Breaking News Wakurugenzi wote wa NSSF wamesimamishwa kazi, kupisha uchunguzi wa idara zao katika shirika hilo.

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

BODI ya wakurugenzi ya Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF), limewasimamisha kazi wakurugenzi sita na meneja watano na Mhandisi mmoja kufuatia matumizi mabaya ya ofisi na kutofuata sheria na kanuni.

Kwa mujibu wa taafia iliyotolewa leo na Mkurugnezi Mkuu wa NSSF,  Profesa Godius Kahyarara imesema hatua ya kuwasimamisha kazi wakurugenzi na mamenja hao inafuatia kikao cha bodi chini ya uenyekiti wa  Prefesa Samweli Wangwe kilichokaa kuanzia Ijumaa iliyopita.

“Bodi imeagiza  kusimamishwa kazi Wakurugenzi , Mameneja watano na Mhandishi mmoja ili kupisha uchunguzi ili kubaini wahusika katika tuhuma za ubadhirifu, matumizi mabaya ya ofisi na kutofuata kanuni, sheria na utatibu katika uwekezaji,  usimamizi wa miradi na manunuzi ya ardhi na ajira,” alisema Profesa Kahyarara.

Aliwataja wakurugenzi hao ni Mkurugenzi wa mipango, Uwekezaji na Miradi, Yakub Kidura, Mkurugenzi wa fedha, Ludovick Mrosso, Mkurugenzi wa rasilimali watu na utawala, Chiku Matessa, Mkurugenzi wa Udhibiti,Hadhara na Majanga, Sadi Shemliwa, Mkurugenzi Mahesabu ya ndani, Pauline Mtunda na Mkurugenzi wa Uendeshaji,  Crescentius Magori.

Aidha Aliwataja mameneja waliosimamishwa ni pamoja na Meneja wa utawala, Amina Abdallah, Meneja wa Uwekezaji, Abdallah Mseli, Meneja Miradi, Mhadisi,John Msemo, Mhasibu Mkuu, Davis Kalanje, Meneja kiongozi mkoa wa Temeke, Wakili,  Chedrick Komba na Mhadisi John Ndazi.

Awali amedaiwa kuwa baadhi ya wakurugenzi na mameneja waliosimamishwa, leo wamefikishwa katika kituo cha polisi cha kati Dar es Salaam kwa mahojiano kufuatia tuhuma hizi zinazowakabili.

a wakurugenzi wote wa NSSF wamepigwa chini leo na wanne kati yao wako chini ya ulinzi.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Wajibika kiuadilifu Na uaminifu..vinginevyo hatutaelewana..hasa kiujanja ujanja

    ReplyDelete
  2. Eeeh safi sana,ukilima matembele utavuna matembele.Wizi huleta
    maringo,uchoyo,ujeuri,ndivyo wengi kati ya hao walivyokuwa kumbe dhambi ya kuiba ndio ilikuwa inazaa yote hayo.Sio wote,lakini watakaowajibishwa wala msiwe na shaka kuna mahakama ya mafisadi yaani ni nzuri kweli kwa ajili yenu.

    ReplyDelete

Top Post Ad