Mafanikio yangu yanampa stress Shilole – Nuh Mziwanda

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Nuh Mziwanda na Mpenzi wake Mpya
Vita vya maneno kati ya Nuh Mziwanda na ex wake Shilole haviishi.

Hata hivyo ni Nuh Mziwanda ndiye anayeonekana kuendelea kurusha makombora mengi zaidi kumzidi mwenzake.

Kwenye mahojiano na kipindi cha Super Mega cha Kings FM ya Njombe kinachoendeshwa na Divine Kweka, Nuh ameibuka na jingine kuwa kusema kuwa mafanikio aliyonayo sasa yanampa stress Shishi.

“Haamini ndani ya moyo wake ndio maana ameanza kupanick, lakini inabidi akubali matokeo kuwa mimi ni mwanamuziki na yeye ni mcheza show,” alisema Nuh.

Muimbaji huyo wa Jike Shupa amedai kuwa baada ya kuachana, Shilole aliamini kuwa maisha yatamwendekea kombo Nuh. Hata hivyo Nuh anasema anatamani ex wake huyo asingekuwa na kinyongo naye kwakuwa kila mmoja kwa sasa ana maisha yake na asiendelee kutaka kushindana naye.

Kwa upande mwingine, Nuh amesema girlfriend wake wa sasa ni wife material na atamuoa.


Tayari wawili hao wameshajichora tattoo za majina yao kuashiria kuwa wanapendana kwa dhati. Nuh amesema anadhani anaweza kuwa amempata ‘the one.’

“Kiukweli hapa nimefika,” alisema.

Nuh aliwahi kumvisha pete Shilole na kujichora tattoo ya jina lake ambayo hadi sasa anayo.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Nuhu kweli ulikua bado una mpenda X wako kila kukicha lazima useme neno juu yake,,,hebu move on na maendeleo yako acha kuzungumzia x wako kila wakati.

    ReplyDelete

Top Post Ad