Milioni 392 Zajenga Barabara HEWA Dar es Salaam

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Boniface Jacob amebaini matumizi ya Sh392 milioni zilizoandikwa kwenye taarifa ya manispaa hiyo kuwa zimetumika kwa ajili ya ukarabati wa barabara ya Sinza - Igesa ambao haukufanyika.

Katika taarifa ya manispaa hiyo, fedha hizo zilidaiwa kutumika kwa ajili ya matengenezo ya mara kwa mara ya barabara hiyo.

Akizungumza kwenye ziara ya Kamati ya Uchumi na Fedha ya Manispaa hiyo, Jacob alisema ni ajabu kuona hakuna matengenezo yoyote yaliyofanyika kama taarifa hiyo inavyoelezwa huku fedha zikionekana kulipwa.

Alisema hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa yeyote atakayebainika kuhusika kwenye matumizi hayo huku akiiomba Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru) kuchunguza matumizi ya fedha hizo.

“Fedha hizi zinaonekana zimelipwa kwa mkandarasi Skol Building Contract Ltd wakati barabara ina mahandaki na mashimo makubwa, ikionyesha kwamba haijakarabatiwa,” alisema.

Alisema kama wasingeamua kukagua thamani ya fedha za halmashauri hiyo zinavyotumika kwenye miradi hiyo katika kipindi cha Jaruari hadi Machi mwaka huu wasingegundua udanganyifu huo.

Meya huyo aliyeonyesha kukasirishwa na hali hiyo, aliwataka wataalamu wa halmashauri hiyo waliohusika kuandika ripoti hiyo kutoa maelezo ya kina kuhusu udanganyifu huo.

“Hivi kama tungenyamaza tusiamue kukagua miradi hii nani angesimama kueleza hayo? Mnaleta hadithi wakati tayari mmeshalidanganya Baraza la Madiwani kwamba fedha hizi zimetumika kukarabati barabara hii?” alisema.

Akitetea matumizi ya fedha hizo, mchumi wa manispaa hiyo, Huruma Eugen alisema zilizoandikwa kwenye taarifa hiyo zimetumika kwa ajili ya kulipa madeni ya nyuma.

Huku kukiwa na mabishano baina yake na Meya, Eugen alisema awali, ujenzi wa barabara hiyo ulifanyika kwa kukopa kutoka fedha za Mfuko wa Barabara, jambo lililowafanya watumie fedha za mapato ya ndani ya halmshauri kulipa deni hilo.

“Hela ilitoka kwenye mfuko wa barabara na imerudishwa kwenye akaunti, japo huku imeandikwa imelipwa kwa mkandarasi aliyejenga barabara hii,” alisema Eugen.

Hata hivyo, Meya huyo alisema kama fedha hizo zimetumika kwa ajili ya kulipa madeni zingeonyesha wazi kwenye taarifa hiyo badala ya kuandikwa kwamba zimeelekezwa kwenye ukarabati wa barabara, wakati jambo hilo halijafanyika.

Diwani wa Sinza, Godfrey Chindaweli alieleza kushangazwa na taarifa inayoonyesha ukarabati wa barabara hiyo wakati ni miongoni mwa barabara zenye mashimo kwenye kata yake.

Alisema mara kadhaa amepokea malalamiko kutoka kwa wananchi kuhusu ubovu wa barabara hiyo na kuahidi kuikarabati akidhani ipo kwenye mpango.

“Nimeshangaa kuona miongoni mwa miradi iliyotumia fedha za robo ya tatu ya mwaka huu wa fedha, barabara ya Sinza ambayo haijaguswa ipo kwenye orodha, jambo hili linahitaji majibu ya haraka,” alisisitiza.

Diwani wa Makongo, Ndeshukuru Tungaraza aliwataka wataalamu wa halmashauri hiyo kueleza ilikuwaje fedha ziandikwe kwamba zimetumika kwa ajili ya ukarabati wa barabara wakati hazikutumika kwa kazi hiyo.

Tungaraza alisema hakuna sheria ya matumizi ya fedha inayoelekezwa kufanya kama ambavyo manispaa hiyo imefanya, jambo ambalo madiwani hawatakubaliana nalo.

Katika eneo la Mwananyamala kwenye Barabara ya Akachube inayoelekea kwenye kituo cha daladala cha Makumbusho, Meya huyo aliwaagiza wahandisi aliowakuta wakiendelea na ujenzi kukamilisha haraka ili kuondoa usumbufu kwa watumiaji wa barabara hiyo.

Alisema malalamiko mengi ya wananchi kuhusu ubovu wa barabara yanatokana na uzembe wa kutosimamia kwa ukamilifu miradi iliyopo.

Hata hivyo, mkandarasi wa kampuni ya Delmonto, Rajab Athman alisema wanashindwa kukamilisha kwa wakati barabara hiyo kutokana na kupasuka kwa mabomba ya maji.

“Maji yanamwagika mengi, hivyo tunawasubiri Dawasco wakishakamilisha kutengeneza mabomba yaliyopasuka tutaendelea kujenga,” alisema.

Katika ujenzi wa Jengo la Bima ya Afya, katika Hospitali ya Mwananyamala linaloendelea kujengwa, Meya Jacob alionyesha wasiwasi wa jengo hilo kukamilika mapema kabla mpango wa matumizi ya bima kwa wananchi wote kuanza.

“Mpango huu unatarajia kuanza Julai lakini mpaka sasa hali inaonyesha halitakamilika kwa wakati, jambo hili linanipa wasiwasi,” alisema.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

7 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. HONGERA MEYA.. hII NDIYO KASI TUNAYOITAKA SIYO KUKAA OFISINI NA KUSUBIRI TAARIFA.. UNATOKA UNAKWENDA UNAKAGUA UNA REKEBISHA PANAPO HITAJI KUREKEBISHWA NA UKUVUMBUA MADUSU UNATUMBUA TENA HARAKA SANA .. UAMUNIFU / UWAJIBIKAJI/ UCHAPA KAZI VIKIKOSEKANA NA IKITHIBITIKA HIVYO WALA HUMGOJI MTUKUFU RAISI ATUMBUE UNATUMBUA WEWE MWENYEWE KUSAIDIA BABA JPJM.. HAPO TUTAENDELEA VIZURI ..HONGERA KUNGUZA KWA KINA NA IKIBAINIKA KWANZA WARUDISHE PESA HIZO HALA MKONDO WA SHERIA UCHUKUE NAFASI YAKE... HIVI NDIVYO TUTAKAVYO.. KILA MTU AWAJIBIKE KATIKA NAFASI YA KIUTENDAJI ALIPO.... BABA JPJM TUKO BEGA KWA BEGA KUMTUMIKIA MTANZANIA WITH POSITIVITY AND INNOVATIONS..

    ReplyDelete
    Replies
    1. MDAU AMINI USIAMINI TANZANIA TULIKUWA NA OXIJENI NYINGI SANA NDIYO MAANA TUKAWEZA KUWA NA WAFANYAKAZI HEWA / MIKATABA HEWA / SASA PIA UKARABATI HEWA NA VIONGOZI WALIOPITA TUTAWAITAJE?? NA SASA MGUNG KAJAALIA AMEKUJA KASSIMU NA MAGU WANAANZA KUIBANA HEWA .. WATU WA NCHI YA HEWA SI WATAKUFA KWA KUISOSA NINI VILE ILE YA KUVUTA KWA MAPAFU..... HEWAAAAAAAAAAAAAAA!!!!!!!!!! MUNGU AKULINDENI WABANA HEWA TUWAONE WATAKAO PATA SHIDA KWA KUKOSA HEWAAAAAAAAAAAA.. INATISHAAAAAAAA.... BABA JPJM BADA HEWA NA MH K.MAJALIWA TUNAONE WANA HEWA WATURUDISHIE HIYO OXIJENI ...

      Delete
    2. MDAU AMINI USIAMINI TANZANIA TULIKUWA NA OXIJENI NYINGI SANA NDIYO MAANA TUKAWEZA KUWA NA WAFANYAKAZI HEWA / MIKATABA HEWA / SASA PIA UKARABATI HEWA NA VIONGOZI WALIOPITA TUTAWAITAJE?? NA SASA MGUNG KAJAALIA AMEKUJA KASSIMU NA MAGU WANAANZA KUIBANA HEWA .. WATU WA NCHI YA HEWA SI WATAKUFA KWA KUISOSA NINI VILE ILE YA KUVUTA KWA MAPAFU..... HEWAAAAAAAAAAAAAAA!!!!!!!!!! MUNGU AKULINDENI WABANA HEWA TUWAONE WATAKAO PATA SHIDA KWA KUKOSA HEWAAAAAAAAAAAA.. INATISHAAAAAAAA.... BABA JPJM BADA HEWA NA MH K.MAJALIWA TUNAONE WANA HEWA WATURUDISHIE HIYO OXIJENI ...

      Delete
    3. MDAU AMINI USIAMINI TANZANIA TULIKUWA NA OXIJENI NYINGI SANA NDIYO MAANA TUKAWEZA KUWA NA WAFANYAKAZI HEWA / MIKATABA HEWA / SASA PIA UKARABATI HEWA NA VIONGOZI WALIOPITA TUTAWAITAJE?? NA SASA MUNGU KAJAALIA AMEKUJA KASSIMU NA MAGU WANAANZA KUIBANA HEWA .. WATU WA NCHI YA HEWA SI WATAKUFA KWA KUISOSA NINI VILE ILE YA KUVUTA KWA MAPAFU..... HEWAAAAAAAAAAAAAAA!!!!!!!!!! MUNGU AKULINDENI WABANA HEWA TUWAONE WATAKAO PATA SHIDA KWA KUKOSA HEWAAAAAAAAAAAA.. INATISHAAAAAAAA.... BABA JPJM BANA HEWA NA MH K.MAJALIWA TUNAONE WANA HEWA WAKOSE HEWA WATURUDISHIE HIYO OXIJENI ...ILI TUWEZE KUAPA HEWA INAYOSTAHIKI..KWA BINADAMU WAPENDA HEWA...iNASIKITISHA TENA SANA.. LEO MTOTO AKOSE DAWATI NA DAWA HOSPITALI NA MAJI SAFI YA KUNYA KUEPUSHA TAIFODI NA KIPINDUPINDU AJILI YA WATU WAPENDA HEWA KATIKA NCHI YA HEWA.. NDUGU ZANGU HAMUONI HURUMA KWA HIVI VIZAZI YA NCHI HEWA.. KUWENI WAAMIFU NA WAADOLIFU... HEWA KILA UNAPOKWENDA INASIKITISHA LAKINI AMINI KWAMBA KATIKA HII AWAMU YETU YA TANO. TUTAIMULIKA HEWA NA TUTAIBANA IPASAVYO NA KUIKOMESHA KWA KIASI KIKUBWA. CHINI YA TIMU KABAMBE YA JPJM N A MH K.MAJALIWA

      Delete
    4. MDAU AMINI USIAMINI TANZANIA TULIKUWA NA OXIJENI NYINGI SANA NDIYO MAANA TUKAWEZA KUWA NA WAFANYAKAZI HEWA / MIKATABA HEWA / SASA PIA UKARABATI HEWA NA VIONGOZI WALIOPITA TUTAWAITAJE?? NA SASA MUNGU KAJAALIA AMEKUJA KASSIMU NA MAGU WANAANZA KUIBANA HEWA .. WATU WA NCHI YA HEWA SI WATAKUFA KWA KUISOSA NINI VILE ILE YA KUVUTA KWA MAPAFU..... HEWAAAAAAAAAAAAAAA!!!!!!!!!! MUNGU AKULINDENI WABANA HEWA TUWAONE WATAKAO PATA SHIDA KWA KUKOSA HEWAAAAAAAAAAAA.. INATISHAAAAAAAA.... BABA JPJM BANA HEWA NA MH K.MAJALIWA TUNAONE WANA HEWA WAKOSE HEWA WATURUDISHIE HIYO OXIJENI ...ILI TUWEZE KUAPA HEWA INAYOSTAHIKI..KWA BINADAMU WAPENDA HEWA...iNASIKITISHA TENA SANA.. LEO MTOTO AKOSE DAWATI NA DAWA HOSPITALI NA MAJI SAFI YA KUNYA KUEPUSHA TAIFODI NA KIPINDUPINDU AJILI YA WATU WAPENDA HEWA KATIKA NCHI YA HEWA.. NDUGU ZANGU HAMUONI HURUMA KWA HIVI VIZAZI YA NCHI HEWA.. KUWENI WAAMIFU NA WAADOLIFU... HEWA KILA UNAPOKWENDA INASIKITISHA LAKINI AMINI KWAMBA KATIKA HII AWAMU YETU YA TANO. TUTAIMULIKA HEWA NA TUTAIBANA IPASAVYO NA KUIKOMESHA KWA KIASI KIKUBWA. CHINI YA TIMU KABAMBE YA JPJM N A MH K.MAJALIWA

      Delete
  2. MDAU AMINI USIAMINI TANZANIA TULIKUWA NA OXIJENI NYINGI SANA NDIYO MAANA TUKAWEZA KUWA NA WAFANYAKAZI HEWA / MIKATABA HEWA / SASA PIA UKARABATI HEWA NA VIONGOZI WALIOPITA TUTAWAITAJE?? NA SASA MUNGU KAJAALIA AMEKUJA KASSIMU NA MAGU WANAANZA KUIBANA HEWA .. WATU WA NCHI YA HEWA SI WATAKUFA KWA KUISOSA NINI VILE ILE YA KUVUTA KWA MAPAFU..... HEWAAAAAAAAAAAAAAA!!!!!!!!!! MUNGU AKULINDENI WABANA HEWA TUWAONE WATAKAO PATA SHIDA KWA KUKOSA HEWAAAAAAAAAAAA.. INATISHAAAAAAAA.... BABA JPJM BANA HEWA NA MH K.MAJALIWA TUNAONE WANA HEWA WAKOSE HEWA WATURUDISHIE HIYO OXIJENI ...ILI TUWEZE KUAPA HEWA INAYOSTAHIKI..KWA BINADAMU WAPENDA HEWA...iNASIKITISHA TENA SANA.. LEO MTOTO AKOSE DAWATI NA DAWA HOSPITALI NA MAJI SAFI YA KUNYA KUEPUSHA TAIFODI NA KIPINDUPINDU AJILI YA WATU WAPENDA HEWA KATIKA NCHI YA HEWA.. NDUGU ZANGU HAMUONI HURUMA KWA HIVI VIZAZI YA NCHI HEWA.. KUWENI WAAMIFU NA WAADOLIFU... HEWA KILA UNAPOKWENDA INASIKITISHA LAKINI AMINI KWAMBA KATIKA HII AWAMU YETU YA TANO. TUTAIMULIKA HEWA NA TUTAIBANA IPASAVYO NA KUIKOMESHA KWA KIASI KIKUBWA. CHINI YA TIMU KABAMBE YA JPJM N A MH K.MAJALIWA

    ReplyDelete
  3. Mdau, kukujubu swali lako Tutawaita Ni viongozi WA kutabiri HEWA KATIKA NCHI YA HEWA WAKATI WA MACHAFUKO YA HEWA KWA MIIUNDO MBINO YA KIHEWA...UPO MWAYA...BARIDA

    ReplyDelete

Top Post Ad