VIDEO: Miaka 13 Baada ya Cameroon Kumpoteza Foe, leo Tena Wamempoteza staa Mwingine Uwanjani

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Kama ni mfuatiliaji mzuri wa mitandao ya soka barani Ulaya huenda utakuwa umekutana na taarifa za kusikitisha kwa taifa la Cameroon, usiku wa May 6 2016 Cameroon na Afrika  kwa ujumla ilipata taarifa za kushtusha, baada ya kupokea taarifa za kifo cha kiungo wa kimataifa wa Cameroon aliyekuwa anaicheze Dinamo Bucuresti Patrick Ekeng.

Ekeng amefariki baada ya kuanguka uwanja dakika ya 70 wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Romania uliokuwa unahusisha klabu yake ya Dinamo Bucuresti  dhidi ya Viitorul, mchezo ambao ulikuwa unarushwa live kwenye TV, tukio la Ekeng kuanguka limetokea wakati akiwa kasimama peke yake bila ya mpira.


Taarifa za kifo cha Ekeng ambaye zilithibitishwa masaa mawili baada ya kufikishwa hospitali, zinakuja baada ya miaka 13 toka Cameroon impoteze kiungo wake Marc-Vivien Foe kwa stahili kama hiyo, tukio ambalo lilitokea June 26 2003 wakati wa michuano ya Kombe la mabara iliyokuwa inafanyika Ufaransa na mchezo ulikuwa dhidi ya Colombia.


Ekeng alizaliwa March 26 1990 na amefariki akiwa na umri wa miaka 26 baada ya kuanguka uwanjani, Ekeng ndio alikuwa kaanza kupata nafasi katika kikosi cha timu ya taifa ya Cameroon ya wakubwa, muda mchache baada ya taarifa za kifo chake kuthibitika, mastaa wa soka walianza kupost na kuonesha huzuni kwa taarifa hizo.

Video ya tukio la kuanguka kwake na kupoteza maisha

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad