Sinema ya Ukawa, Dk Tulia yaendelea

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Wabunge wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), wameendelea kususia vikao vinavyoendeshwa na Naibu Spika, Dk Tulia Ackson.

Jana, wabunge hao walitoka kwa muda katika Ukumbi wa Pius Msekwa wakati naibu spika huyo alipokuwa akifungua semina kuhusu ubia kati ya sekta binafsi na umma (PPP) na walirejea muda mfupi baada ya kumaliza kusoma hotuba yake na kumwachia Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti, Josephat Kandege kuongoza.

Hata hivyo, waliporejea walikaa upande mmoja wa ukumbi huo wakijitenga na wabunge wa CCM na baada ya kumaliza semina hiyo, wabunge hao walionekana wakikwepa kusalimiana na wenzao wa CCM.

Akizungumzia kitendo hicho, Mwenyekiti Mwenza wa Ukawa, James Mbatia alisema, “Wabunge wote wa Ukawa huwa tunaenda katika kamati, hilo hatujalikataa, tuliyokataa ni mambo ya michezo, ya kushiriki katika kantini, kusalimiana na vikao vyote vinavyoendeshwa na Dk Tulia,” alisema Mbatia.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kazi ipo
    Magufuli vunja bunge

    ReplyDelete
  2. Ionachusha ukawa!!

    ReplyDelete
  3. Me ni ukawa ila hicho mnachokifanya ni utoto na upuuzi mkubwa. Nawachikia sana mnaleta uhasama wa vyama mkitoka huko c mtakuja kwa udini na ukabila. Hicho sicho tulichowatuma. Kama mmefikia hapo basi na posho msichukue kwani walipa kodi ni sote cc ukawa na Ccm sasa posho ni pesa ya walipa kodi. Huo ni uchochezi mnafanya nyie akina mbowe na mwisho wake c Mzuri. Watanzania wenzangu tusiwafuate hawa viongozi wanamaslahi yao binafc ila wengine ni bendera fuata upepo wenye maslahi wasitufanye wajinga.tumewachoka kwahili hakuna chama wala udini tukemeeni ujinga huu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ukawa wewe
      Ukawa wa ccm unayeropka Kama lile teja lenye ufunguo wa posta chini

      Delete
    2. Posho, Posho ... POSHO ... Unacheza na Shombo la Posho... Inakatwa... Filimbi nyingi!! mwisho utarudi ndani kuokoa Posho.. Lakini Jua kuwa hii ni pesa ya mlipa kodi.. ambae sasa amesha istukia Hakuna Nguvu Jaso nHAKUNA MALIPO.. MPO NDUGU ZETU???????

      Delete
    3. Posho, Posho ... POSHO ... Unacheza na Shombo la Posho... Inakatwa... Filimbi nyingi!! mwisho utarudi ndani kuokoa Posho.. Lakini Jua kuwa hii ni pesa ya mlipa kodi.. ambae sasa amesha istukia Hakuna Nguvu Jaso nHAKUNA MALIPO.. MPO NDUGU ZETU???????

      Delete

Top Post Ad