Wanaume Wanne Wambaka Binti Mdogo Kwa Zamu na Kumuharibu Vibaya Sehemu za Siri.....

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

JESHI la Polisi katika Kanda Maalumu ya Tarime/Rorya mkoani Mara, linawasaka watuhumiwa watano wanaotajwa kuhusika kubaka wasichana wawili katika eneo hilo.

Kamanda wa Polisi wa kanda hiyo, Andrew Satta alisema, watu hao wanatuhumiwa kuwabaka wasichana hao katika matukio mawili tofauti yaliyotendwa kwa nyakati tofauti Machi 26, mwaka huu katika wilaya za Rorya na Tarime.

Satta alisema kuwa, katika tukio la kwanza mwanafunzi wa shule ya msingi Kibasisi iliyopo kwenye kijiji cha Kangariani wilayani Tarime (Jina limehifadhiwa), alibakwa na watu wawili wakati akirejea nyumbani kutoka shuleni siku hiyo ya Machi 26.

Kamanda Satta alisema kuwa, mwanafunzi huyo alikutana njiani na watu wawili waliokuwa wamejifunga vitambaa vyeusi usoni, ambao walimkamata kwa nguvu, kumburuza vichakani na kumbaka kwa zamu. Alieleza zaidi kuwa, baada ya kumbaka, watu hao walimdhibiti asipige kelele kwa kumfunga kitambaa mdomoni.

“Walipomaliza kumbaka walitokomea kwenye vichaka na kutorokea mahali pasipojulikana, lakini Polisi inawasaka,” alisema na kuongeza kuwa, tukio hilo liliripotiwa Polisi na mwanafunzi huyo.

Katika tukio la pili, Kamanda Satta alisema kuwa, siku hiyo usiku kwenye kijiji cha Ruhu kwenye mwalo wa wavuvi wilayani Rorya, msichana mwenye umri wa miaka 21 (Jina limehifadhiwa), alidanganywa na vijana wanne kuwa aliitwa na rafiki yake wa kiume, jambo lililomfanya awaombe wamsindikize alipo na walitii.

Kamanda Satta alisema kuwa, bila kujua nia ya vijana hao kumdanganya hivyo, binti huyo ambaye hata hivyo anawatambua na kufahamu majina yao, alikubali na kuondoka nao. 

Alisema kuwa baada ya kufika kwenye eneo la mwalo wa wavuvi, karibu na vichaka, huku kukiwa na giza nene, waliamua kumkamata kwa nguvu na kumfunga mdomo kwa kitambaa asiweze kupiga kelele.

“Walipofanikiwa kudhibiti asipige kelele vijana hao wanne walimbaka kwa zamu na kumwacha akiwa hoi vichakani, ndipo binti huyo alipoamua kujikongoja hadi kwenye eneo alipopata msaada wa wasamaria waliomsindikiza kutoa taarifa kwenye kituo cha Polisi na kwenda hospitali kwa matibabu”, alisema.

Watu hao waliotajwa na binti huyo kuwa ndio waliombaka ni pamoja na Ophia Robert ambaye amekamatwa, Nchama Bureki, Robert Shija na mwingine aliyetajwa kwa jina moja, Mashije. 

Aliwaonya wanaoendeleza ubakaji katika kanda hiyo kuacha kwa sababu msako unaofanywa ni endelevu na jeshi hilo halitasita kuwachukulia hatua za kisheria.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. WAPEWE ADHABU KALI SANA. CHUKULIA KAMA MTOTO WAKO NDIO KAFANYIWA HIVYO

    ReplyDelete
  2. mie naona watu wa mara wamelaaniwa maana mabaya yote yako kwao hao watu wa huko hawana dini ya kiislam wa ukiristo hawajui kanisa wala msikiti mungu atawachoma natamani tuwatenge wasiwe watanzania

    ReplyDelete
    Replies
    1. Usiwatenge. Bali wanaitaji msaada hata wa kiimani kama ulivyosema hapo ili wawe binadam wazuri. Ila kwa kitendo hicho wanaelewa nini? Wanachokifanya kama si vizuri ni mabaya kwa hiyo wapewe adhabu kali kwani ni watu wabaya. Ili iwe fundisho katika jamii

      Delete

Top Post Ad