Exclusive: Wastara Juma Anasa Ujauzito.......

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Exclusive! Habari mpya ya motomoto ni kwamba, staa wa sinema za Kibongo, Wastara Juma amenasa ujauzito, Risasi Jumamosi linakuwa la kwanza kukupa mchapo huu!
Ujauzito huo ni wa aliyekuwa mumewe, Sadifa Juma, mbunge wa Jimbo la Donge, Visiwani Zanzibar ambapo kitendo cha mimba hiyo kuwa ya mbunge, kimemsumbua Wastara hadi kuamua kuondoka ili akapate muda mzuri wa kutafakari nchini Msumbiji.

Taarifa kutoka kwa vyanzo, zinaeleza kuwa Wastara alipoondoka nchini, aliwaaga baadhi ya mastaa wenzake kuwa anakwenda kufuata biashara zake za nguo nchini humo lakini Risasi Jumamosi lilichimba na kupata ubuyu ulionyooka kuwa aliondoka nchini kwa ajili ya kwenda kutafakari ujauzito huo.

NDUGU AVUJISHA UBUYU KAMILI
Ndugu wa karibu na Wastara ambaye hakupenda jina lake lichorwe gazeti, amefunguka kuwa baada ya Wastara kuachika, aligundua ni mjamzito hivyo alichanganyikiwa na kuamua kwenda Msumbiji kwa ajili ya kutafakari zaidi ujauzito huo.
“Hakuwa na jinsi kwani akiangalia alishatoka kwa mwanaume, angewezaje kumwambia kuwa ana ujauzito wake? Akaamua kukimbilia huko kwa ajili ya kujipanga ingawa anavyoonekana anatamani amzalie mbunge huyo,” alisema ndugu huyo.

NDUGU AZIDI KUTIRIRIKA
Ndugu huyo alizidi kushusha ‘vesi’ kuwa mimba ya Wastara inasadikiwa kuwa na miezi miwili au mitatu kwani tangu aachane na mumewe huyo, alikuwa akiumwaumwa na wakati mwingine alikuwa akitapika hovyo ambapo mwanzo alificha lakini yalipomfika shingoni alifunguka.
“Alitufichaficha lakini baadaye akawa hana jinsi, akaona atueleze na sisi tumemshauri tu aende akapumzike na ajiandae kutuletea kiumbe kipya,” alisema ndugu huyo.
Baada ya habari hiyo kutua Risasi Jumamosi,  Wastara alitafutwa kwa njia ya simu ya mkononi, akafunguka:

“Dah! Sijui niseme nini, kiukweli watu wanaongea sana, nimeondoka nchini kwa shughuli zangu binafsi lakini maneno ni mengi, wewe si wa kwanza kunipigia simu. Sikutaka kuongea kabisa juu ya masuala yangu ya ndoa iliyopita wala maisha yangu kwa jumla.”

Risasi Jumamosi: Kwa nini unaongea hivyo wewe funguka swali nililokuuliza, una ujauzito au la?
Wastara: Ndiyo, kwani cha ajabu ni nini? Yule niliyekuwa nalala naye si shangazi yangu, kila mtu anajua niliolewa na aliyenioa (Sadifa) wala si mjomba wangu.

TUJIKUMBUSHE
Wastara aliachika Aprili, mwaka huu baada ya kufunga ndoa na Mbunge wa Jimbo la Donge, Sadifa Juma ambapo ndoa yao ilidumu kwa muda kwa miezi mitatu tu na kuvunjika.

GPL
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mmmh,watoto 4 na kila mmoja na baba yake,kwa umri huo usipoangalia watafika 7.Ushauri,kama ni kweli ukiolewa tena olewa na mtu ambaye hana haja na watoto.

    ReplyDelete
  2. Wastara ndiyo kitu ulichokifuata kwa mbunge kuolewa na mbunge mwenye pesa halafu kunasa ujauzito na kuamua kumuacha sababu unajua itabidi awe anakupa hela ya matumizi ya mtoto kila mwezi hela itaingia, hayo mambo yanatokea sana Marekani wanawake wanazaa makusudi na wasanii wakubwa wenye pesa halafu wanatafuta sababu za kuwasepa ili waweze kupata hela ya matumizi ya kulea mtoto kila mwezi, mambo hayo yalimkuta Chris Brown bahati nzuri alishinda kesi yeye ndiyo akaonekana ndiyo mlezi wa mtoto wake kwa hiyo mama mtoto hakupata kile alichokuwa anataka,wewe Wastara usingehitaji kuongea kuwa umenasa ujauzito kwenye social media hata kama uliulizwa swali na paparazi umefanya hivyo makusudi ili mbunge ajue kuwa wewe ni mjamzito, kwanza utanasaje ujauzito kwa kuolewa kwa muda wa miezi mitatu tu na mtu ambaye hata ulikuwa humjui vizuri, hapo inaelekea wazi tu ulifuata ujauzito kwa mbunge wala siyo kitu kingine

    ReplyDelete
    Replies
    1. unaropoka mipovu mingi mdomoni mambo yenyewe ya udaku! kwani hata akihudumiwa wewe inakuumia nini kwani inatoka mfukoni mwako??? mwe pole mbunge mwenyewe wa kutoa huduma yuko wapi?? acha roho ya korosho bi kidude!!

      Delete
    2. ndiyo naropoka kila mtu anajua Wastara ana tamaa ya hela arijaribu yeye mwenyewe kuwa mbunge lakini ikashindikana, na mume wake wa zamani alipofariki Wastara akaenda social media kusema kuwa anataka kuolewa na mtu tajili mwenye pesa zake sababu anataka kuendesha magari ya kifahari unakumbuka? watu walimsema vibaya sana kwa kutamka kitu kama kile wakati mume wake wa zamani alipofariki, nazani Wastara alimroga mume wake wake wa zamani maana mpaka leo haijafahamika kuwa mume wake wa zamani alikufa kwa kitu gani, hata huyo mbunge alishtuka kuwa Wastara anataka kumroga ndiyo maana jamaa akamuacha, Waarabu ni wachawi sana mambo ya kuroga wanayajua sana

      Delete
    3. Huyo mwenye kutoa povu hapo juu ni wastara mwenyewe,achana nae,kashaona sifa kwa ustaa wa kubadilisha wanaume kila mwaka.

      Delete
  3. Pole bi mkora nilifikiri
    Utalea watoto na kuuguza miguu
    Haya mimba kulikoni
    Pole

    ReplyDelete

Top Post Ad