Kosa Moja Linaposahaulisha Mazuri 100 Uliyoyafanya – Mkasa wa Zamaradi na Shoga

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Jumanne hii kwenye kipindi chake cha Take One, alirusha mahojiano na mwanaume anayejihusisha na mapenzi ya jinsia moja, tena aliyekubuhu na ambaye maisha hayo kwake ameyakubali na anayafurahia. Hicho kimekuwa kipindi controversial kuliko vyote vilivyowahi kurushwa Clouds TV.

Kuna sababu kadhaa kwanini wananchi wengi hawajapendezwa na kipindi hicho. Kubwa na muhimu kabisa, ni kuwa mjadala wa ushoga kwenye vyombo vyetu vya habari hasa redio na runinga bado inatia ukakasi mkubwa kwa wasikiliza/watazamaji. Kwa maadili na mila zetu, shoga ni mtu anayetia hata aibu kumuona akipita mtaani, seuze akihojiwa kwenye runinga ya taifa akijieleza kwa madaha anavyotembea na wanaume wenziwe, wa kila aina.

Mijadala ya ushoga kwenye redio na TV za Tanzania ni sawa na mtoto wa kiume kuongelea mapenzi na mama yake mzazi. Inakera masikioni, wanaudhi machoni na kwa kipindi kama kile kinachoruka saa tatu usiku, muda ambao familia nyingi zinakuwa zimekusanyika sebuleni baada ya chakula cha usiku ni aibu kubwa.

Ninaamini kuwa wengi walihamisha stesheni zao kuepuka fedheha ya kumuona mtu huyo akihojiwa kama si kutamani kujificha uvunguni kwa aibu.

Jambo la pili ni ‘timing’ ya kurushwa kwa kipindi hicho. Mwezi Mtukufu wa Ramadhan kwa waislamu ni mwezi muhimu mno. Ni mwezi wanaoutumia kurekebisha mienendo yao, kutubu dhambi zao na kuwa karibu zaidi Mungu. Hivyo kwa kurushwa kipindi kama hicho katika mwezi huu, ilikuwa ni sawa na kukiwekea kidonda chumvi.

THE MEANS DOES NOT JUSTIFY THE END!

Dhumuni la Zamaradi kukirusha kipindi hicho lilikuwa zuri na muhimu mno. Hiyo ni tabia inayokera wengi na ongezeko la vitendo hivyo linatisha. Mtangazaji huyo aliandaa kipindi hicho kutaka kujua chimbuko lake. Kwa maelezo yake alidai muda wa kunyamazia tatizo hilo umepita na ni muda wa kulizungumza bila kificho.

Lakini wakati mwingine njia inayotumika haihalalishi nia njema. Ndio maana pamoja na Zamaradi kueleza kwa kina kwanini aliamua kumhoji jamaa huyo, bado watu hawamwelewi kwasababu ukweli ni kwamba muda wa kuiweka mijadala ya aina hiyo kwa Tanzania haujafika.

Bado ushoga ni kitu cha aibu kukisikia kikijadiliwa. Na jambo baya zaidi ni kuwa shoga huyo alipewa muda mwingi wa kujieleza na kuonesha ufahari wake. Kwake yeye, maisha hayo ni sawa na kwa wengi hiyo ndiyo ilikuwa tafsiri ya kipindi hicho – kwamba kiliuza zaidi dhana ya ushoga badala ya kuikemea kwa kumwalika mtu anayejutia kujiingiza kwenye tabia hiyo ili iwe funzo kwa jamii.

Mwanazuoni mmoja wa masuala ya habari ameandika:

Kwanza,nikili wazi kumualika shoga kwenye kipindi,kama tunavyoshuhudia wanaotumia madawa ya kulevya,si kosa, kosa unamualika aje kufanya nini? Unakwenda kumuuliza nini? Unataka peleka ujumbe gani? Kama unamualika kwa nia ya kuhakikisha anaeleza madhara ya anachokifanya,kwa nia ya kuonesha ubaya wa mchezo huu ili jamii ichukue tahadhari,hakuna shida.

Nimebahatika kukiona hicho kipindi kupitia mitandao ya kijamii,na kuona mapungufu yafuatayo.

1. Mtangazaji alimuachia muda mwingi mgeni wake kueleza jinsi anavyofurahia mazingira ya mchezo huo mchafu,alitumia mbinu dhaifu ya kufanya mahojiano (space interview) wakati kwa mazingira yale alitakiwa kutumia mbinu ya ‘shotgun.’ Tunatakiwa kutumia shotgun pale unapokuwa huna imani na mgeni wako, bahati mbaya Zamaradi aliacha kutumia mbinu hii akatumia ‘space interview’ matokeo yake mgeni akatumia mwanya huo kuharibu kipindi na kuharibu nia njema ya mtangazaji ambayo kwa jinsi nilivyomsikia,asubuhi alisema alilenga kuwaelimisha wazazi juu ya umuhimu wa kumnasua mtoto na hatari. Zamaradi alitakiwa kutumia shotgun ili kutompa nafasi ya kuupamba ushoga kama alivyofanya.

2.Nadhani mtangazaji hakutafakari kabla ni aina gani ya mahojiano anakwenda kuyafanya,siku zote aina ya mahojiano ndiyo huamua aina ya maswali na mbinu za kuuliza. Kama Zamaradi alilenga kuandaa kipindi kinachotaka kuhakikisha ushoga unapigwa vita na kutokomezwa, aina hiyo ya mahojiano huitwa CRITIC INTERVIEW. Aina hii ya mahojiano humtaka mtangazaji kuwa critical kwa mgeni wake na mada. Anatakiwa kumbana mgeni kwa kumuonesha ubaya wa anachokifanya.

ZAMARADI BADO NI MTANGAZAJI BORA WA TV

Maisha yana changamoto nyingi sana na wakati mwingine huja kwa kushtukiza kabisa. Leo hii Zamaradi anaandamwa kwa matusi na kejeli kwenye mitandao wa kijamii kwa kuteleza mara moja kwenye kitu ambacho alipanga kwa nia njema.

Wanasema vyombo vya habari ni ‘mbwa mlinzi’ ama watchdog – kwa maana kwamba hutumika pia kulinda masuala muhimu kwenye jamii. Zamaradi alitumia kipindi hicho kama njia moja wapo ya kutafuta suluhisho la janga hilo na jinsi ya kuwanusuru watoto wetu. Bahati mbaya njia aliyotumia imeleta mrejesho hasi, tofauti kabisa na matarajio yake, na tayari madhara yameonekana.

Zamaradi anafahamika kwa uwezo wake mkubwa katika tasnia hiyo na sisi ni mashahidi, kipindi cha Take One ni miongoni mwa vipindi bora kwenye TV. Juzi tu kabla ya hapo alimwalika Sheikh Kipozeo, ambaye licha ya visa vyake, alitoa mawaidha muhimu kwa waislamu katika mwezi huu wa Ramadhan. Tusimlaumu tu Zamaradi kuteleza mara moja, bali pia tumkumbuke na kumtetea kwa mazuri 100 aliyoyafanya.

TCRA ISITOE ADHABU KWA SHINIKIZO LA WANANCHI, BALI KWA KUZINGATIA NIA HALISI YA KIPINDI HICHO

Kupitia akaunti yake ya Twitter, mamlaka ya mawasiliano Tanzania imeandika: TCRA imepokea malalamiko Kuhusu kipindi kilichorushwa na Clouds TV cha Take1. Kamati ya Maudhui inalifanyia kazi na maamuzi yatatolewa.

Nafahamu kuwa mamlaka hiyo imepokea malalamiko mengi sana kuhusu kipindi hicho na naelewa kuwa ‘kutokujua kosa si kinga katika mambo ya sheria’ lakini ningeshauri ipitie shauri hili kwa kuzingatia nia halisi ya kurushwa kipindi hicho na kutohukumu kwa pressure ya wananchi na madhara yaliyotokea.

FUNZO

Sisi tuliopo kwenye tasnia ya habari tutambue kuwa hakuna mada bomu kama ya ushoga, tuiepuke kwa uwezo wetu wote na kama kuna ulazima wa kuiongelea basi tuwe makini sana.

Pole Zamaradi, hayo ndio machangu ya fani hii ya habari.

Imeandikwa na Fred Bundala
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. the all issue of gay community is not the matter of who is right or wrong,firstly i would like to congratulate zamaradi to take a huge decision to air the most considered immoral fact in our country (Tanzania) and most countries in Africa the gay-ism is openly and wide practice in our country every gay or lesbian are known in our street community at lager but its not the fact that easly can spoken in open be it in churches,parliament,mosques,synagogue,schools,streets etc
    now its a time to speak about it and each and everyone lets take part and stop being jugmental gay peopele are human being like straight people why condemn them but also im not condoning the act or encouraging it but let get to know what is the core problem embedded and those who wish to educate them wether spritually or otherwise may begins to do so dont punish them by calling names or killing even jails gay person only God can judge stop be single minded community we have to hear the otherside too what if they suffering from food poisoning or medical or biological side effects or even social upbringing there are a lot going on on gay community take them as other human beings and treat them equally on God can judge
    im not a gay myself but i treat them as fellow human beings

    ReplyDelete
  2. JAMANI PAMOJA NA YOTE HAYO HAPO JUU UKWELI UNABAKI PALE PALE KUWA KILE KIPINDI HAKIKUFAA KUONYESHWA . KIMEKUWA KAMA NI KUUPROMOTE USHOGA. A

    ReplyDelete
  3. IMETUUDHI WENGI SANA,HALAFU PAMOJA NA KUSOMA MITANDAONI JINSI WATU WALIKERWA NA HILI JAMBO,ZAMA YUKO KIMYA TU,BASI HATA ANGESEMA SAMAHANI TU.INA MAANA KAONA POA?LAKINI SISHANGAI MAANA HAWA WANAOJIITA VIOO AU NYOTA SIJUI NDIO WA KWANZA KUALIKA HAO MASHOGA KWENYE SHUGHULI ZAO.(WANAWAPENDA)

    ReplyDelete
  4. Nasisitiza bado sijaona tatizo funzo lipo ktk kile kipindi...tatizo wa tz ni fuata mkondo tu

    ReplyDelete
  5. Nyiyi wa Tz mbona mna mambo!! Sisi huku ughaibuni mbona watu wa namna hiyo tunaishi nao,tunakula nao tunafanya nao kazi. Mtangazaji alicho kifanya hakina ubaya wowote. Swali la kujiuliza je mashoga wapo?? Kama wapo mimi na wewe wametukosea nini?? Si niwatu wazima, sasa shida iko wapi. Ngoja ni ulize swali unijibu utakavyo: Fisadi na shoga yupi bora, jambazi na shoga yupi bora,mtu unaye tembea nje ya ndoa na kuleta maganjwa ndani ya familia yako kipi bora. Mashoga walikuwepo tangu mwanzo na wataendelea kuwepo mpaka mwisho wa dunia. Kitu cha msingi jiombee wewe na familia yako na kila mtu atabeba mzigo wakw mwenyewe. Nafikili tumeelewana kama hatukuelewana shauri yako.

    ReplyDelete

Top Post Ad