Sasa Wakuu wa Wilaya Mguu Pande, Mguu Sawa..Wakati Wowote Rais Magufuli Atafunguka....

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

UTEUZI unaotarajiwa kufanywa wakati wowote wiki hii wa wakuu wa wilaya kote nchini, unawaweka viongozi hao mguu pande, mguu sawa, kwa maana kuwa tayari kwa lolote linaloweza kutokea.

Tokea aapishwe kuwa rais wa awamu ya  tano Tanzania, Novemba 5, mwaka jana, Rais  Dk. John Pombe Magufuli amekuwa msiri katika uteuzi wake, kwani mara nyingi amekuwa akiibuka na watu wasiotarajiwa, kitu kinachowapa hofu viongozi waliopo madarakani hivi sasa, kwani hawana uhakika wa kurudi katika nafasi zao.

Wakati akizungumza na wazee wa jiji la Dar es Salaam wiki chache zilizopita, rais Magufuli alisema mojawapo ya sifa zitakazowarejesha viongozi katika nafasi za ukuu wa mikoa na wilaya, ni pamoja na ushiriki wao katika kumaliza au kushughulikia migogoro ya ardhi katika maeneo yao na kuondoa tatizo la madawati katika shule za msingi na sekondari za serikali.

Hadi mwaka 2012, Tanzania ilikuwa na jumla ya wilaya 127 ambazo hata hivyo, zinaweza kuongezeka au kupungua kutokana na uamuzi binafsi wa rais kwani anayo mamlaka ya kikatiba ya kufanya hivyo pale anapoona inafaa.

Kaimu Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu, Greyson Msigwa hakuweza kuzungumzia suala la uteuzi huo akidai kuwepo katika kikao na badala yake akataka atumiwe ujumbe mfupi wa maneno, ambao hata hivyo baada ya kutumiwa hakuweza kuujibu.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad