Kwa Makomredi Hawa Museveni Asingeitosa Tanzania Hata Siku Moja Kwenye Bomba la Mafuta....

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Nimekuwa nikilifuatilia kwa umakini mkubwa sana hili suala la wapi Bomba la Mafuta lipite huku Ndugu zetu Wakenya WAKIJITUTUMUA kama kawaida yao kutaka KUMILIKI kila kitu hapa Afrika ya Mashariki kana kwamba Mwenyezi Mungu aliwabariki wao tu wakati si kweli.

Rais wa Kenya Kenyatta pamoja na team wake wamejitahidi na kwa taarifa nilizonazo zinasema kuwa mpaka jana Jumamosi bado Kenya ilikuwa inaendelea na lobbying kwa Rais wa Uganda Mzee Museveni ili apitishe Bomba hilo kwao na Tanzania tuambulie patupu.

Ila Wakenya na hasa Rais wao Uhuru Kenyatta wamesahau historia ya KUTUKUKA ya Rais Yoweri Kaguta Museveni na nchi yetu hii ya Tanzania. Hakuna ubishi kuwa Rais wa Uganda Mzee Museveni bila jitihada za Tanzania leo hii asingekuwa hapo alipo.

Ukianzia zile harakari zake za kuiokomboa nchi ya Uganda akiwa anatokea huku huku Tanzania na wakati huo huo makazi ya familia yake hasa mkewe Janet na Watoto wao wawili wa kwanza wa Kiume Muhoozi Kainerugaba na Natasha Nankuunda ambao waliishi vizuri sana pale Upanga mkabala kabisa na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili huku.

Baada ya Mzee Museveni kumaliza masomo yake UDSM alianza kazi ya kufundisha Chuoni huko Mkoani Kilimanjaro lakini hapo hapo tena akiendeleza harakati zake za kupambana vita ya msituni kuuondoa Uongozi wa Milton Obote akishirikiana na wenzie kama Jemedari Serwanga Lwanga ( R.I.P ), mdogo wake Caleb Akandwabaho ( Salim Salehe ), Kahinda Otafiire, Paul Kagame ( Rais wa Rwanda ), Samson Mande aliyekuwa Ugandan Millitary Attache to Tanzania 1995 - 1998 na wengineo wengi tu ambao kwa msaada wa Tanzania waliweza kufanikisha Wapiganaji wa NRA waliokuwa wakiongozwa na Mzee Museveni kuiteka Uganda na kuwa Watawala mpaka leo japo kuna waliotangulia mbele za haki huku wengine wakitofautiana Kisiasa na Mzee Museveni.

Leo nataka tu niwapashe Wakenya kuwa walikuwa wanapoteza tu muda kufanya USHAWISHI wao kwa Mzee Museveni Rais wa Uganda kwani kwa aina ya Marafiki wa KUFA na KUZIKANA hawa Wafuatao wa Rais Museveni asingeitosa Tanzania yetu hata iweje. Nitawagawa hawa Marafiki wa karibu wa Museveni kwa makundi ili Wakenya mfahamu kuwa mlikuwa ( Wakwere wanasema ) KUZOZA mnapiga tu soga na kupoteza muda wenu.

MARAFIKI WA KARIBU wa Rais Museveni wa KUFA na KUZIKANA ni:
Hayati Baba wa Taifa Nyerere na sasa Familia yake nzima.
Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu na Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Mwalimu Nyerere Mzee Joseph Butiku.
Balozi Mstaafu na aliyekuwa Mshauri wa Masuala ya Nje na NYETI Mzee Adam Marwa.
Hayati Brigadier Hashim Mbita.
Mkurugenzi Mtendaji wa MKUKI Publishers Mzee Walter Bgoya.
Aliyekuwa Mbunge wa Karatu Hayati Mzee Patrick Qorro.
Mkuu wa Majeshi Mstaafu Mzee David Bugozi Musuguri.

MARAFIKI WA KUHESHIMIANA wa Rais Museveni ni :
Rais Mstaafu wa awamu ya pili Mzee Ally Hassan Mwinyi.
Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Mzee Benjamin William Mkapa.
Rais Mstaafu wa awamu ya nne Mzee Jakaya Mrisho Kikwete.
Waziri Mkuu Mstaafu Mzee Joseph Sinde Warioba.
Balozi Mstaafu wa Tanzania nchini Uganda Mzee Tambwe.
Naibu Balozi Mstaafu wa Tanzania nchini Uganda Hayati Mzee Mufungo Mujaya.

MARAFIKI wa KUHESHIMIANA KIUTENDAJI wa Rais Museveni ni :
Jeshi la Wananchi wa Tanzania ( JWTZ )

MARAFIKI wa KIUPENDO kwa UKARIMU kwa Rais Museveni ni :
Wananchi wote wa Tanzania hasa hasa Wakazi wa Dar es salaam, Kilimanjaro na Kagera.
NB: Japo nimewataja Watu kadhaa hapo kwa umuhimu wao ila hakuna Watu ambao hadi dakika hii Rais wa Uganda Mzee Yoweri Kaguta Museveni anawasikiliza na kila mara kuomba ushauri kwao kama Mjane wa Baba wa Taifa Mama Maria Nyerere na Mwanae Madaraka, Katibu Mkuu Kiongozi Mzee Joseph Butiku na Balozi Mstaafu Mzee Adam Marwa na nakumbuka ili kuonyesha kuwa Museveni ANAWAHESHIMU na KUWAPENDA hawa Watu watatu niliowataja hapa takribani miaka mitano ( 5 ) iliyopita tu katika Sherehe za Uhuru wa Uganda Rais Museveni aliwavisha TUZO ZA JUU na za HESHIMA KWA NCHINI Uganda Rais Mstaafu Mzee Kikwete kwa niaba ya Tanzania, Mama Maria, Mzee Butiku na Mzee Marwa na nakumbuka akiwa anahutubia pale Viwanja vya Kololo jijini Kampala mbele ya Waganda huku Rais wetu Mstaafu wa awamu ya nne ( 4 ) Mzee Kikwete akishuhudia Rais Museveni alisema maneno haya kwa Waganda namnukuu " today I am very happy that We are celebrating our independence together with people whom I call the true Comrades of Uganda. May I take this opportunity to introduce to you my other Mum, brothers and good friends from Tanzania the country that have a great history with Uganda. This is His Excellency President of Tanzania Jakaya Kikwete and next to him is Mama Maria Nyerere the former first lady of Tanzania and Nyerere's widow then these two are not only my friends but they are now my relatives ( akawatania Waganda kwa kuwaambia...) so you Ugandans if you think once you chase me from here I will have no where to go you're just wasting your time because Tanzania is my second home. This is Mr. Joseph Butiku former chief secretary of Tanzania and this one is Mr. Adam Marwa retired ambassador and a former close aide to late President Nyerere. Please together lets give them a hand of applause and wish them well " mwisho wa kumnukuu Rais wa Uganda Mzee Museveni kisha akawapa hizo TUZO tena kwa KUWAVISHA kwa MADAHA yote na Rais Museveni akionekana ni mwenye FURAHA ILIYOTUKUKA.

Hata hivyo najua na nikiri pia kuwa zipo sababu nyingi na tena muhimu pengine hata nje ya hii au hizi ambazo pia zimewezeshesha Uganda kukubali kupitisha Bomba lake nchini Tanzania badala ya Kenya lakini ni ukweli usiopingika kuwa Rais wa Uganda Yoweri Museveni ana UPENDO WA DHATI na ULIOTUKUKA kwa Nchi ya Tanzania na ANATUHESHIMU pengine hata kuliko Waganda anaowaongoza. Sababu hizo KUU za kihistoria na kirafiki ndizo zimekuwa HUKUMU kwa nchi ya Kenya.

Poleni sana Wakenya ila msihofu FURSA bado zipo nyingi tu tutawashirikisheni na zingine pia ila acheni MAJUNGU na WIVU wenu kwetu Watanzania.

Akhsante Rais Yoweri Kaguta Museveni kwa kuwaonyesha Wakenya kuwa Tanzania ndiyo kila kitu kwako na kwa Waganda wote na usichoke kutupa fursa zingine.

Imeandikwa na GENTAMYCINE/Jamii Forums
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Article imetulia sana hii aisee

    ReplyDelete
  2. Eakenya wapee wapeee tena uwape antibiotics kali kabisa hiyo gentamycn naona kama haitoshi ongezea na sindano za xstapen hahahhahah...wakenya wamezidi dharau

    ReplyDelete

Top Post Ad