Timu ya Yanga yatinga Rasmi Fainali Kombe la Shirikisho...Coastal Union Imepigwa Faini

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Uamuzi huo umefanywa na Kamati ya Mashindano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) iliyokutana leo (Aprili 27, 2016) jijini Dar es Salaam kwa kuzingatia Kanuni ya 28(2) ya Kombe la Shirikisho. Wakati mechi hiyo inavunjwa, Yanga ilikuwa ikiongoza kwa mabao 2-1.

Pia Coastal Union imepigwa faini ya sh. 2,000,000 (milioni mbili) kwa kuzingatia Kanuni ya 42(26) ya Ligi Kuu kutokana na vitendo vya vurugu za washabiki wake wakati wa mechi hiyo. Pia TFF haitasita kufungiwa uwanja huo iwapo vitendo hivyo vya vurugu za washabiki havitakoma.

Mwamuzi wa mchezo huo Abdallah Kambuzi amefungiwa mwaka mmoja wakati Mwamuzi Msaidizi namba mbili Charles Simon ameondolewa kwenye ratiba ya waamuzi. Adhabu hizo zimetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 38(1) ya Ligi Kuu.

Mchezaji Adeyum Ahmed wa Coastal Union anapelekwa Kamati ya Nidhamu ya TFF kwa ajili ya hatua zaidi kutokana na kitendo chake cha kumpiga kichwa Mwamuzi wa Akiba baada ya kutolewa nje. Hata hivyo, Ahmed hakufanikiwa kutimiza azma hiyo baada ya Mwamuzi huyo kumkwepa.
Yanga imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kwa mujibu wa Kanuni ya 14(13) ya Ligi Kuu kutokana na kutoingia vyumbani kwenye mechi hiyo ya Kombe la Shirikisho.

Vilevile malalamiko ya Coastal Union kutaka mechi hiyo irudiwe yametupwa baada ya Kamati ya Mashindano kubaini kuwa hayana msingi wowote.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Bora mweeh,Sasa coastal ya sasa ni ya kutuwakilisha kimataifa kweli?Bora hata wangeshinda MWADUI kama lengo ni kubadilisha na kwamba wasiwe au wasizoeleke walewale kila mwaka.Coastal union
    nidhamu sifuri,kuanzia wachezaji mpaka mashabiki wao,ushirikina na mbinu za wale waarabu wa...........ndio wanatumia na wenyewe kiasi wageni hawataki hata kuingia vyumbani wakiwa dimbani kwao.SAFI NDIO MJIFUNZE.

    ReplyDelete
  2. YANGA (wakimataifa) hoyeeeeeeeeee!!!!! wamchangani mtabaki kutoa kauli za kushindwa kila siku, TUMEBEBWA!

    ReplyDelete
  3. TUWAACHE WAKIMATAIFA WAKUTANE,COASTAL NA AZAM WAPI NA WAPI.

    ReplyDelete
  4. TFF ni yanga, sasa mlitegemea nini

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nafasi zinaombwa,sasa si na wewe simba uombe.

      Delete

Top Post Ad