Jamal Malinzi anahofia pia Uwanja Wa Karume Kupigwa Mnada na (TRA)

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Hiyo inafuatia TRA kukamata magari matano ya TFF kutokana na deni la kodi Sh. Bilioni 1 Milioni 118 ambazo ni malimbikizo tangu mwaka 2010, wakati TFF ikiwa chini ya Rais Leodegar Tenga.

“Kwa kweli hali mbaya, na sitashangaa hata kesho Uwanja wa Karume nao ukipigwa mnada, kwa sababu magari waliyokamata thamani yake haifiki deni wanalodai,”amesema Malinzi alipo kuwa akiongea na waandishi.

Ofisa wa TRA, Richard Kayombo amesema wamekamata magari hayo ili kuwapa shinikizo TFF waweze kulipa madeni hayo.

Amesema deni hilo la Sh. Bilioni 1 na Milioni 118 ni malimbikizo ya kodi mbalimbali kuanzia mwaka 2010 hadi 2015, zikiwemo za VAT na mishahara ya wafanyakazi wake.

“Ikumbukwe awali tulikamata akaunti zao kwa sababu deni lilifikia Bilioni 1. 6 na baada ya kupunguza deni tukawaachia akaunti zao, lakini bado halijaisha na ndiyo sababu ya kukamata hayo magari matano,”amesema Kayombo.

Ofisa huyo wa TRA amesema magari yote yaliyokamatwa, likiwemo basi la wachezaji wa timu ya taifa, Taifa Stars yapo kwenye kampuni minada ya Yono.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad