Mwita Waitara Azusha Tafrani Bungeni.......Ni Baada ya Kutaka Kumchapa Ngumi Mbunge wa Kasulu Aliyedai Tundu Lissu na Mnyika Ni Vichaa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mbunge  wa Ukonga, Mwita Waitara (Chadema) ametolewa nje ya Bunge baada ya kutaka kumkwida Mbunge wa Kasulu Vijijini, Agustine Holle (CCM) aliyedai kuwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu na Mbunge wa Kibamba, John Mnyika wote wa Chadema kuwa wanaugua kichaa.

Waitara alionesha kukerwa na kauli hiyo hasa pale Holle alipokataa kufuta kauli yake, licha ya kutakiwa kufanya hivyo na Naibu Spika, Dk Tulia Akson.

Wakati Holle akichangia, Waitara alinyanyuka kwenye kiti chake na alipofika alipo mbunge huyo alimzungumzisha maneno ambayo hayakusikika na kuonesha kama kutaka kumpiga kabla ya kukaa kwenye kiti kilicho mbele yake ndipo, Holle alisikika akisema “wewe unataka nini” ndipo Naibu Spika alipogundua kuwa Waitara anataka kumpiga Holle na kumuamuru atoke nje lakini hakutii amri hiyo.

Kutokana na kutotii, Naibu Spika aliamuru askari wamtoe ndipo walipoingia zaidi ya askari watano na kutoka naye hadi nje ya geti kubwa la kuingilia bungeni.

Holle wakati anachangia bajeti ya Wizara ya Katiba na Sheria kwa mwaka wa fedha 2016/2017, alimtaja Lissu ambaye ni Waziri Kivuli wa Wizara hiyo kuwa ana taarifa kuwa Lissu amewahi kuugua ugonjwa wa kichaa na hadi sasa ana faili kwenye Hospitali ya Vichaa ya Mirembe iliyopo mkoani Dodoma.

Hata hivyo, alipopewa nafasi na Naibu Spika kufuta kauli yake akasema “nafuta kauli yangu lakini kwa taarifa zilizozagaa nimeamini ni kweli na mbona kwao(Chadema) wapo wengi hata Mnyika sasa hivi yupo Muhimbili anatibiwa kichaa”.

Kutokana na kauli hiyo, Lissu alisema licha ya kuifahamu Hospitali ya Mirembe, hajawahi hata kuingia kwenye geti la hospitali hiyo wala kuugua ugonjwa huo na kutaka kiti cha Naibu Spika kimtake Holle athibitishe ; na akishindwa kanuni zielekeze hatua za kuchukua kama zilivyowekwa.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Vituko vya waheshimiwa bwanaaa hahahahahaha

    ReplyDelete
  2. Ndio maana wanataka bunge lionyeshwe live ili tuonae ubavu wao wa kurusha makonde

    ReplyDelete
  3. Duh! Kama ni hivyo, basi hata huyo Waitara nayeye ni kichaa......kaaaaazi kwelikweli

    ReplyDelete
  4. Ndugu wananchi Na. Serrikali yetu ya awamu hii ya Tano..Questionnaire kwa hawa. Tuliowapa heshima Na kuwaamini Na baadae kuwaita Waheshimiwa je tunyamaze kwa Wao kuto Jiheshimu..manake wanavunja Heshima Na Maadili ya Bunge letu..it should be made Mandatory ...mbwa bwajikaji simu zote Ni mvivu. .na hawa hawana hadhi Na vigezo vya kuwa ndani ya Hilo Bunge Ni vizuri tuwatathmini pia..ni lazima wajaze hizi questionnaire Na mahudhurio pia Na hakuna kurusha Bunge laivu kuwaoneaha watovu WA Nidhamu..pls kata posho kwa kila anaekosa kuhudhuria pesa zetu za kodi zinauma Mzee NDUNGAI NA IKIBIDI WSCALATE HAPO HAPO TUPATE UFUMBUZI WA POSHO...DODOMA NI PAZURI LAKINI SIYO VACATION DESTINATION IT'S ACHIEVEMENT AND PERFORMANCE OBSERVATION..FOR THE COUNTRY PROGRESS..WAJOBIKA MBUNGGE..HUWEZI ACHIA KAMBA..URUDI ULIKOTOKA

    ReplyDelete
  5. Yanazzuka mengine ya madawa ya kulevya na Bange..hiyo Ni baada ya vichaa...Inaendelea kutusikitisha na kutuvunja moyo...Safari italuwa yakukongoja...kufika tutafika lakini muda unaonesha utakuwa mreffu so kama tunabyotarajia..JPJM HAPA KAZI IPO NA NI KUBWA..

    ReplyDelete

Top Post Ad