Lowassa Amwandikia Waraka Mzito Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Ernest Mangu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Waziri Mkuu wa Zamani, Edward Lowassa ambaye pia alikuwa mgombea urais kwa tiketi ya Chadema akiungwa mkono na vyama vya upinzani vinavyounda Ukawa, jana alimuandikia waraka Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Ernest Mangu.

Waraka huo ulijikita katika maagizo ya Jeshi hilo kupiga marufuku mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa pamoja na kuwashikilia na kuwahoji viongozi wa vyama hivyo akiwemo mwenyekiti wake, Freeman Mbowe hivi karibuni.

Lowassa alimueleza IGP kuwa amelazimika kumuandikia barua hiyo ili kuweka kumbukumbu sahihi baada ya kupata taarifa za kuzuiwa kwa viongozi wa Chadema kufanya mikutano wakati yeye alipokuwa nje ya nchi.

Alihoji sababu za kiintelijensia zinazotolewa na jeshi hilo kuzuia mikutano hiyo kwa madai kuwa limebaini kuna uwezekano wa kutokea vurugu zimetumika ili kuhalalisha uminywaji wa demokrasia ya vyama vya siasa kwani hata historia inaonesha vinginevyo.

“Uzoefu wa historia unakinzana na madai hayo, kwa sababu yako matukio mengi ambayo yamethibitisha kwamba mijumuiko ya wanasiasa wa vyama vya upinzani, yakiwemo maandamano na hata mikutano ya hadhara yamefanyika kwa amani,” alisema.

“Iko mifano mingi inayoonesha kwamba tumefanya shughuli mbalimbali za siasa kwa maana ya maandamano na mikutano ya hadhara kwa amani na pasipo kuwapo hata ulinzi wa polisi,” alisema Lowassa kwenye waraka huo.

Alisema kuwa sababu hizo ndizo zinazopelekea wao kupinga maagizo hayo ya polisi ya kuzuia kufanyika kwa mikutano kwa kuwa sababu za kiintelijensi zinatumika kama kichaka cha misukumo iliyo nyuma ya maagizo hayo.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. anasaini kitabu cha maombolezo au anaandika barua?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hiyo ni picha tu jamaa...

      Delete
  2. mwandishi nenda shule

    ReplyDelete
  3. Ahhh!! Lowassa wewe Si uligonbea kiti cha Uraisi Na unaweza kuandika hivi!! Tutaaninije Kama ndiyo wewe?? Maanake Ni utumbo Na hakuna maintiki wala Uzalendo au kwa ajili ya heshimma waliokupa sasa unalipa fadhila zao???? Lowassa hwbu rudia kuisoma Na ujiulize wananchi wataipokea vipi?? Maanake Mimi nakushangaa!!

    ReplyDelete
  4. kweli wewe Lowassa mimi nilikuwa nakuona umewiva.. lakini 😎 hapa umechemsha na haii ingii akilini ila kama una fikiria kuwa Dj Mbowe ataona hauumpi tafu wakati kama huu hapo tunaweza kukuelewa kwamba unalimda masilahi yako ya kibinafsi..au sivyo???? Inasikitisha

    ReplyDelete

Top Post Ad