwamba awe makini na watendaji wake lakini dio kumwachisha. Imeniboa.

    ReplyDelete
  10. Mwanamke shujaa wa kuficha majipu sugu? Acheni kuwadhililisha akina mama zetu kwa kuwapa ushujaa wa hovyo,they are far better than that.

    ReplyDelete
  11. Hujamsikiliza hoja zake bungeni?

    ReplyDelete
    Replies
    1. hoja za bungeni na ukuu wa mkoa ni tofauti sana, jamani alipokuwa anaapishwa si mwajili wao aliwaambia wakafanye kazi gani kwanza???? alitakiwa ajiridhishe kwanza kabla ya kutangaza kwenye press, hapa tatizo ni kufanya kazi kwa mazoea, tuache hizo bhana

      Delete
  12. pole mama anne hayo ni mapito tu! kwani hata yeye mtumbua majipu ni binadamu ana madhaifu yake je yeye ni nani atakaye mtumbua jipu?

    ReplyDelete

Top Post Ad