Kibao Chamgeukia NAPE Nhauye Bungeni...Awekwa Kikaangoni na Wabunge..Aitwa Waziri Mzigo

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Wabunge wamemcharukia Waziri wa Habari, Nape Nnauye kwamba aliwahi kuwaita mawaziri wa Serikali iliyopita mizigo, lakini yeye amezuia matangazo ya moja kwa moja ya Bunge, ili wananchi washindwe kumpima kama ni mzigo au lumbesa.

Hayo yalijitokeza jana wakati wabunge walipochangia hotuba ya bajeti ya Wizara ya Habari kwa mwaka 2016/2017, iliyowasilishwa bungeni na Waziri Nape.

Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara (Chadema) alieleza kushangazwa na hatua ya Serikali ya Awamu ya Tano kuhimiza wananchi kudai risiti wanaponunua bidhaa, lakini haitaki wananchi waone inavyopanga matumizi yake.

Alisema Nape akiwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, aliwaita baadhi ya mawaziri ni mizigo, lakini amepewa wizara hiyo amezuia mijadala ya wazi ambayo ingesaidia wananchi kumpima.

“Nilipoona amepewa wizara ya habari nikajua ataruhusu mijadala ya wazi ili tumuone yeye kuwa hatakuwa mzigo, lakini yeye akawa lumbesa. Hilo amelizuia kwa hiyo tunashindwa kumpima,” alisema.

Alisema waziri huyo hawezi kukwepa lawama ya hicho kinachoendelea cha kuzuia matangazo ya Bunge, kwa vile wanaopiga picha na kuhariri taarifa zinazorushwa ni watumishi wa TBC.

Udhibiti wa Bunge
Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe (Act-Wazalendo), alisema kuwa wabunge wote waliopinga Bunge kutoonyeshwa ‘live’ na kusababisha mtafaruku bungeni, wameitwa kuhojiwa na Kamati ya Maadili ya Bunge.

“Wabunge hapa tulisimama tukapinga na wapo waliounga mkono, lakini kiti chako kimetuita wabunge wote tuliopinga kauli ya Serikali kwenye kamati ya maadili. Jana mimi nimepata barua,” alisema Zitto.

“Kwamba mnatubana kusema. Mnazuia Bunge lisionekane. Hata kutoa maoni ndani ya Bunge tunakwenda kuhojiwa? TBC ni chombo cha umma, siyo chombo cha Serikali, inaendeshwa kwa kodi za wananchi,” alisisitiza.

Baada ya mchango huo, Naibu Spika, Dk Tulia Ackson alisema si kweli wabunge hao wanahojiwa kutokana na michango yao, bali wanahojiwa kutokana na mambo waliyoyafanya kwa kutotii maagizo ya kiti wakati wa mjadala wa ‘Bunge Live’.

Kwa upande wake, Mbunge wa Chemba, Juma Nkamia (CCM), aliunga mkono hoja ya Zitto ya kuifanya TBC iendeshwe kama inavyoendeshwa BBC kwa kupewa  leseni maalumu.

Pia, aliitaka Serikali kupeleka muswada bungeni utakaowabana wamiliki wa vyombo vya habari kuwa na mikataba na waandishi wanaowaandikia, pia, akadai baadhi ya vyombo haviwalipi waandishi wake.

Hata hivyo Mbunge wa Viti Maalumu, Agness Marwa (CCM) alitetea uamuzi wa Serikali kuondoa matangazo ya moja kwa moja ya Bunge, akisema wabunge wanaodai hilo ni wale waliokuwa wakiuza sura.

Katika hatua nyingine, Waitara alisema kitendo cha Nape kuwaalika wabunge kwenye muziki, baada ya bajeti yake kupita ilikuwa ni kuwahonga.

Juzi jioni wakati akitoa matangazo kabla ya kuahirisha Bunge, Naibu Spika alisema baada ya kupitisha bajeti ya Wizara ya Habari, wanamuziki Diamond Plutnum na King Kiki watatumbuiza katika viwanja vya Bunge.

“Mnaposema mnabana matumizi hao wanamuziki wameletwa kwa gharama za nani,” alihoji mbunge huyo.

 “Wabunge wote ambao wataenda katika hiyo miziki ili kuunga mkono habari ya Nape mtakuwa mmekula rushwa,” alisisitiza Waitara, kauli ambayo ilimfanya Naibu Spika, Dk Tulia kufafanua, akisema suala hilo lilitangazwa bungeni kama mengine, lisiingizwe kosa la jina la rushwa.

Upinzani na udikteta
Msemaji mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni katika Wizara ya Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, Joseph Mbilinyi, alisema kitendo cha Serikali kuminya uhuru wa habari ni kuelekea kwenye udikteta.

 “Kana kwamba haitoshi, Serikali sasa imezuia Televisheni ya Umma, inayoendeshwa na kodi ya wananchi (TBC1) kurusha matangazo ya moja kwa moja ya mijadala inayofanyika bungeni. Dalili hizi siyo njema kwa ukuaji wa demokrasia na uhuru wa habari hapa nchini na zinatoa taswira ya utawala wa ki-dikteta,” alisisitiza.

“Tunaitaka Serikali kuliomba radhi Bunge hili, kwa kosa la kuminya uhuru wa habari kinyume na Katiba na kuviacha vyombo vya habari hususan vya umma kufanya kazi zao za kuhabarisha umma kwa uhuru,” alisema.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Saa nyingine vi vigumu mtu kujitambua ni Mtanzania ki vipi. Hivi hawa wapuuzi wa Upinzani na hiyo issue ya BUNGE LIVE mbona wameishikilia sana kwani hawana ajenda yoyote ni TV tu. Ni vile tu haiwezekani ila Udikteta ni mzuri kwani uliweza kuuficha ujinga wetu kwa kuwaruhusu watu timamu tu kupata nafasi ya kusikilizwa sasa hii Demokrasia na Uhuru ambao Tanzania imeupata hivi majuzi tu ni taabu
    Ombi langu kwenu udaku baneni nafasi kwa hao wanaodai kuonekana LIVE muwashauri wakaombe kazi Star TV, Clouds EATV na kwingineko kwani labda wame-qualify huko chonde,chonde, chonde Udaku tunapenda kusoma blog zenu lakini mweeee!!!!! ni LIVE, LIVE, LIVE BUNGE hata hatulali mimi naishi kijiji cha Ujamaa MBATAMILA Tunduru na TV hatuijui na ni wengi tusio na TV Tanzania karibu 85% au zaidi ya raia wote au zaidi bunge live kama ajenda yao ya msingi siyo kazi tuliwachagulia wakatuwakilishe huko Dodoma hapana,,,bunge live redioni kwetu dili

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ulipewa kofia shati na suruali ya chama tawala bure walisahau kukupa sabuni ya kufulia hivyo unaendeleza kiherehere chako ili ufanikiwe kupata sabuni imekula kwako hata ujikombe vipi si leo labda chaguzi zijazo.

      Delete
  2. Swala la serikari kusitisha kuoshesha matangazo ya binge kwa kisingizio chakubana matumizi halina mashiko kwa sababu ikumbukwe bunge sio la serikali bali la wanainchi, utandaji wa wabunge haupimwi kwa yale yanayoletwa jimboni kila nw jinsi anavyotetea taiga, kurusha binge Ni njia moja ya kukuza demokrasia nchini lakini sasa nimeiamini kauli ya waziri wa habari kuwa raisi JPM ataudhoufisha upizani, sasa yametimia,
    Serikali ijiamini inafanya mambo mazuri sana lakini itajiaribia isipokuwa makini

    ReplyDelete

Top Post Ad