Siwezi Kumuomba Msamaha Chidi Benz Kwa Kauli Yangu ‘Acha Afe’ – Dudu Baya

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Msanii mkongwe wa muziki, Dudu Baya, amesema hawezi muomba msamaha Chidi Benz kutokana na kauli yake ‘acha afe’ ambayo aliitoa baada ya rapa huyo kuzidiwa na matumizi ya Madawa ya kulevya na kuomba msaada.
Dudu Baya

Akizungumza na Bongo5 Jumatano hii, Dudu Baya amesema aliitoa kauli hiyo baada ya kuona rapa huyo hakuwa tayari kusaidiwa na watu ambao walijitokeza kumsaidia.

“Siwezi kumuomba msamaha Chidi Benz kwa kauli yangu ya acha afe,” alisema Dudu Baya “Nachoweza kufanya ni kumpa pole kwa matatizo yaliyompata, na ninamwombea dua Mungu ampe nguvu mpya, akili mpya, mwanga mpya. Bongofleva inamwitaji, jamii imemmis, familia yake inamwitaji na inamtegemea. My best rapper, my friend Chidi Benz hakuna wa kukuokoa, jiokoe,”

Chizi Benz kwa sasa anaendelea vizuri baada ya kukubali kupelekwa Bagamoyo Sober House kumsaidiwa kuondokana na matatizo yanayomkabili.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Wewe Dudu Baya unamsema mwenzako nilipokuona ukiongea kwenye video jinsi ulivyoonekana umechoka sababu ya pombe inatia huruma, na wewe jisaidie mwenyewe kutumia pombe kupita kiasi mpaka unawatukana wazazi wa watu kipindi uko bwi, heri ya Chidi Benz kaomba msaada sasa anayo nafuu, je wewe Dudu baya?

    ReplyDelete

Top Post Ad