Mchezaji wa Azam Farid Mussa Afaulu Majaribio Nchini Hispania....

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

WINGA wa kimataifa wa Tanzania, Farid Mussa Malik (pichani kulia) wa klabu ya Azam ya Dar es Salaam amefaulu majaribio katika klabu ya Deportivo Tenerife ya Ligi Daraja la Kwanza nchini Hispania.
Mkurugenzi wa Azam FC, Yussuf Bakhresa anayefuatilia majaribio ya mchezaji huyo Hispania, amesema kwamba CD Tenerife sasa inatarajiwa kuingia katika mazungumzo na Azam FC juu ya kumnunua mchezaji huyo.

“Tunatarajia kuanza mazungumzo nao juu ya suala la Farid, ingawa wazo lao la awali ni kumchukua kwa mkopo wa miaka miwili. Sasa tunasubiri ofa yao rasmi, kisha Bodi ya Ukurugenzi itajadili na kutoa maamuzi,”amesema Bakhresa.

Kwa upande wake, Farid amefurahia matokeo hayo na kusema haikuwa kazi nyepesi kwake kuweza kuwaridhisha maofisa wa benchi la ufundi la Tenerife.

“Kwa kweli nimefurahi sana na ninamshukuru Mungu kwa kufuzu majaribio, ila haikuwa kazi nyepesi, mpira wa Ulaya mgumu,”amesema.

Awali, Farid ilikuwa apelekwe moja ya klabu za Ligi Kuu ya Hispania, maarufu kama La Liga, kati ya Las Palmas na Athletic ya Bilbao kwa majaribio, lakini wakala wake akashauri mchezaji huyo aanzie timu ya Daraja la Kwanza Hispania ili kupata nafasi ya kucheza na kuinuka haraka.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Big up Farid ndo daraja la kutokea Hilo kikubwa kukaza

    ReplyDelete
  2. Hongera Farid Musa, Tenerife ni team nzuri sana. Miaka miwili iliyopita Newcastle United ilimnunua Mshambuliaji wake hatari Ayoze Perez kutoka Team hii ya Deportivo Tenerife so hata na wewe utatupiwa jicho na vilabu vikubwa nw.

    ReplyDelete

Top Post Ad