Marufuku Watumishi wa Serikalini Kuwa na Tenda Serikalini

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI George Simbachawene amesema serikali tayari imekataza watumishi wa umma kujiingiza katika kuomba tenda mbalimbali za serikali na hawaruhusiwi na kama mtu anajihusisha na jambo hilo basi anakiuka misingi ya sheria

Waziri Simbachawene ameyasema hayo kwenye mahojiano maalumu na East Africa Radio kuhusu baadhi ya watendaji wa umma ambao wanamiliki kampuni ambazo zinashiriki kufanya tenda ya serikali na zimekuwa zikifanya vibaya na kusababisha malumbano baina ya wanachi na halmashauri mbalimbali nchini.

Amesema wamezuia swala hilo kisheria ili kuepuka usumbufu ambao umekuwa ukijirudia mara kwa mara pindi serikali ifanyapo ukaguzi wa utekelezaji wa kampuni hizo sambamba na kuwepo kwa malalamiko kutoka kwa wananchi kuhusu utendaji kazi wa kampuni hizo, ambazo zinakuwa zimepewa tenda na halmashauri mbalimbali nchini.

Amewataka wakurugenzi na viongozi wa mikoa kuzingatia sheria ya manunuzi inavyoelekeza na tayari wameanza uchunguzi kuwabaini watendaji wasio waaminifu juu ya swala hilo na pindi watakapogundulika kuhusika na swala hilo serikali itachukua hatua za kisheria.

Ametoa wito kwa watumishi wote wa serikali kutokujihusisha na swala hilo na wazingatie katika kusimamia haki na usawa kwa watanzania ambao ndiyo walipa kodi na watumiaji wa huduma mbalimbali za serikali.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad