Nuh Mziwanda Amuumbua Upya Shilole

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Msanii anayefanya poa kwenye Bongo Fleva, Naftal Mlawa ‘Nuh Mziwanda’ amemuumbua upya aliyekuwa mwandani wake, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ kwa kuanika A-Z ya namna alivyokuwa anamnyanyasa kwenye uhusiano wao wa kimapenzi kiasi cha kuamua kuachana naye. Wikenda limeinyaka.

Akizungumza na Wikienda mara baada ya kuachia video ya wimbo wake mpya wa Jike Shupa huku ndani yake akigusia kiduchu figisufigisu alizokutana nazo kwenye uhusiano huo akimtumia mrembo anayefanana na Shilole ‘Shilole bandia’.

Nuh aliliambia gazeti hili kuwa alishindwa kustahimili kuacha matukio ya uhusiano wake yapite hivihivi bila kuyagusia kidogo kwenye wimbo wake huo kwa sababu alihisi watu hawamuelewi kile alichokuwa anakisema juu ya Shilole.

“Nimeamua kufanya hivi ili Watanzania waone jinsi Shilole alivyokuwa ananifanyia kupitia mtiririko wa matukio kwenye kichupa changu. Kiukweli inaumiza sana lakini hivyo ndivyo roho yake ilivyo, sijali ataumbuka kwa kiasi gani lakini hizo ni hisia zangu ambazo nimeamua kuziweka upya,” alisema Nuh huku akiongeza kuwa kwa sasa yuko kwenye uhusiano na mwanadada aitwaye Nawal.

Hata hivyo, baada ya gazeti hili kuchonga na Nuh lilimtafuta Shilole ambaye alipoulizwa juu ya sakata hilo alidai kuwa hataki kumzungumzia Nuh wala kusikia habari zake maana hata video yenyewe hawezi kuiangalia.

“Sitaki kusungumzia habari za mtu mwingine, no coment, labda kama kuna ishu nyingine unaweza
kuniambia,” alisema Shilole. Shilole na Nuh waliachana miezi kadhaa iliyopita ambapo mrembo huyo alidai alikuwa akimlea jamaa huyo hivyo Nuh naye ameamua kueleza ukweli namna ambavyo Shilole aligeuka mwanamasumbwi ndani ya nyumba.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. wewe Nuh, yaani kila kukicha mara Shilole hivi mara hivi, inaelekea una akili ya kitoto sana ndiyo maana Shilole amekushit, mwenzio Shilole ana akili ya kiustarabu ameamua kunyamaza kimya, umesema unaye demu mwingine sasa endelea na maisha yako na huyo demu mpya na siyo kazi ya kumtaja Shilole kila kukicha mpaka kumuimba kwenye video inaonekana bado unampenda Shilole unatamani jinsi alivyokuwa anakulea kama mtoto mdogo, sasa huna wa kukulea ndiyo maana unalilia hovyo kwenye social media, tumekuchoka sasa inatosha mpaka inaboa

    ReplyDelete
  2. its good that you wake its not too late you are still young and you have long way to go achana na mtu ambae hata kwenye karata hayupu big bro my prayers are with you

    ReplyDelete

Top Post Ad